Kibona
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 1,023
- 652
Mkuu unapokuwa umeaminiwa na jamii kwa kiwango kama CCM ilivyokuwa imeaminiwa na watz basi inatakiwa uheshimu sana wanaokuamini, ulinde imani hiyo na uwe na mpango wa kuimarisha. Lakini ukianza kuitumia vibaya kwa maslahi binafsi ni wazi imani hiyo itatoweka na ikitoweka imani ya jamii kwako basi kila kitu huwa kigumu kwako.mangatara
Ninyi muishi tu kwa assumpitions hizohizo badala ya kustuka na kutoa ushirikiano kwa serikali,kalieni hayohayo kwamba ni mbinu zaCCM.
Tuombe uzima. Mtakiri tu kwamba ushabiki kama huo mnaoufanya hauna mantiki hata kidogo.
Take my words with a special regards. Nakuhakikishia jambo hilo.
Bahati mbaya CCM wanaendelea na tabia yao ya siasa za maji taka sasa wewe subiri mwisho wake, wanaccm ndio watakuwa waathirika nambari moja japo tutaathirika wengi pia. Yaani CCM wanataka waendelee kufanya madudu halafu watu wavumilie tu kwasababu eti mabadiliko yanaweza kuvunja amani, hicho kitu hakiwezekani na sasa inaonesha watu wanayahitaji mabadiliko bila kujali yatakuwa ya aina gani. Hivyo ccm walitakiwa kwasasa watii mahitaji ya jamii wasichelewe kama walivyochukua muda mrefu huko Zanzibar, na kimsingi rasimu ya warioba ndio ilikuwa mwanzo mzuri na walichotakiwa wakifanye ccm ni kuziongezea nguvu taasisi za muungano lakini sio kuvuruga structure nzima.