CHADEMA yazipelekea barua balozi za Marekani na Ujerumani kuhusu tuhuma za Musiba kwamba zinaihujumu Tanzania

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekwenda balozi za Marekani na Ujerumani kupeleka video zinazomuonyesha Cyprian Musiba akizituhumu nchi hizo kupanga mikakati ya kuhatarisha Usalama wa Taifa la Tanzania.

Akizungumza na JUPITA, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene amekiri chama chake kuandika barua yenye Kumbukumbu Nambari C/HQ/ADM/KS/24/02 iliyofika Ubalozi wa Marekani na yenye Kumbukumbu Nambari C/HQ/ADM/KS/24/01 iliyofikia Ubalozi wa Ujerumani,

Makene alisema barua ya Ujerumani ilielekezwa kwa Mkuu wa Kitengo cha Siasa na Uchumi, John Espinos huku ile ya Marekani ikielekezwa kwa Mkuu wa Kitengo cha Siasa na Uchumi wa nchi hiyo, Joerg Hererra.

“Tumeandika barua hizi tukizitaka nchi hizo zijibu tuhuma zilizoelekezwa kwao na Cyprian Musiba ambaye alisema Marekani kupitia FBI inaendesha mikakati ya kuhatarisha Usalama wa Tanzania.

“Lakini pia, Musiba alikihusisha chama tawala cha Ujerumani CDU kuwa kinashirikiana na Watanzania kula njama za kuhatarisha Usalama wa Taifa,” alisema Makene.

CHADEMA kupitia kwa Makene kimesema kiliguswa sana na tuhuma hizo na kikaona sio za kuzipuuza kwani ni tuhuma nzito na zisipofanyiwa kazi na kuachwa basi mipango hiyo inaweza kuliingiza taifa kwenye hatari kubwa huko mbeleni.

Makene anasema sambamba na barua hizo, pia chama chake kimeambatanisha CD za video zinazomuonyesha Musiba akiongea maneno hayo mbele ya vyombo vya habari Februari 25, 2018.
Sasa musiba ajiandae kuwa musiba wa Kweli maana anacheza na CIA
 
Chadema acheni siasa za kienyeji, kwanini huyo Msiba msimripoti kwenye taasisi za usalama ili kulisaidia taifa kwa taarifa alizonazo. Na badala ya kwenda kwenye hizo balozi wangeenda tu pale wizarani kwa Dr Mahiga!
mtuhumiwa ajichunguzi
hivi
upelelezi wa Lissu vipi
wa Ben Saanane je?

ndio vizuri
mbona mkuu kama unataka kuitetea sisiemu na serikali yake wakati Watuhumiwa CHADEMA wamejipeleka wenyewe kwa watuhumiwa wenzao?
 
Haha bavicha bwana, Balozi hazifanyi kazi kwa mashinikizo ya vyama vya kijasiriamali.
 
Dah, ina chadema ni wahaini. Lengo la hii move ni nini haswa?? Hata kama ni kweli, wanategemea marekani na ujerumani watasema ni kweli??
Uzalendo ni ishu pana sana, na hapa pia chadema wamekosa uzalendo. Bahati nzuri wazungu sio wajinga kivile kama wazee wa ufipa, watajua lengo la chadema ni nini.

Waliokosa uzalendo ni serikali kwa kunyamazia tuhuma nzito kama zile na kumwacha Musiba uraiani mpaka sasa! Kama hii habari ni ya kweli basi ni jambo jema sana kwani litailazimisha serikali kuingia uwanjani kuchukua hatua na kukemea watu wa sampuli ya Musiba! Kama kuna watu serikalini wako nyuma ya Musiba ndio watajuta kwamba siasa za majitaka hazilipi!
 
Mawazo ya kitoto haya.
 
Chadema acheni siasa za kienyeji, kwanini huyo Msiba msimripoti kwenye taasisi za usalama ili kulisaidia taifa kwa taarifa alizonazo. Na badala ya kwenda kwenye hizo balozi wangeenda tu pale wizarani kwa Dr Mahiga!
taayari polisi ilishasema inafanyia kazi ulitaka iweje?
 
Tangu lini ushahidi wa Chadema unapokelewa.
Na toka wameanza kulialia sihaona walipofanikiwakumfungulia kesi makonda-hola,ukuta-hola,kwenda the hegue-hola,mbowe kumshitaki makonda-hola,meya kunshtaki makonda-hola,lisu kuwashawishi UN-hola.....mwalimu kushinda ubunge-hola....
 
Back
Top Bottom