Chakula cha Mama Ntilie ni kwaajili ya masikini

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,693
36,080
Sina mengi wakuu nawasalimu.

Hii misosi ya mama nitilie ni kwa ajili ya maskini.
  • Mabenchi machafu
  • Viti vimevunjika
  • Meza chafu, inzi wakutosha
  • Msosi sometimes unanuka moshi
  • Wahudumu wachafu
  • Customer care iko chini

Kula kwa mama nitilie ni umaskini au labda ukumbwe na dharuura.

Mchele wanapika ule wa 1100/-(wa bei ya mwisho)

Nyanya wanatumia yale masalo wanayouza mateja.

Chapati au maandazi ya mama nitilie viko chini ya kiwango.
 
Sina mengi wakuu nawasalimu.
Hii misosi ya mama nitilie ni kwaajili ya maskini.
Mabenchi machafu
Viti vimevunjika
Meza chafu, inzi wakutosha
Msosi sometimes unanuka moshi
Wahudumu wachafu
Customer care iko chini.
Kula kwa mama nitilie ni umaskini au labda ukumbwe na dharuura.
Sema huko ulipokula ndio wachafu mbona huku kwetu mamantilie wasafi bwana. Na misosi misafi wanatujali na vitambi vimetutoka
 
Lakini vinatutoa shavu mkuu Tena unapimiwa mzigo wakutosha Mboga Kama zoote yaani tunafaidi Sana

Ila ukienda kwenye hotel zenye hadhi msosi unapewa Kama umeomba Tena ukute hakijaiva vzr na wananyodo Sana wahudumu wahiyo mihotel
Mahotelini chakula ovyo vinatunzwa kwenye mafrizi
Kwa mama ntilie chakula fresh bei nafuu na nyongeza unapewa
 
Kwa Mama ntilie;
Msosi ni wa leoleo yaani Todayday
Kama haujashiba unaongezewa yaani mlo mmoja umebeba milo 3.
Wahudumu wanachukulika,
Bei ni rafiki yaani unakula kulingana na hela uliyonayo,
Unaweza ukakopeshwa msosi deileee na kulipa mwisho wa mwezi,

MWISHO;
Kuhusu uchafu ni huko unapokula wewe,
 
Sina mengi wakuu nawasalimu.
Hii misosi ya mama nitilie ni kwaajili ya maskini.
Mabenchi machafu
Viti vimevunjika
Meza chafu, inzi wakutosha
Msosi sometimes unanuka moshi
Wahudumu wachafu
Customer care iko chini.
Kula kwa mama nitilie ni umaskini au labda ukumbwe na dharuura.
Hapo unaweza kuta umeshindia kipande cha Chungwa, wacha ujinga
 
Huuu ni ukweli usiopingika mkuu,, Mama ntilie ni huduma kwa ajili ya makapuku, mwenye hela hawezi kula kwa mama ntilie.. Me nayesema hivi ni miongoni mwa mwa makapuku na ndo maana nasupport hv ni kutoka na ushuhuda was wazi kabisa nilionao..
Sisis makapuku pekee ndo tunakula kwa mama ntilie
 
Audio...hii I'd yako nyngne
 
Kuna watu watabisha ila huo ndo ukweli..

Tena wanapika chakula kibaya sana mpka unajiuliza hivi huyu mtu mme wake nyumban anampikia hivi hivi!?
 
Walinilisha ugali,baada ya lisaa tu mbele nikapoteza funguo aise nusu nife, chooni narudia mara kwa mara kama naingiza vocha kwenye simu ikanifikisha mpaka asubuhi niko hoi,kimenipoa kula kwa mama ntilie,ile asubuhi nikapata dawa za kuzuia kuharisha mambo yakakaa sawa.Ila nilikaa siku nne bila kupata choo Aisee.
Naunga mkono hoja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom