Zomeazomea hizi hazina mahusiano yoyotete na Chama cha Siasa; Kumbuka zomeazomea iliyomkumba Waziri Mkuu PM. PINDA Mwanza. Unafikiri KINANA au mawaziri hao wanao umaarufu kuliko PM?.
Zomea Zomea hizo kwa CCM na serikali yake pasitafutwe mchawi kwani hiyo ni true reflection of what is going on ktk uelewa wa watanzania. Hawatazomewa iwapo tu wataweza kutimiza yale wanayoyasema, kwani imekuwa ni Utamaduni kwa CCM na serikari yake kustrategise kwenye makaratsi na mikutano lakini uhalisia ni HAKUNA lolote. Kama CCM watatenda kadri ya wasemavyo basi Watanzania ni wasitaarabu na kusomewa hakutakuwepo.
La msingi ni kwa CCM na seriakali yake Kufanya utafiti huru waweze kujua ni wapi wamejikwaa badala ya kung'ang'ana na sehemu ilipoanguka kwenye madhaifu. Wanaowazomea hao Mawaziri si wana CHADEMA tu bali hata wana CCM wenyewe kwani nao ni sehemu ya jamii inayokipata cha moto ( maisha magumu, na kutoona future yao na familia zao) . Ukiona watu wazima wanakuzomea kama Bongo zako zinacheza vizuri ( timamu) basi unabidi ujiulize kulikoni tatizo nini?, Jitafakari na kujitadhimini, nasiyo itakuwia vigumu kama kingozi kufikisha ujumbe unaoupeleka kwa jamii .
Zomeazomea hazitakoma hadi CCM na serikali yake itakapo kuwa tayari kutenda sawa sawa na maneno inayoyahubiri kwenye majukwaa na makongamano. Naona kama kuna mawaziri wawili au watatu wanaoweza kusimama kwenye majukwaa ya kisiasa kwa uapande wa serikali ya CCM wakasikizwa na wasizomewe. Ni utamaduni mpya na pia sio usitaarabu kuzomewa kiongozi, lakini basi badala ya wanachi kuangua vilio au kupiga mayowe,wawaonapo viongozi hao wameona Zomea zomea waongo ndio njia sahihi kwa kufikisha ujumbe kwa watu wasiokuwa wasikivu wenye kujali matumbo yao na familia zao.