Kama ID yangu invyojieleza, Igwachanya ndo home. Nilikuwa huko a month ago. Hakika kuna-class dogo tu linalotakiwa kuwa written off pale kijijini ili mambo yaende, akiwemo Diwani. Nilijitahidi sana kuelimisha na kuhamasisha watu hasa kundi la vijana. Kiukweli, tatizo kubwa ni uelewa wa watu kwani ukiongea nao wanaonekana kuvutiwa na M4C.
Chamsingi, uongozi wa wilaya wa M4C lazima uweke mikakati endelevu katika kuhakikisha tawi la CHADEMA linakuwepo likiongozwa na watu makini. Aidha, Igwachanya ni kijiji chenye ushawishi mkubwa ktk wilaya mpya ya Wanging'ombe. Hivyo, kuwekeza nguvu Igwachanya kutarahisisha kuzoa vijiji vyote kama kusukuma mlevi vile! Hata hivyo, viongozi wa M4C wapo ingawa wanajitolea tuu. Nao ni Dickson Kiswaga-Katibu na mama Luvanda-Mwenyekiti.
Sasa ushauri wangu kwa M4C, wajitahidi ku-organize mkutano mkubwa wa ukombozi ukiongozwa na watu makini kama akina Rev. Msigwa, Sugu, V. Nyerere, Zitto, Mnyika, nk. mbona hadi mabalozi manyumba kumi watajivua magamba! Pia, kuwe na inspiration endelevu, tusiwatelekeze wale watakao kuwa wamejivua magamba!
Baada ya magamba kugundua potentiality ya kijiji hiki, kwenye uchaguzi wa 2010 Bibi Kiroboto, Riz 1, na uongozi wa CCM Mkoa na wilaya walifanya kufuru ya kumwaga hela kwa wenyeviti wa vijiji na mitaa na kutishiwa kuwa endapo jimbo lingeenda upinzani basi nao wangeadhibiwa kwa kupoteza vibarua vyao. Kwa kuhitimisha, Igwachanya ndo moyo wa M4C kama tunataka siasa za jimbo hili ziwe za manufaa kwa taifa.