Chake ni Chake?

Chake ni Chake?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,266
Reaction score
44,691
CHAKE NI CHAKE

Kinachopita ni chake, hata kama si cha kwake,
Chochote kwake ni chake, hata kama cha mwenzake,
Ukicheka usicheke, akikipenda ni chake,
Yeye chake ni cha kwake, cha kwake si cha wenzake!

Kikipendeza ni chake, chake yeye chakwake,
Ukikiona kileke, usikitamani chake,
Macho mbele yapeleke, usigeuzie kwake,
Yeye chake ni cha kwake, cha kwake si cha wenzake!

Kiwe kitamu cha kwake, na vitamu vya wenzake
Vyote kwake ni vyake, ati yeye haki yake,
Ugonjwa wake ni wake, tiba ati vya wenzake!
Yeye chake ni cha kwake, cha kwake si cha wenzake!

Kina umbo uzuri chake, chake yeye peke yake,
Mara akishike shike, kuringishia wenzake,
Atakupiga mateke, ukikigusa cha kwake!
Yeye chake ni cha kwake, cha kwake si cha wenzake!

Vya wanyonge ni vyake, na vya matajiri vya kwake,
Si haramu huko kwake, vikizuka anga zake,
Toka Pemba Chakechake, hadi Kigoma Isike,
Yeye chake ni cha kwake, cha kwake si cha wenzake!

Kama vya wenzake vyake, halali kula vya kwake,
Haki haiwi ya kwake, kama siyo ya wenzake,
Akivila vya wenzake, vitaliwa na vya kwake,
Yeye chake ni cha kwake, cha kwake ni cha wenzake!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
good umejitahidi saana kama umetunga mwenyewe
 
Umenikumbusha malenga wa bara enzi zile RTD... Ngoja waje washairi wenzio wakujibu!

Chake si chako changu, si changu chawenzake chako.
 
Back
Top Bottom