CHADEMA yawataka watanzania kubana matumizi

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Posts
7,533
Reaction score
22,288
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Vincent Mashinji amewataka wananchi kutumia fedha kwa umakini kwa kubana bajeti ya matumizi yao ili kuhakikisha wanaweza kumudu hali ya maisha kwa sasa.

Dkt. Vincent Mashinji Akijibu maswali ya wananchi waliotaka maoni yake kuhusu hali ya maisha kwa sasa kupitia KIKAANGONI kinachorushwa na EATV, Dkt. Mashinji amewataka watanzania kuhakikisha wanatumia fedha vizuri kwa sababu hali ya uchumi siyo nzuri kwa wananchi wa kawaida.

“Watanzania wenzangu tutumie fedha vizuri, hali ni ngumu na ni ngumu kwa sababu ajira nazo hazipo hadi makampuni binafsi yanakusudia kupunguza watu, hivyo tujipange vizuri chini ya uongozi wa awamu hii ya tano, na hali itazidi kuwa ngumu zaidi” Amesema Dkt. Mashinji.

Amesema jambo pekee linaloweza kurudisha nchi katika hali ya kawaida na wananchi wakawa na maisha mazuri, ni kwa Rais Magufuli, kurudi nyuma na kufanya mashauriano na wadau mbalimbali vikiwemo vyama vya upinzani juu ya nini cha kufanya huku akimtaka pia kukubali ushauri badala ya kwenda na mwelekeo anaokwenda nao sasa.

Aidha Mashinji ameongeza kuwa kutokana na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira nchini CHADEMA imejipanga kupitia Baraza la Vijana kuanza mkakati maalumu wa kuwafundisha vijana ujasiriamali ili waondokane na dhana ya kuajiriwa wajiajiri wenyewe.

FB_IMG_1477717290173.jpg
 
Safi Sana. Naiona chadema ikirudi kwenye siasa za ukweli.. Muache kuandamana Bila sababu.. Maisha magumu Kwa WOTE.. Wanaofurahia maisha ni kina lowasa na kina magufuli SISI wengine tufanye kazi tujikomboe NDUGU ZANGU
 
Eti ili hali iwe nzuri Magufuli ashauriane na wapinzani,wamezoea kudeka hawa halafu wanaitwa ikulu kunywa juice
Wana nini kipya cha kushauri wasanii hawa
 
Anaongea vizuri humohumo
Anachanganya na pumba !!!
Kiasi amejaribu kutoka nje ya ujinga
Japo kaujinga kapo
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Vincent Mashinji amewataka wananchi kutumia fedha kwa umakini kwa kubana bajeti ya matumizi yao ili kuhakikisha wanaweza kumudu hali ya maisha kwa sasa.
Dkt. Vincent Mashinji
Akijibu maswali ya wananchi waliotaka maoni yake kuhusu hali ya maisha kwa sasa kupitia KIKAANGONI kinachorushwa na EATV, Dkt. Mashinji amewataka watanzania kuhakikisha wanatumia fedha vizuri kwa sababu hali ya uchumi siyo nzuri kwa wananchi wa kawaida.
“Watanzania wenzangu tutumie fedha vizuri, hali ni ngumu na ni ngumu kwa sababu ajira nazo hazipo hadi makampuni binafsi yanakusudia kupunguza watu, hivyo tujipange vizuri chini ya uongozi wa awamu hii ya tano, na hali itazidi kuwa ngumu zaidi” Amesema Dkt. Mashinji.
Amesema jambo pekee linaloweza kurudisha nchi katika hali ya kawaida na wananchi wakawa na maisha mazuri, ni kwa Rais Magufuli, kurudi nyuma na kufanya mashauriano na wadau mbalimbali vikiwemo vyama vya upinzani juu ya nini cha kufanya huku akimtaka pia kukubali ushauri badala ya kwenda na mwelekeo anaokwenda nao sasa.
Aidha Mashinji ameongeza kuwa kutokana na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira nchini CHADEMA imejipanga kupitia Baraza la Vijana kuanza mkakati maalumu wa kuwafundisha vijana ujasiriamali ili waondokane na dhana ya kuajiriwa wajiajiri wenyewe.
View attachment 425953

Tuache Siasa zetu za ' maji tope ' ama hakika huyu Katibu Mkuuu wa CHADEMA amesema maneno ya Hekima na Busara mno hadi Mimi mwana CCM yamenigusa na nimeyapenda. Hata Mimi namuahidi kufuata huo ushauri wake. Ni Kiongozi na Mtu makini sana na nadhani si tu CHADEMA bali hata tusio wana CHADEMA huyu ' Jamaa ' tumtumie kwani ana kitu fulani cha kuweza ' kutusaidia ' Watanzania kwa ujumla wetu. Tanzania si ya CCM na CHADEMA pekee bali ni ya Watanzania wote. Napenda mno Wanasiasa kama hawa wanaojua ' kufikiri ' na ' kutafakari ' kwa maslahi ya Mama Tanzania. CHADEMA mmepata ' Jembe ' litumieni vizuri tafadhalini.
 
Miaka yote hapa Africa tumekua tunapaswa kuishi kwa kubana matumizi ili tukue kiuchumi japo na sisi tuwakimbilie watu weupe wa huko ulaya,haijawah tokea maisha yakawa mepesi,leo ndo watukumbushe kubana matumizi jambo ambalo tunalijua
 
Huyu Mashinji aliyewahi kusababisha vifo na vilema vya kudumu kwa wagonjwa ana akili ya kushauri serikali?..huu utakuwa upotoshaji.
 
Mbona tumeanza siku nyingi kubana matumizi, sema tuanzishe shughuli za ziada ili kujiongezea kipato
 
Miaka yote hapa Africa tumekua tunapaswa kuishi kwa kubana matumizi ili tukue kiuchumi japo na sisi tuwakimbilie watu weupe wa huko ulaya,haijawah tokea maisha yakawa mepesi,leo ndo watukumbushe kubana matumizi jambo ambalo tunalijua
Kukumbushwa muhimu boss
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Vincent Mashinji amewataka wananchi kutumia fedha kwa umakini kwa kubana bajeti ya matumizi yao ili kuhakikisha wanaweza kumudu hali ya maisha kwa sasa.
Kwa mara ya kwanza nakuunga mkono kwa kuongea hoja yenye uhalisia. Achana na UKUTA WA BISKUTI

Dkt. Vincent Mashinji Akijibu maswali ya wananchi waliotaka maoni yake kuhusu hali ya maisha kwa sasa kupitia KIKAANGONI kinachorushwa na EATV, Dkt. Mashinji amewataka watanzania kuhakikisha wanatumia fedha vizuri kwa sababu hali ya uchumi siyo nzuri kwa wananchi wa kawaida.

“Watanzania wenzangu tutumie fedha vizuri, hali ni ngumu na ni ngumu kwa sababu ajira nazo hazipo hadi makampuni binafsi yanakusudia kupunguza watu, hivyo tujipange vizuri chini ya uongozi wa awamu hii ya tano, na hali itazidi kuwa ngumu zaidi” Amesema Dkt. Mashinji.

Amesema jambo pekee linaloweza kurudisha nchi katika hali ya kawaida na wananchi wakawa na maisha mazuri, ni kwa Rais Magufuli, kurudi nyuma na kufanya mashauriano na wadau mbalimbali vikiwemo vyama vya upinzani juu ya nini cha kufanya huku akimtaka pia kukubali ushauri badala ya kwenda na mwelekeo anaokwenda nao sasa.

Aidha Mashinji ameongeza kuwa kutokana na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira nchini CHADEMA imejipanga kupitia Baraza la Vijana kuanza mkakati maalumu wa kuwafundisha vijana ujasiriamali ili waondokane na dhana ya kuajiriwa wajiajiri wenyewe.
View attachment 425953
Kwa mara ya kwanza nakuunga mkono baada ya kuzungumza hoja yenye uhalisia. Achana na UKUTA WA BISKUTI afu unabahati wewe HUKUZUNGUSHA MIKONO KUASHIRIA MABADILIKO MWAKA 2015 na kwa hilo natoa pongezi zangu nyingine kwako.
 
Tuache Siasa zetu za ' maji tope ' ama hakika huyu Katibu Mkuuu wa CHADEMA amesema maneno ya Hekima na Busara mno hadi Mimi mwana CCM yamenigusa na nimeyapenda. Hata Mimi namuahidi kufuata huo ushauri wake. Ni Kiongozi na Mtu makini sana na nadhani si tu CHADEMA bali hata tusio wana CHADEMA huyu ' Jamaa ' tumtumie kwani ana kitu fulani cha kuweza ' kutusaidia ' Watanzania kwa ujumla wetu. Tanzania si ya CCM na CHADEMA pekee bali ni ya Watanzania wote. Napenda mno Wanasiasa kama hawa wanaojua ' kufikiri ' na ' kutafakari ' kwa maslahi ya Mama Tanzania. CHADEMA mmepata ' Jembe ' litumieni vizuri tafadhalini.
Wenzako wanamtaka katibu mkuu fuska kama Dr Mihogo kuhamasisha vurugu watu wauwawe na kutangaza nchi haitotawalika.
 
Back
Top Bottom