Chagonja na sinema ya mwaka!

ccm mwaka huu wanahaha. Sinema bado nyingo kwenye foleni. Mwaka huu wameanza na sera ya Division six, wamekuja na Hio ya Tanga lakini haziuziki.

Kituko ni kwenda kupambana ma majambazi ambao waliitwa magaidi ukiwa kwenye shangingi. Nimeliona Jana ITV wakiwa na msafara wa mashangingi na Pick up kadhaa. Ni sinema za kitoto.
 


Naam, You may have point. Lakini yote hii ni ishara kwamba kila kukicha ufa ndani ya Tanzania unazidi kupanuka na ghadhabu miongoni mwa baadhi ya wananchi inaongezeka. Mimi na wewe, pamoja na watawala wetu, tunadhani hao ni wachache; hawatufanyi kitu! Lakini hawa ni wa-tz, swali ufa huu na ghadhabu hizi zimetoka wapi? mbona miaka michache hazikuwepo? Hivi, zimeanza lini hasa? Kila mmoja wetu ana jibu lake. Lakini Mwalimu alituonya katika uhai wake kuwa ni ujinga kudhani kuwa Tanzania ni tofauti na Somalia; kwa maana kwamba ipo "stable'. Alionya kuwa nchi za Kiafrika zote ni dhaifu sana kiasi kwamba kitu kidogo kinaweza kuwagawa wananchi na nchi ikasambaratika. Kwetu sisi hapa, hicho kitu kidogo kinachotugawa sasa ni ubinafsi wa wanasiasa wetu. Tufanye tafakuri ya kina; vinginevyo tutaumia sote kama jamii moja.
 
Mh! kwamba Tz ndo mwamba kuliko Nigeria ktk Africa au Kenya kias yakwamba hakuna Kikundi chochote cha kigaidi kinaweza kufanya vurumai?

Huo ni mtazamo wako tu mkuu. Amini issue hii iko serious.
Yaani factors zote zinazoifanya Boko haram iwepo hakuna hata moja TZ, halafu hivi kama hata hao alshabab wameshindwa kukaa kwenye ardhi ya Kenya zaidi ya kuvizia na kukimbia, wanalikimbia Jeshi disorganised kama Kenya halafu kikundi cha wahuni ambao hawajui hata dunia inaendaje kilisimamishe JWTZ kwa masaa 48? Kisha unasema hii issue ni serious, kwani serious kuliko bomu lililorushwa kwenye mkutano wa chadema halafu polisi wakawa wanamlinda mrushaji?
 
TUNTEMEKESang

Mheshimiwa usiitetee CCM, unless kama unajua unachokitetea. Toka mwaka 1995 CCM imekuwa ikitumia mbinu chafu kuwavuruga watz ili kibaki madarakani. Mwaka 1995 walivitumia vyombo vya habari kurusha picha za mauaji ya Rwanda na kuelezea kuwa Vyama vya upinzani vikichaguliwa vitaleta mauaji. Mwaka 2000 CCM walisimama kidete kupublish kuwa CUF ni chama cha kiislam huku wakijua kabisa kuwa hakuna chama cha kidini kinaweza kupata usajili nchini, walilitumia Polisi pia kuonesha kuwa CUF walikuwa na mpango wa kuleta vurugu.

Mwaka 2005 walitumia sana habari ya ukabila, wakiichafua chadema na mbowe kwa kusema chama ni cha wachagga na kwamba chadema ikishinda itakuwa balaa. Mwaka 2010 hilo kila mtu aliona jinsi ccm walivyoimarisha nguvu kubrand chadema kama chama cha kikristu na kuwa Slaa ni padre ambaye akishinda atasimamia ajenda za RC na propaganda hizi ziliambatana na matukio ya kuhatarisha usalama ili kuwakumbusha watu umuhimu wa kutowachagua wapinzani.

Ndio maana nasema Polisi kwasasa hawawezi kushawishi watu kwa sasa mpaka baada ya uchaguzi ndio sasa tunaweza kuongea lugha moja. Lakini vinginevyo hii itabaki ni mpango wa ccm na chagonja, maana naona movie inaelekea kuonesha kuwa kikundi hicho ndio kimekuwa kikiiba silaha za polisi kwaajili ya shughuli zao.
 
Last edited by a moderator:
Unajivamia,unajiteka,unajitorosha,unajisaka na hatimaye unatangaza kujitafuta kwa udi na uvumba.Matukio yote haya haya hayana majina ya waathirika.

Kweli siasa zimefikia mahala pake!Tutashuhudia mengi 2015.

Zinaibiwa silaha polisi halafu zinatangazwa kuwa zimeibiwa na magaidi halafu polisi wanapambana nao na kugundua kuwa silaha zilizoibiwa polisi zimejigeuza kuwa nzito na hivyo jeshi linaingilia kati na silaha nzito!! Sinema ya Mrundi!!
 

Mkuu sinema yoote ni kuwa silaha hizo zilizogeuka kuwa nzito za kivita ziliibiwa polisi!
 
CHAGONJWA muvi imeshitukiwa,aibu yenu aibu yao waliowaingiza mkenge(ccm).....bora ufilisike mali sio akili,mnakoelekea mtakuja mumteke tezi dume mseme magaidi
 

Mh! mimi si kiongozi. Ni raia tu kama wewe mkuu. Najaribu kutumia haki yangu ya msingi kueleza kile ninachokiamini juu ya jambo hili na mengneyo.

Ni bahati mbaya sana kila mtu ana uhuru wa kusema yanayomsibu na anayoona ni sahihi. Na ni katika uhuru huu ndipo watu hupindisha kwa maslah binafsi(tena bila hata sababu maalum).

Shime Watanzania. Nchi hii inahitaji mitazamo zaid ya ushabiki huu tunaojiingiza kwao.
Thnx!
 

Teh! mara ooh CHACHA WANGWE aliuawa na CDM?(naona hili ulilisahau Mkuu).

Lakini naamini hata kama si ktk matukio yote hayo, lakini kuna baadhi kabisa CDM imejihusisha nayo. Be it directly or indirectly.

Habari ya CDM kumuua Wangwe imekuja kutanabaishwa na Z.KABWE.

"Mlimuua Chacha Wangwe, mimi hamtaniweza"-Z.KABWE akiwaeleza CDM. Sasa sijui huyo naye ni CHAGONJA au aje!
 

Ubarikiwe sana Mkuu.

Tafakhur nzuri sana hii. Niwasihi wachangiaji wengine pia wajaribu kujikita ktk "constructive aspects" namna hii kuliko destructive & aggressive/arrogant ones!

Thnx!
 

Nakupongeza kwani umejibu kwa busara, lakini busara yako haitalisaidia taifa letu kwani wewe ni mmoja wapo ya watu ambao hata mambo yakiharibika huwa mnasema usibishane na serekali. Inakuwa kama serekali ni sehemu ambayo hata ikifanya kosa basi hupaswi kuionya. Na huwa najisikia vibaya sana ninapokutana na mtu anayekwepa wajibu wake kwa serekali tena kwa kutumia majibu ya busara kama yako. Watu kama nyinyi ndi mmechangia nchi yetu kuendeshwa kitapeli na kiujanjaujanja eti kisa ni serekali imeamua. Jitambue ndugu serekali ni wewe na unao wajibu mkubwa kuliko kuweka busara mahali unaona kodi zetu zinapotea bure. Hivi kama kweli sio unayechangia serekali kufanya ipendavyo, imegundulika walioko kule sio magaidi bali ni vibaka tu kama vibaka wengine kwanini itumike nguvu kubwa vile wakati zingeweza kwenda gari zisizozidi 3, yale mavx siku hizi yamekuwa magari yakivita? Unakwenda kupambana na gaidi ukiwa kwenye kiyoyozi!! Ndugu yangu jisikie aibu kutetea mambo yasiyo na tija. Ni kweli wewe umejaribu kuchomoka kwenye tundu la kusema ni ushabiki nakubaliana na wewe kabisa. Hivi si umesikia kuna hela zilichukuliwa kule stanbic kinyume na utaratibu? Ni madifender na mavx mangapi yamekwenda kujua hayo majina achia mbali hata kurudisha hizo hela. Unapoamua kuonyesha unatumia busara huoni kama umekuja kupotosha zaidi. Naomba dhamira yako ikusute kama wewe ni mkweli. Samahani kwa kukukwaza ndugu yangu. Ila tafakari na simamia ukweli.
 
Unajivamia, unajiteka, unajitorosha, unajisaka na hatimaye unatangaza kujitafuta kwa udi na uvumba. Matukio yote haya haya hayana majina ya waathirika.

Kweli siasa zimefikia mahala pake! Tutashuhudia mengi 2015.

Nimesikia pia wamejiua...
 
Umesahau mapanga ya IGP Mahita na hayo makontena? Kumbe mapanga hayo yalichorowa rangi na bendera ya CUF pale polisi Kilwa Road. Uchaguzi unakuja, elimu bure, matokeo ya kidato cha nne WOTE wamefaulu, MUNGU wangu nchi hii.........

kkarumekenge;
Ni lazima Watz tufunguke macho. Lazima tuelewe kuwa ccm wameshaona kuwa hawana njia tena ya kurudi kwenye dola. Wanatafuta kila njia ya kuifanya nchi ionekane kama haiwezekani kutawalika na haswa kwa rais ajaye hivyo wawape wanajeshi kuongoza.
Toka lini Jeshi popote likaenda ati kusimamia uchaguzi?? Kulikoni mpaka waletwe kusimamia uchaguzi? Mbona mgambo ni wengi tu, mbona JKT tunao kibao na wengine wanaandamana kuomba ajira si ndo hao wangepewa hiyo mihela wanayo gawana kwa masandalusi??
Wanatibua amani yetu kwa vyovyote ili ionekane hakuna amani Jeshi lipewe madaraka. Ole wenu maccm. Mmekwisha sera mnaleta ugomvi. Hakuna atakaye salimika.
 
Hii sio serikali ya kuipa ushirikiano hata kidogo jinsi walivvogeuza taifa kuwa lakizushi ni kuwakatalia kabisa Polisi kuendelea na sinema za kichina
 

Si kweli mkuu.

Kwamba kikundi kiundwe na Serikali kwa dhumuni la kuzuru na kuuwa Polisi & Wanajeshi?

Tuache "poor assumptions" jamani. Mwisho wa siku ni mimi na wewe ndio tutakaoteteleka in case tukibeza na kuchangia kuliangusha jeshi lisifanye kazi yake.

Nina ushahidi wa mahala fulani huku kwetu. Watu wamewanyima ushirikiano Polisi kuchunguza mauaji fulani kisa tu eti ni PoliCCM.

Let's go. Itafahamika tu.
 
Last edited by a moderator:
maneno hayo aliyasema baada tuu yakukabidhiwa sanduku lekundu lilojaa mafwedha, na wewe ukawa ndio msabazaji wa taarifa ulipotea kidogo baada ya kutoka kwenye pay roll ya Lumumba karibu
 
Hakuna anayengoja majibu labda wewe na co Lumumba product wote tunajua mchezo wa CCM umefika kikomo manake kila mtu anawajua uchaguzi ukikaribia wanakuja na mbinu za kuwatisha wananchi history lives kwa sasa wawadanganye wake zao, waume zao na wana wao sio watanzania kuchele kumekucha hakuna mamburulazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…