Kupiga chafya (sternutation) ni kitendo cha utowaji wa hewa kwa nguvu bila ya kutarajia (burst of air), kutoka kwenye mapafu kwa kupitia njia ya pua na mdomo. Kwa kawaida chafya inasababishwa na chembechembe ndogo sana ambazo uleta aina ya muwasho kwenye pua.
Wakati mwingine chafya inaweza kusababishwa na mwanga mkali wa taa, ukikupiga usoni, au aina fulani ya virusi (mafua), chafya pia upelekea kusambaa kwa aina ya maradhi, ndio maana huwa tunashauriwa tunapotaka kupiga chafya tuzuie kwa kuweka kitambaa karibu na mdomo au kuzuiya kwa kiganja cha mkono.
Upigaji wa chafya ujumuisha misuri mbali mbali ya kwenye mwili wa binadamu, ikiwemo misuri ya tumbo, misuri ya kifua, dayaflam (diaphragm), vile vile misuri ya koo bila kusahau misuri ya kwenye macho. Ndio maana upigaji wa chafya uendana na ufungaji wa macho.
Kwa hayo machache ni matumaini kuwa utakuwa umeelewa japo kidogo, sababu za upigaji chafya.