CHADEMA yataka Polisi kuharakisha uchunguzi tukio la kutekwa mgombea udiwani Muleba

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Kutokana na mwenendo uliooneshwa na polisi Wilaya ya Muleba ktk tukio hilo na kauli iliyotolewa na polisi ngazi ya mkoa,tunatoa wito Polisi Makao Makuu kuingilia kati ili uchunguzi wa haraka wa suala hilo ufanyike na haki kutendeka na hatua za kisheria kuchukuliwa" Tumain Makene

"Mbali ya Jeshi la Polisi Makao Makuu, pia tunatoa wito kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBU) kutumia mamlaka yake ya kikatiba na kisheria kuhakikisha tukio hilo linafanyiwa uchunguzi wa haraka na kuwabaini wahusika na kuchukua hatua." Tumaini Makene

"Ni muhimu sana vyombo vya dola vikaonesha mwenendo ambao utawashawishi wananchi waamini kuwa kweli vinachukizwa na vitendo vya upoteaji, utekwaji na kushambuliwa kwa risasi kama matukio hatarishi sana ya usalama wa raia na mali zao." Tumaini Makene

"Mojawapo ya dalili za mwenendo sahihi ni kuchukua hatua za haraka za uchunguzi wa matukio ya namna hiyo na kutoa taarifa.Kinyume na hayo,vyombo vya dola vitakuwa vinahalalisha vyenyewe kuendelea kuwekwa katikati ya shutuma na tuhuma kila matukio hayo yanapojitokeza" Tumaini Makene

"Tunaitaka NEC kutoka hadharani kukemea tukio hilo la utekwaji wa mgombea wetu. Vitendo kama hivyo vinatia doa mfumo wa uchaguzi na demokrasia nchini" Mkuu wa Mawasiliano na Habari CHADEMA

"Ukimya wa NEC unaashiria kuwa wanakubaliana na tabia hii katika uchaguzi, ambayo tuliilalamikia hata wakati wa uchaguzi wa marudio wa kata 43 ambao ulipelekea baadhi ya vyama vya upinzani kususia uchaguzi wa marudio Januari 13" @Tumaini Makene
 
Back
Top Bottom