CHADEMA yetu ya mabadiliko ipo wapi?

CHADEMA yetu ya mabadiliko ipo wapi?

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
54,185
Reaction score
43,263
Wanaukumbi,

Tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020. Sioni ile nguvu ya Chadema iliyokuwa nayo miaka kumi iliyopita, Chadema ya mabadiliko, CHADEMA ya Maandamo kila kona.

Ni kitu gani kimetokea ndani ya Chadema, kinapoelekea naona kama kitakuwa kama TLP, naona wabunge wengi wanarudi CCM na wafuasi wao bila hamna tena mshikamano wa maandamano wala matamko ambayo tulikuwa tumeyazoea.

Viongozi wa juu ebu jitokezeni kuweka sawa hili jambo, naona hata wafuasi wa Chadema humu JF wamekata tamaa hawajui nini cha kufanya.

Hivi kweli kwa hili kuna matumaini tena ya kuwa chama kikuu cha upinzani au kuchukuwa dola?
 
Ritz,
Mwaipanya na Nusrat wako mahabusu singida kwa kuimba wimbo wa taifa, viongozi wakuu lissu na mbowe wamevunjwa miguu, halina mdee na bulaya wamevunjwa mikono, kamanda Mawazo na ben saanane wako kaburini
Alafu unauliza maswali ya kiupumbuvu kwa kejeli
 
Ni vigumu kusikia hayo unayoyataka kwanza hata vyombo vya habari haviruhusiwi kuonyesha au kurusha habari za wapinzani za kukosoa au kupinga chama tawala,na watakao fanya hivyo wanatishiwa kufutiwa license au kufungiwa, kwa awamu hii imekuwa ngumu kusikia habari za upinzani kwenye vyombo vya habari, vyombo vya habari vipo kusifia chama tawala na ni kweli hilo lime athiri Sana vyama pinzani, hata midahalo kwa Sasa haipo na ikiwepo ni kwa wanao sifia tu,unaweza rejea kipindi Cha ajenda 2020 Cha Mtozi Nyanda wa star tv je siku hizi wanakaribisha wageni wa aina gani!?

chadema hawawezi karibishwa toka akaribishwe mwenyekiti bavicha kipindi kikamriwa kufungwa.chadema nawakubali Mambo yanaendelea kimya kimya.
 
Hahaha Ritz! Karibu sana mkuu, Naona ulikimbia kwa miaka 5.

Ila kwa mwaka huu ndugu yangu jipangeni. Chadema ya sasa imekaa kimipango zaidi. Wanajua wapi Walikosea na wamejifunza sana. Jiandaeni kukabidhi nchi kwa Chadema hapo October
Mzee wa mtama kasha tuvurugia misheni yotedola haichukuliki,acha tu twahadae wafadhili mambo yaende.
 
Ki ukweli kuna sinto fahamu kubwa sana kwetu sisi wanachama, hatujui uongozi kwanini upo kimya?!
 
Wanaukumbi,

Tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020. Sioni ile nguvu ya Chadema iliyokuwa nayo miaka kumi iliyopita, Chadema ya mabadiliko, Chadema ya Maandamo kila kona.

Ni kitu gani kimetokea ndani ya Chadema, kinapoelekea naona kama kitakuwa kama TLP, naona wabunge wengi wanarudi CCM na wafuasi wao bila hamna tena mshikamano wa maandamano wala matamko ambayo tulikuwa tumeyazoea.

Viongozi wa juu ebu jitokezeni kuweka sawa hili jambo, naona hata wafuasi wa Chadema humu JF wamekata tamaa hawajui nini cha kufanya.

Hivi kweli kwa hili kuna matumaini tena ya kuwa chama kikuu cha upinzani au kuchukuwa dola?
Mkuu ulipotelea wapi. Karibu sana ukumbini
 
Wanaukumbi,

Tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020. Sioni ile nguvu ya Chadema iliyokuwa nayo miaka kumi iliyopita, Chadema ya mabadiliko, CHADEMA ya Maandamo kila kona.

Ni kitu gani kimetokea ndani ya Chadema, kinapoelekea naona kama kitakuwa kama TLP, naona wabunge wengi wanarudi CCM na wafuasi wao bila hamna tena mshikamano wa maandamano wala matamko ambayo tulikuwa tumeyazoea.

Viongozi wa juu ebu jitokezeni kuweka sawa hili jambo, naona hata wafuasi wa Chadema humu JF wamekata tamaa hawajui nini cha kufanya.

Hivi kweli kwa hili kuna matumaini tena ya kuwa chama kikuu cha upinzani au kuchukuwa dola?

Naona umetoka jela na nguvu nyingine. Cdm sio chama cha kigaidi, sasa hivi cdm inafanya siasa dhidi ya polisi na kundi la watu wasiojulikana. Hivyo inabidi ili ifanye ulichokuwa unakiona hapo kabla, inabidi wamiliki silaha za kijeshi ili iweze kwenda sambamba na siasa hizo. Sasa ccm imekuwa chama cha pili kwa umaarufu, baada ya yesu wa chattle kujigeuza yeye ndio mihili ya nchi.

By nature yesu wa chattle hawezi siasa za ushindani, bali anahitaji kuabudiwa tu, na yoyote anayemkosoa anaishia jela, kuachiwa kilema cha maisha, kuhujumiwa shughuli zake za kujiingizia kipato nk. Kwa ujumla yesu wa chattle anaaminisha wananchi kuwa ukiwa na demokrasia, huwezi kupata maendeleo.
 
Back
Top Bottom