Hata hivyo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Robert Boaz alisema kuwa kijana huyo alikuwa mhalifu sugu ambaye Polisi ilikuwa inamtafuta.
"Huyu kijana tulikuwa tunamtafuta siku nyingi kutokana na kuwa na matukio mengi ya kihalifu lakini leo (jana) alikutana na wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wanashangilia ushindi," alisema Kamanda Boaz.
Alisema kuwa kijana huyo baada ya kujichanganya katika kikundi hicho cha wafuasi wa Chadema aliposimamishwa na wafuasi hao alijihami kwa kutoa panga ambalo lilikuwa kiunoni mwake na kuwatishia kuwakata ndipo walipomvaa na kumpiga.