CHADEMA yapata pigo kali Nbeya -365 waenda CCM

CHADEMA yapata pigo kali Nbeya -365 waenda CCM

MJIMPYA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
506
Reaction score
273
Jisomee mwenyewe.

Na Thomas Mtinge, Mbeya
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),kimepata pigo baada ya wanachama wake 365 akiwemo Mjumbe wa NEC na Baraza Kuu la Vijana(BAVICHA),Frank Fumpa kukihama chama hicho na kujiungana CCM. Mbali na CHADEMA, wanachama sita kutoka TLP na wanne CUF nao wamevihama vyama vyao na kujiunga na CCM.

Fumpa na wenzake wali chukua uamuzi huo juzi baada ya kukabidhi kadi zao za uanachamakwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Ab dallah Bulembo katika mkutano wa hadhara uliofanyika maeneo ya Nzovwe mkoaniMbeya.

Miongoni mwa wanachama hao, wamo Ambundile Mwamtondo na Alex Mwaisango ambaoni wapigadebe wakubwa na wa kutegemewa na CHADEMA katika soko la Mwanjelwa mkoani hapa eneo anako ishi Mbunge wa Jimbo la Mbeya, Joseph Mbilinyi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi kadi hiyo,Fumpa alisema aliamua kuchukua uamuzi huo aliouita kuwa ni mgumu kwake ili kuondokana na adha ya kutumika na CHADEMA.
" Kuwepo ndani ya CHADEMAsi utukufu na kuingia CCM si dhambi, nimeamua kurudi CCM kwa baba na mama baada ya kuchoshwa na sera mbovu za CHADEMA ," alisema Fumpa.
Alisema, anajuta kupoteza muda wake mwingi akiwa CHADEMA kwa kukosa nafasi ya kuwatumikia wananchi wenzake katika kuleta maendeleo.

"Sisi tulikuwa tukipoteza muda tu. Pamoja na kushikilia jimbo hili la Mbeya Mjini, lakini hakuna chochote tulichowafanyia wananchi wetu zaidi ya kupinga kila jambo linalofanywa na serikali ya CCM hata kama ni zuri," alisema.
Fumpa alisema, anashangaa CHADEMA kukebehi maendeleo yanayofanywa na serikali ya CCM huku chenyewe kikishindwa kuonesha mfano wa kile ilichokifanya.

Alisema, Serikali ya CCM ina kila hali ya kujivunia na kutembea kifua mbele kutokana na mengi iliyoyafanya kwa wananchi wake katika kipindi cha utawala wake.
"Anayesema serikali ya CCM haikufanya kitu huyo ana dhambi. Ndiyo maana hata mimi niliamua kuondoka mapema CHADEMA ili nisiendelee kupata dhambi," alisema Fumpa.
Kwa upande wake Mwaisango alisema, kuondoka kwao kumekipa pigo kubwa CHADEMA na kwamba kuanzia sasa watafanya operesheni 'Safisha CHADEMA' kwa kuhamasisha wanachama wake wajiunge na CCM.

Naye Mwamtondo alisema CCM ina kila sababu ya kujivunia baada ya kupata wanachama hao ambao walikuwa tegemeo la CHADEMA.

"Mwenyekiti sisi hatuna la kusema, tumerudi CCM kwa hiari yetu sasa kazi moja tu ni ushindi kwa CCM," alisema.

Akiwahutubia mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo, Bulembo alisema kujiunga CCM kwa wanachama hao kumeichimbia kaburi CHADEMA.


Source: Majira leo
 
kumbe ccm wananunua kadi?Ninauza kadi yangu ya chadema ila mimi sihami chadema.anayetaka ani pm
 
Ila urudi shule kwanza huu mwandiko toka juu kwenye kiini cha habari umepandanisha herufi umeacha nafas pasipo.YAWEZAKANA HATA AKILI ZAKO ZIKO OVYO OVYO KAMA HERUFI ZILIVYO OVYO OVYO NENDA SHULE.
 
Mkuu hiki ni kisafwa kinyiha au kimatengo andika kiswahili basi ili ueleweke
weee wasafwa tuko makini,huyu hata akili zake ndo zilivo hvo hvo maana mwandiko heruf zmebebana mara nafasi,hawa ni vijana waliosoma kipindi cha mulugo..!
 
Dah..iyo lugha iliyotumika sjui kichina au kimasai,maana jamaa anaonekana alitumia muda mwingi kutunga iyo stori yake.Lakini pamoja na hilo naomaba makamanda wa CDM tukaze buti coz hata katika ulimwengu wa roho kuna kambi mbili yaani ya kambi ya Mungu na Shetani.Kwa maana iyo ata shetani ana wafuasi kama mungu pia,nijuavyo mimi cku zote mpenda haki yupo upande wa Mungu,kinyume na hapo.sasa rejea kwenye siasa za Bongo na ujiulize ni nani anaetetea haki za wanyonge,ukipata jibu ujue uyo au chama yupo kambi ya mungu na kinyume chake..
 
Mkuu hiki ni kisafwa kinyiha au kimatengo andika kiswahili basi ili ueleweke

Nahisi ameandika kimalila mbwiga huyu... anatuaibisha watu wa Mbeya tunaosifika kwa umakini.
 
Hakuna atokae CDM kwenda CCM akapata mafanikio ya kuheshimiwa na jamii isipokuwa ni kujiongezea dharau.pili nina mashaka na taarifa hii imekaa kipropaganda zaidi mkutano huo haukuwa na watu wengi inamaanisha uliudhuriwa na hao wanachama wa CDM waliokuja kwa ajili ya kujiunga CCM? na je katika eneo hilo hakukuwa na wanachama wa CCM?
 
Ametuaibisha sana huyu yani, afu mbeya ipi ccm wapate wanachadema 350 au mbeya ya kisalawe
Nahisi ameandika kimalila mbwiga huyu... anatuaibisha watu wa Mbeya tunaosifika kwa umakini.
 
Mkuu MJIMPYA tafadhali edit bandiko lako lisomeke vizuri
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom