MUSSA ALLAN
JF-Expert Member
- Oct 13, 2013
- 18,925
- 13,280
Maandamano sio hisani ya polisi ni haki ya kikatiba
akaungane na mwanasheria mkuu wa chama chako??Wewe unapaswa kupelekwa mirembe kwa lazima
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO(CHADEMA)
H/SE NO 8.NHC STREET
NGARENARO
www.Chadema.or.tz
TAARIFA KWA UMMA
Tunachukua fursa hii kuujulisha umma wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kuwa maandamano yetu ya amani yaliyokuwa yafanyike Feb 5 yameahirishwa hadi hapo tutakapotangaza tena,
Hata hivyo tunawashukuru sana umma wa Arusha kwa utayari wao wa kupinga Ukandamizaji,dhuluma,na ukiukwaji wa haki za msingi za binadamu.Tunauhakikishia umma kuwa CHADEMA tutaendelea kuwa msitari mbele katika mapambano haya hadi kieleweke.Tunauhakikishia umma wa sombetini na Arusha na Tanzania kwa ujumla kuwa vikosi vyetu vya B 52,Qx Mapambano,Mandela scorpion,Guerila 40,El Che889,Lenin 34PH,na Mama Haki,vimekamilisha maandalizi kabambe kwa ajili ya Sombetini ili kulinda ushindi wetu ambao ni wa 95%+.Kamwe hatutavumilia hujuma yoyote kutoka kwa yeyote.
CHADEMA tupo imara sana,tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu
Nanyaro EJ
Mwenyekiti CHADEMA Wilaya ya Arusha mjini
Mkuu hili liko wazi na ccm wanajua sasa hivi wanaandaa mbinu chafu za kuvuruga kama walivofanikiwa kwa kata zile zingine uchaguzi ukaarishwa lakini bado wakapigwa chinituandamane, tusiandamane ile kata inakwenda chadema..
Polisi wamefanikiwa kudhibiti huu uhuni uliopangwa kufanywa na LEMA. huu ni ushindi dhidi ya uonevu unyanyasaji, ukabaji, uporaji na kila aina ya dhuluma wanaofanyiwa raia wema na hawa waandamanaji.
Kupora kumezuiwa, hamjasitisha, mmekatazwa.
Mkuu Msuki naomba kutofautiana na wewe katika hili. Kwanza,ki-nadharia napinga hatua ya Jeshi la Polisi kuzuia maandamano ya amani iwe kwa CCM, Chadema, CUF or whatever party or socio-political group. Si kweli kuwa eti Chadema wakiandamana ni chanzo cha fujo na uporaji kwani matukio haya hutokea popote utakapotokea mkusanyiko wa watu. Vibaka kumbuka ni opportunists, mwizi hana itikadi isipokuwa wizi. Pili napinga hii dhana kuwa uchumi wa Arusha unashushwa na maandamano ya Chadema. Hili haliingii akilini; iweje maandamano ya siku moja yakashusha uchumi wa jiji zima? Mimi namuunga mkono Mheshimiwa Lowassa lakini kwenye hili nasema mnawaonea Chadema bure.
hayo maandamano haramu ya lema na wahuni wenzake yamepigwa marufuku na jeshi la polisi, ucha upotoshaji
Mnatishia kujamba wakati mna tumbo la kuhara mtaaibika kwasasa hamna mazezeta tena chuga
Kwa watu tuliopo Arusha tunajionea umbulula wa hili jeshi la polisi, maana leo kila kona ya jiji wamepaki Defender zisizo pungua mbili na magari ya maji ya kuwasha mawili na hapo ni katikati ya jiji. Kwenye kata yenyewe ya Sombetini ndo usiseme mitaa yote utafikiri ni makambi ya Feed-force jinsi askari walivyojazana na bunduki zao.
Swali:
Je Chadema Arusha ikiamua kutangaza maandamano kila week polisi si itafilisika?
Baada ya kutangaza maandamano na wafuasi wake maana tunajua hawana wanachama, serikali yayapiga stop maandamano hayo yenye lengo lilofunikwa la kupora mali za raia.
Tumekuwa tukishuhudia kila yanapotokea maandamano; wapo watu wanaopata hasara kubwa kwa kuporwa na waandamanaji, kupoteza mali n.k. Kikubwa kinachotokea ni uporaji hasa maeneo yafuatayo; bar, hotelini, maduka, vibandani, wapo pia wanaoporwa mikoba, pochi, walet, simu na vitu vingine vya thamani na waandamanaji ndio maana wanajitokeza kwa wingi maana ni siku yao ya kutengeneza
kama chadema wameshaona dalili za kushindwa huo uchaguzi ni vema wakajipanga upya maana bado kuna chaguz kibao zinakuja. Yanini kutumia vurugu kama timu ambayo imeshafungwa inavuruga mchezo?
Na kama chadema wanaamini askari wengi wanawaunga mkono kwanini wasiheshimu kazi yao ya uaskari?
Kwa watu tuliopo Arusha tunajionea umbulula wa hili jeshi la polisi, maana leo kila kona ya jiji wamepaki Defender zisizo pungua mbili na magari ya maji ya kuwasha mawili na hapo ni katikati ya jiji. Kwenye kata yenyewe ya Sombetini ndo usiseme mitaa yote utafikiri ni makambi ya Feed-force jinsi askari walivyojazana na bunduki zao.
Swali:
Je Chadema Arusha ikiamua kutangaza maandamano kila week polisi si itafilisika?