CHADEMA yazidi kutikisa UZINI Zazibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yazidi kutikisa UZINI Zazibar

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Molemo, Feb 7, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  IKIWA ni wiki ya lala salama ya kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la uwakilishi la Uzini, visiwani Zanzibar, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tayari kimefanya mikutano 68 ya kumnadi mgombea wake, Ali Mbarouk Mshimba.
  Hatua hiyo inatokana na chama hicho kufanya mikutano minane ya hadhara kila siku ili kuhakikisha jimbo hilo linatua mikononi mwake pamoja na kuwafikia wananchi wengi.Ni wazi kuwa chama hicho sasa kinatishia vyama viwili vya CCM na CUF na upo uwezekano mkubwa wa CHADEMA kunyakua jimbo hilo.
  Katika mkutano uliofanyika kwenye Shehia ya Pagali, kada wa CHADEMA, Mtera Mwampamba, aliwataka vijana kujiepusha na kasumba ya kubebwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye mikutano yake kwa ahadi ya kupatiwa ajira.
  Mwampamba alisema badala yake vijana hao wanatakiwa kukumbuka walichofanyiwa katika uchaguzi mkuu uliopita baada ya kubebwa na kupelekwa kisiwani Pemba ambapo wengi wao walirudi na vilema na wengine kupoteza maisha.
  Aliwataka vijana hao wasiwe na ugonjwa wa kusahau kiasi hicho, kwa kuwa hadi leo kati ya hao waliopelekwa, hakuna hata mmoja aliyepata ajira.
  Naye, Ofisa Mwandamizi wa Utafiti na Sera wa CHADEMA, Mwita Waitara, aliwataka wakazi wa Uzini kutosita kuitosa CCM, kwa kuwa katika miaka 48 iliyokaa madarakani hakuna maendeleo iliyowafanyia.
  Akitolea mfano alisema Uzini leo isingetakiwa kukosa huduma za maji ukizingatia kwamba Zanzibar pembe zote imezungukwa na maji, pia jimbo hilo halina shule wala zahanati, pamoja na kufahamika kuwa ndilo la pili katika harakati za kuleta mapinduzi.

  SOURCE:TANZANIA DAIMA

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  asante kwa taarifa
   
 3. T

  Tata JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,733
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280
  Majibu kwenye sanduku la kura. Hatutaki kusikia hadithi za CDM kulalamika kuchakachuliwa na CCM/CUF safari hii. Kama ni kura kwa udogo wa jimbo lenyewe mnaweza kabisa kuzilinda na kuhakikisha zote zinahesabiwa kwa haki na kutangazwa kama zilivyo.
   
 4. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,229
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  kwa zanzibar CDM wanacheza, sijui.. itakuwa ni maajabu ya Mwaka wakichukua jimbo. Hapo ndipo nitaamini sasa Maalim Seif kwisha kazi.
   
 5. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  peoples' powerrrrrrrrrrrr
   
 6. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  padri slaa na dj mbowe wamepakimbia kule
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mwendawazimu siku zote utamjua kwa anachoandika
   
 8. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Hivi huyu Mwita Waitara anajua anachoongea au na yeye analipukua tu kama Magamba?! Hivi anajua technology and cost ya kufanya DESALINATION of Ocean/sea water?

  Ndiyo Zanzaibar imezungukwa na maji lakini yale ni maji ya chumvi. Hata nchi zilizoendelea kama Japan haithubutu kufanya desalination of ocean water for domestic use insteady wametafuta vyanzo vinginevyo vya kupata maji ambayo siyo ya chumvi.

  Anataka kuwadanganya wana Uzini kwamba CDM ikipewa dola itaweza kufanya desalination of ocean water kuondoa tatizo la maji?

  Ama kweli all politician are alike. Ujinga wa wana Siasa tuukate out right, vinginevyo hata sisi wasomi tutaonekana bogus!
   
 9. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Big up... CDM.. Vivaaa..
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  chadema haiwezi kupata hata sheha huku zanzibar.huo ndio ukweli.
   
 11. l

  luckman JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  mfalme wa 16 unaumwa kifaduro!hivi unadhani dr na mwenyekiti kazi yao ni kampeni tu??? Unaumwa wewe!
   
 12. l

  luckman JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  kila kitu ni mipango wewe!hakuna kinachoshindikana!
   
 13. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  :nerd::poa:lol:
   
 14. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Acha kudanganya watu kwa kukariri mambo, Japan hawajashindwa bali hawajaamua, haiingii akilini Japan washindwe and then Cyprus waweze.
   
 15. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Zanzibar ina wenyewe chadema ipate umaarufu kutoka wapi? propaganda inapendeza kama inakaribiana na ukweli.
   
 16. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
   
 17. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #17
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Suala la Uzini na chadema linakuzwa wakati chadema haina jeuri ya kutamba znz, siasa za maji taka.
   
 18. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  tuambie kiwango chako cha usomi...
   
 19. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #19
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ili kuipenya zanzibar chadema wanahitaji propaganda ya juu sana na hii ni kati ya propaganda hiyo kwamba inakubarika zanzibar wakati ukweli haikubariki.
   
 20. M

  Molemo JF-Expert Member

  #20
  Feb 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Malaria sugu at work
   
Loading...