PostGE2025 CHADEMA yatangaza kutoitambua Serikali ya Tanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Inside10

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
33,615
Reaction score
40,161
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kutoitambua serikali ya Tanzania iliyozaliwa na uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, ikidai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na ukiukwaji wa haki, sheria na misingi ya demokrasia.

Katika taarifa yao kwa umma iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, Desemba 11, 2025, CHADEMA imetaka kuvunjwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) iliyosimamia uchaguzi huo ikisema tume hiyo “haina uhuru, haina uaminifu na haiwezi kusimamia uchaguzi wa haki.”

Katika maelezo yao, chama kimeorodhesha matukio kadhaa ya kile walichokiita ukandamizaji ikiwamo kuzuiwa kwa shughuli za kisiasa, kufungiwa akaunti za chama, kukamatwa kwa viongozi, kuzimwa kwa mitandao, kutekwa na kupotezwa kwa raia, pamoja na kupigwa risasi kwa wananchi wakati wa uchaguzi, huku ikitaka miili ya watu waliouawa kukabidhiwa kwa familia zao ili “izikwe kwa heshima za Kitanzania.”

Kutokana na matukio hayo CHADEMA imetaka kuundwa kwa Serikali ya Mpito itakayowekwa chini ya uangalizi wa taasisi za kimataifa, kurejesha utulivu na kufungua anga la kisiasa.

Chama hicho kimetoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuwawekea vikwazo wote waliotajwa kuhusika katika uhalifu wa kibinadamu, huku kikipendekeza fedha za misaada zisipelekwe serikalini bali kwa asasi huru.

Chanzo Jambo TV
 
Ahhahh!
 
Ile ya CCM iliyowekwa kwenye uchaguzi wa October 30 2020 waliitambua na kuiona kuwa ilisimikwa kwa haki?
Wangetangaza wakati wa Magufuli angekifuta hicho chama ndani ya masaa 5 tu.
Kosa la CHADEMA ni kutaka kutuliza machungu ya awamu ya 5 ndani ya awamu ya 6 .
 
Chadema wako sawa, tatizo ni CCM na wafuasi wao maana
Serikali ya muuaji Samia inaweza kupinga wazo la serikali ya mpito kwa hoja kuwa ina mamlaka halali ya kikatiba.
- Bila shinikizo la kutosha kutoka kwa wananchi, vyombo vya habari hivi tayari Viko Mfuko mwa msigwa,hivyo having usaidizi, msaada pekee ni kutoka jumuiya ya kimataifa, uwezekano wa serikali ya samia muuaji kukubali serikali ya mpito ni mdogo.

Kwani Serikali iliyopo iliyopora madaraka inaweza kupinga wazo la serikali ya mpito kwa hoja kuwa ina mamlaka halali ya kikatiba.
- Bila shinikizo la kutosha kutoka kwa wananchi, vyombo vya habari, na jumuiya ya kimataifa, uwezekano wa serikali ya sasa kukubali serikali ya mpito ni mdogo.

Nafasi ya Jumuiya ya Kimataifa
  • Taasisi kama Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU), na SADC zinaweza kusaidia kama wawezeshaji wa mazungumzo ya kitaifa.
  • Hata hivyo, hatua hii inahitaji ushahidi wa kutosha wa mgogoro mkubwa wa kisiasa au ukiukwaji wa haki za binadamu ambapo kwa sasa ushahidi upo tena mkubwa shida ni jeuri ya serikali ya muuaji Samia.

Mwisho chadema waje na mchakato wa kupata sapoti ya nguvu ya umma,hapa lazima Samia ateme bungo
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kutoitambua serikali ya Tanzania iliyozaliwa na uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, ikidai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na ukiukwaji wa haki, sheria na misingi ya demokrasia.

Katika taarifa yao kwa umma iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, Desemba 11, 2025, CHADEMA imetaka kuvunjwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) iliyosimamia uchaguzi huo ikisema tume hiyo “haina uhuru, haina uaminifu na haiwezi kusimamia uchaguzi wa haki.”

Katika maelezo yao, chama kimeorodhesha matukio kadhaa ya kile walichokiita ukandamizaji ikiwamo kuzuiwa kwa shughuli za kisiasa, kufungiwa akaunti za chama, kukamatwa kwa viongozi, kuzimwa kwa mitandao, kutekwa na kupotezwa kwa raia, pamoja na kupigwa risasi kwa wananchi wakati wa uchaguzi, huku ikitaka miili ya watu waliouawa kukabidhiwa kwa familia zao ili “izikwe kwa heshima za Kitanzania.”

Kutokana na matukio hayo CHADEMA imetaka kuundwa kwa Serikali ya Mpito itakayowekwa chini ya uangalizi wa taasisi za kimataifa, kurejesha utulivu na kufungua anga la kisiasa.

Chama hicho kimetoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuwawekea vikwazo wote waliotajwa kuhusika katika uhalifu wa kibinadamu, huku kikipendekeza fedha za misaada zisipelekwe serikalini bali kwa asasi huru.

Chanzo Jambo TV
Serikali ya WAHUNi waliopora uchaguzi.
 
Back
Top Bottom