sepema
JF-Expert Member
- Jun 13, 2019
- 591
- 1,000
Salaam waungwana, poleni na hongereni nyote mnaopambana kuutafuta mkate wenu wa kila siku.
Naomba niende kwenye mada.
Binadamu ama kiumbe yeyote iki awe katika ustawi unaotakiwa ni lazima apate mahitaji muhimu ya kumuwezesha kuishi. Miongoni mwa mahitaji muhimu kwa kiumbe hai ni chakula, mengine yatafuata baada ya shibe. Wanafunzi hasa wa ngazi ya shule za msingi na sekondari ni moja Kati ya viumbe hai hivyo nao suala la chakula sio lakupuuza kabisa.
Nimeshawishika kuandika haya baada ya kutembelea shule kadhaa huku wilayani kwangu nilipo. Picha niliyoipata nikwamba wanafunzi wengi hasa wa kutwa hawapati chakula cha mchana shuleni huku ratiba ya shule ikienda hadi saa 10 jioni. Nimebahatika kuongea na baadhi ya wanafunzi ambapo walieleza kuwa wengi wao wanaondoka nyumbani asubuhi bila kupata kitu chochote hali inayosababishwa na Hali ngumu ya maisha huko majumbani kwao.
Watoto hawa wanaambiwa na wazazi wao wavumilie hadi jioni wakirudi nyumbani watakuta chakula ambacho pia hakina uhakika. Wanaeleza kuwa utimamu wa akili huanza kupotea kuanzia saa 4 asubuhi ambapo wengi husinzia madarasani. Changamoto hii imeathiri maendeleo yao kitaaluma Jambo linalosababisha kufanya vibaya kwenye mitihani yao. Nani alaumiwe, serikali au mzazi.? Wazazi wanadai hawana uwezo wakuchangia chakula cha mchana shuleni na wakati huo wanaamini hilo nijukumu la Serikali kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula wawapo shuleni.
Serikali nayo inahamasisha wazazi kuhakikisha watoto wao wanakula shuleni kwa kuwachangia. Serikali nayo inaamini hili nijukumu la mzazi sawa na lile la kununua kalamu, sare na madaftari. Wakati hizi pande mbili zinavutana kuhusu chakula tukumbuke kuwa huyu mwanafunzi anapoteza umakini wakusikiliza kuanzia saa 4 asubuhi.
Tutarudi na roho zetu?
NB: Sina picha za mtoto mwenye njaa.