tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 26,984
- 27,154
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama kinachojipambanua kama chama cha ukombozi wa wantanzania kutoka ukoloni mkongwe wa CCM. Lengo na dhamira ya CHADEMA ni kuona kwamba kila mtanzania aliyefungwa nira ya ukandamizaji na utumwa wa CCM anapata kukombolewa, kuwa huru na kuishi maisha bora. Nchi hii imekuwa chini ya utawala wa CCM tangu mwaka 1960 lakini badala ya kupiga hatua za maendeleo, imekuwa ikirudi nyuma kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Imani ya wananchi kwa CCM imeshuka kwa 99%, hasa kutokana na vitendo vya kifisadi vinavyofanywa na makada wake. Lakini baya zaidi ni kwamba hata Rais wa nchi naye amejiingiza waziwazi katika harakati za kuwatetea mafisadi bila aibu. Mfano halisi wa hili ni pale mheshimwa Rais alipotumia madaraka yake vibaya kwa kuwasamehe wezi walioiba fedha za umma kupitia EPA kwa kuwaamuru wamrejeshee fedha za umma kisha akawaachia huru warudi mtaani na kuendelea kuiba. Na zile fedha za umma, zipatazo billion 33, hazikupata kurejeshwa mikononi mwa umma hadi leo.
CHADEMA ndicho chama makini na shupavu kitakachowakomboa watanzania kutoka unyanyasaji, ukandamizaji na unyonyaji wa CCM. Imani ya wananchi kwa chama hiki cha ukombozi ni zaidi ya 99%. Sote ni mashahidi jinsi CHADEMA ianvyozidi kujizolea umaarufu na kutanua misuli yake hadi mashinani. Ushahidi wa haya ni mwelekeo wake tangu uchaguzi wa mwaka 1995. Tangu wakati huo, CHADEMA kimeweza kuongeza idadi ya wabunge na madiwani na kuzidi kujitanua hadi vijijini. Pamoja na jitihada za makusudi zinazofanywa na CCM dhidi ya viongozi na wanachama wa CHADEMA, wananchi wameendelea kuwa na imani na chama, chini ya uongozi shupavu wa Mwenyekiti, Freeman Aikael Mbowe (Kamanda wa Anga), na Katibu Mkuu, Dr Wilbroad Peter Slaa (Kamanda wa Ardhini).
CCM huwatumia mamluki kuichafua CHADEMA kwa gharama zozote zile ili kupunguza kasi ya chama hiki kuelekea ikulu mwaka 2015. Lakini, kwa ushupavu wa intellijensia ya chama, chini ya Kamanda Wilfred Muganyizi Lwakatare, njama hizo ovu zimekuwa zikigunduliwa mapema na kudhibitiwa. Baada ya CCM kuona juhudi zao za kuichafua CHADEMA zimegonga mwamba, wameamua kumtumia kada wao machachari, Jaji Mutungi, kutunga uongo dhidi ya CHADEMA na kuueneza kwa umma kwa lengo la kuwakanganya watanzania kwa makusudi. Lakini kwa kuwa Mungu hamtupi mja wake, bado CHADEMA imeendelea kuchanua na kustawi kila kukicha.
CHADEMA imekuwa mstari wa mbele kutetea wananchi dhidi ya uporaji wa rasilimali za taifa unaofanywa na CCM na serikali yake. Dhamira ya CHADEMA ni kuona kwamba rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi wa tabaka zote badala ya kushuhudia rasilimali hizo zikitafunwa na mafisadi wachache wanaolindwa kwa nguvu zote na serikali ya CCM. CHADEMA itakapoingia madarakani mwaka 2015 itahakikisha kwamba mali zote za umma zilizoporwa na CCM na makuwadi wake zinarejeshwa mikononi mwa umma ili kuwanufaisha wananchi wote. Baadhi ya rasilimali hizo ni majengo, mashamba na viwanja vya mpira ambavyo CCM imejimilikisha kwa mabavu. Kila mtu anafahamu kwamba rasilimali hizi zilikuwa ni mali ya wananchi wote lakini baada ya mfumo wa vyama vingi CCM walitumia mabavu kujimilikisha mali hizo kwa nguvu badala ya kurudisha miliki yake kwa umma.
Aidha, mikataba yote ya kilaghai iliyosainiwa kati ya CCM na mabeberu mamboleo (wanaopambwa kwa jina la "wawekezaji"), itavunjiliwa mbali na kusainiwa upya kwa maslahi mapana ya watanzania walio wengi, tofauti na sasa ambapo mikataba hiyo huwanufaisha makada wa CCM na mafisadi wachache ambao hawatosheki na mali kedekede za wananchi walizokwishapora hadi sasa.
Umakini wa CHADEMA katika kusimamia rasilimali za taifa na kuwatetea wanyonge, ndio utakaotuvusha kutoka kwenye kiza nene la utumwa wa CCM na kutupeleka kwenye mafanikio na maisha bora kwa kila mtanzania. Mpaka sasa CHADEMA ndicho chama pekee nchini Tanzania ambacho kimebeba matumaini ya wananchi waliomasikinishwa na CCM tangu nchi hii ipate uhuru. Ni jambo la kusikitisha kwamba CCM wamekosa haya na badala yake wamekuwa wakiwalaghai wananchi kwa kila njia huku wakiikandamiza CHADEMA kwa nguvu zao zote, wakati CHADEMA ndio kimbilio la wanyonge na wale wote waliokatishwa tamaa na utawala kandamizi wa CCM.
Jambo la muhimu ambalo watanzania wote mnapaswa kulitilia mkazo ni kuendelea kukiunga mkono CHADEMA kwa kuhakikisha kwamba mnawapigia kura wagombea wake katika ngazi zote za uongozi kuanzia, wenyeviti wa serikali za mitaa, madiwani, wabunge na Rais katika chaguzi zijazo. Wakopeshe kura CHADEMA, watakulipa maendeleo endelevu. Watanzania wote tuseme "ukandamizaji wa CCM sasa basi". Tanzania yenye neema, chini ya utawala makini wa CHADEMA inawezekana, ikiwa tu mtawezesha serikali ya CHADEMA kuunda serikali mwaka 2015. Sasa ya ukombozi ni sasa. Linalowezekana leo lisingoje kesho. Ewe mtanzania unayelemewa na mizigo ya CCM, njoo kwa CHADEMA na itakupumzisha na mizigo mizito unayobebeshwa tangu nchi hii ipate uhuru mpaka sasa. CHADEMA yatosha!