CHADEMA yapaa vijijin (interior)


Inaonyesha unavyoumia maskin poleeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 

Hongera kaka kazi njema kwani elimu ya uraia inatakiwa kuenezwa kwa wingi hasa vijijini. Ili kuweza kuleta mabadiliko ya kweli ni lazima ifike wakati CCM ipumzike ili hata kama itarudi baadae irudi na mawazo mapya kwani kwa hivi sasa imefilisika kisera na kiutendaji. Hebu jiulize inakuwaje taifa lenye polisi na usalama wa taifa then wakina masogage wanapita airport na unga wa bilion 6.8 na kuenda kukamatiwa sauzi? Hivi kweli kunauwajibikaji hapa si rushwa tu imejaa na imekisiri kwa kiasi kikubwa.

Swali la kujiuliza ni je Taifa letu litakaa liendelee kweli taifa ambalo tunaishi kwa kudra za mwenyezi mungu kwa maana hata kulinda mipaka yetu tumeshindwa. Wageni wanajiingilia tu watakavyo wanaishi kwenye nchi yetu bila vibali wanajifanyia watakavyo na vyombo vya ulizi na usalama vipo vimekaa tu havijui kinachoendelea kazi yao kubwa ni kupambana na wapinzani kwa maslahi ya CCM si kupambana na dawa za kulevya na kulinda usalama wa nchi na wananchi wake kama ilivyopaswa kuwa. Nahisi ipo siku tutakuja tuangamizwe wote ni bora sasa CCM ipumzike ijipange upya kwa kuwa nadhani kwa hali ilivyo sasa hawajui nini uwajibu wao kwa taifa.

Ndovu wanauawa maelfu kwa maelfu, madini yetu yanachotwa na wageni kama mchanga, elimu yetu ni mbovu walishaiua ili wapate kufanya biashara ya shule zao binafsi enzi za mwalimu ukifaulu kwenda shule ya secondari ya umma ulikuwa unaonekana kichwa lakini leo tunaogopa kuwapeleka watoto wetu huko kwa sababu elimu ya umma ilishachimbiwa kaburi na kuzikwa na CCM, Jeshi la polisi na usalama wataifa ambavyo zamani enzi za mwalimu vilisifika na hata watu wakasema tanzania ilikuwa ni nchi inayoongoza kwa upelelezi leo vimekuwa vyombo vya CCM vimeacha kazi ya kulinda raia na mali zao na usalama wa nchi. Leo tanzania imekuwa geti la kupitishia madawa ya kulevya tena hayapiti kwa njia za panya bali yanapita Airport ni aibu kubwa taifa kama tanzania. Sasa taifa letu ni taifa ambalo halina maadili tena hasa kwa viongozi nchi inanuka rushwa kila kona, vitendo vya uonevu na unyanyasaji wa raia pamoja na dhuluma kwa wananchi vimekisiri. Ndio maana tunasema ni heri CCM ikapumzika maanake imelewa madaraka haijitambui tena iko wapi na inaenda wapi.
Hongereni sana mnaoeneza elimu ya demokrasia hatimaye nchi yetu itaokoka kutoka katika makucha ya mkoloni mweusi.

Usahauri kwa vyama vya upizani ni kuwa vijenge kwanza msingi huku chini visikimbilie kwenye nafasi ya uraisi ni ngumu kufika huko kama hujajenga msingi imara huku chini vihakikishe vinaongeza madiwani na kushika uongozi wa hata baadhi ya halmashauri then vionyeshe uwezo wao wa kuongoza na nina imani vitaweza kuwashawishi wananchi walio wengi kuvichagua najua kunaugumu fulani maslani arusha CDM inamadiwani wengi ilipaswa kuongoza manispaa ya arusha lakini CCM haijawa tiari kuwapa mwanya lakini wasikate tamaa naamini kwenye uchakuguzi wa serekali za mitaa mwakani kama watashika maeneo mengi basi itakuwa na impact hata kwenye uchaguzi mkuu 2015 lakini wakichemsha hapo then 2015 tusitarajie miujiza bado CCM itaendelea kushika dola
 



acha kutuvuruga we mwanadamu,uchaggani ndo nn? na cc ambao c wachagga unatufanya wachagga?hata hivyo c kosa lako ni umaskini tu,unafanyia kazi buku 7;pole mwanadamu.
 
poa mkuu,kazi njema.Sisi tupo ktk kijiji fulani kilichopo mkoani kagera kinaitwa nyakatanga,watu hawana hata kandambili lkn wote vidole 2 juu wanaitika poweeeer...tupo na kamanda wenje ktk M4C,chezea cdm wewe.
 
thats wonderful and beautiful words of life....inapendeza kijana, una stahili kuigwa....viva chadema
 

mhe.zitto hajagi huko?
 

Hongera sana, na Mungu akufanikishe. Na huku Mwanza tunasonga tunaendelea kupenya vijijini, Tutafika!
 
tena vijijini ccm ikifa haitaweza kurudi ! Mimi nimefanya yangu kyela , tena kwa mafanikio makubwa ! Japo kuna mtu alikurupa kwenda kugawa bodaboda .
kamanda pa1 sana yani huku mababu, kisyosyo ngyekye yote kazi kwisha na kata ya matema kwa ujumla tunasubili siku ya kuapishwa makanda wa cdm kwani mwakyembe ametuongopea vya kutosha na zao letu kuu la kokoa linazidi kupoteza thamani. Viva cdm
 
kamanda pa1 sana yani huku mababu, kisyosyo ngyekye yote kazi kwisha na kata ya matema kwa ujumla tunasubili siku ya kuapishwa makanda wa cdm kwani mwakyembe ametuongopea vya kutosha na zao letu kuu la kokoa linazidi kupoteza thamani. Viva cdm

Ha! Ha! Ha! Ha! Asante sana mkuu , tushirikiane kuikomboa kyela , umoja ni nguvu .
 
safi sana mkuu , na naomba uungane na Bwn Tatizo Muhenera naye anaishi hapo hapo itumbiko ni mudau mkubwa sana.

Mungu bwana ananjia nyinyi sn , walilifungia Gazeti la Mwanahalisi ili wananchi tusielimishwe , lakini mungu ametupa chombo kinginne mbadala , niwaombe sana hasa wadau wa chombo hiki tukipe support ya kutosha , maombi ni muhimu
kila mtu afanye hivyo kwa imani yake , ni imani yangu kuwa hakika tunaweza.


PONGEZI KUBWA KWENU JAMII FORMU .
 
Umenielimisha na mimi naslekea kuelimisha wengine mamia, tupo na Mola.......
 
Kamanda nami nimeona kokoa inakua si mali tena, wananchi wa kyela hatuwezi vumilia porojo za mtu huyu zaid aondoke. Mpunga bei chini kokoa bei chini makamamda tupige elim ya uraia watu wajitambua waikatae ccm
kamanda pa1 sana yani huku mababu, kisyosyo ngyekye yote kazi kwisha na kata ya matema kwa ujumla tunasubili siku ya kuapishwa makanda wa cdm kwani mwakyembe ametuongopea vya kutosha na zao letu kuu la kokoa linazidi kupoteza thamani. Viva cdm
 
Ccm ndiyo kipenzi cha wengi vijijini mtajipanga sana ccm inajulikana zaidi kama chama cha nyerere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…