Elections 2010 Chadema yashangilia ushindi kwa kuua

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
KIJANA aliyejulikana kwa jina la Matekele Mbayi mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 20, mkazi wa Manispaa ya Musoma, Mkoani Mara amefariki dunia baada ya kupigwa na wafuasi wa Chadema wakati wakishangilia ushindi wa chama chao.

Tukio hilo lilitokea jana katika eneo la Barabara ya Nyerere ndani ya Manispaa hiyo.

Hata hivyo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Robert Boaz alisema kuwa kijana huyo alikuwa mhalifu sugu ambaye Polisi ilikuwa inamtafuta.

“Huyu kijana tulikuwa tunamtafuta siku nyingi kutokana na kuwa na matukio mengi ya kihalifu lakini leo (jana) alikutana na wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wanashangilia ushindi,” alisema Kamanda Boaz.

Alisema kuwa kijana huyo baada ya kujichanganya katika kikundi hicho cha wafuasi wa Chadema aliposimamishwa na wafuasi hao alijihami kwa kutoa panga ambalo lilikuwa kiunoni mwake na kuwatishia kuwakata ndipo walipomvaa na kumpiga.

Kamanda Boaz alisema kuwa kijana huyo baada ya kupigwa na wafuasi hao wa Chadema alikimbizwa hadi katika hospitali ya Mkoa huo lakini kabla ya kupatiwa matibabu alifariki dunia.

Alisema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili sheria ichukue hatua.
 
KIJANA aliyejulikana kwa jina la Matekele Mbayi mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 20, mkazi wa Manispaa ya Musoma, Mkoani Mara amefariki dunia baada ya kupigwa na wafuasi wa Chadema wakati wakishangilia ushindi wa chama chao.

Hata hivyo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Robert Boaz alisema kuwa kijana huyo alikuwa mhalifu sugu ambaye Polisi ilikuwa inamtafuta.

"Huyu kijana tulikuwa tunamtafuta siku nyingi kutokana na kuwa na matukio mengi ya kihalifu lakini leo (jana) alikutana na wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wanashangilia ushindi," alisema Kamanda Boaz.

Alisema kuwa kijana huyo baada ya kujichanganya katika kikundi hicho cha wafuasi wa Chadema aliposimamishwa na wafuasi hao alijihami kwa kutoa panga ambalo lilikuwa kiunoni mwake na kuwatishia kuwakata ndipo walipomvaa na kumpiga.

kilimasera!

Kichwa cha "thread" na "contents" haviwiani::: Nahisi una hali ya ushabiki ndani yako ndiyo maana ukaweka ili bandiko::: Badilisha "heading" ili wasomaji waweza kuelewa vizuri halafu jaribu kuonyesha hekima::: hamna haja ya ku-instigate violence bila sababu!:nono:
 
MODS mwambieni huyu jamaa abadilishe title ya post yake kabla hatujaanza kumuadhibu halafu mtufungie.
 
Basi hata wale wafuasi wa CCM waliopata ajali Tabora mtasema walipigwa na CHADEMA.
 
UYO JAMAA ALIEANDIKA IYO POST NI MSENGErema..
mbona anatumia lugha za uchochezi???
 
Wee Kilimasera, peleka uchochezi wako kwenye blogu vibaraka kama Michuziblog au Wazalendoforums.
Hapa Hutufai.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom