kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
KIJANA aliyejulikana kwa jina la Matekele Mbayi mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 20, mkazi wa Manispaa ya Musoma, Mkoani Mara amefariki dunia baada ya kupigwa na wafuasi wa Chadema wakati wakishangilia ushindi wa chama chao.
Tukio hilo lilitokea jana katika eneo la Barabara ya Nyerere ndani ya Manispaa hiyo.
Hata hivyo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Robert Boaz alisema kuwa kijana huyo alikuwa mhalifu sugu ambaye Polisi ilikuwa inamtafuta.
Huyu kijana tulikuwa tunamtafuta siku nyingi kutokana na kuwa na matukio mengi ya kihalifu lakini leo (jana) alikutana na wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wanashangilia ushindi, alisema Kamanda Boaz.
Alisema kuwa kijana huyo baada ya kujichanganya katika kikundi hicho cha wafuasi wa Chadema aliposimamishwa na wafuasi hao alijihami kwa kutoa panga ambalo lilikuwa kiunoni mwake na kuwatishia kuwakata ndipo walipomvaa na kumpiga.
Kamanda Boaz alisema kuwa kijana huyo baada ya kupigwa na wafuasi hao wa Chadema alikimbizwa hadi katika hospitali ya Mkoa huo lakini kabla ya kupatiwa matibabu alifariki dunia.
Alisema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili sheria ichukue hatua.