PreGE2025 CHADEMA yaomba siku 21 kujibu hoja zilizowasilishwa Mahakamani na wanachadema wanne kusimamisha shughuli zote za kisiasa za chama

PreGE2025 CHADEMA yaomba siku 21 kujibu hoja zilizowasilishwa Mahakamani na wanachadema wanne kusimamisha shughuli zote za kisiasa za chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
UKIONA CHAMA KINAKOSA MAJIBU YA TUHUMA ZINAZOWAKABILI JUWA HICHO CHAMA NI MFU
 
Wanaenda mahakamani lakini wanajificha! Ukitaka ucheke ufe, utaona hiyo kesi itatolewa hukumu harakaharaka, wakati ya covid19 ilichukua muda kibao, na hukumu ikatoka isiyoeleweka.
 
Wanaenda mahakamani lakini wanajificha! Ukitaka ucheke ufe, utaona hiyo kesi itatolewa hukumu harakaharaka, wakati ya covid19 ilichukua muda kibao, na hukumu ikatoka isiyoeleweka.
Chokonozi za aina hii ndizo zinazo endelea kuwafunua macho wasiojuwa kinacho endelea chini kwa chini katika muungano huu.
 
Kuliko wizi wa fedha katika report ya CAG??

WE KWELI NI KENGE!!🤣🤣🤣 unaacha kuwa na concern na mambo ya maana ya huko kwenu!!
Gentleman,
mgao wa pesa za chadema kwenda Zanzibar, kibaka na tapeli mropokaji aliziuia akazipeleka kwenye matumizi ya whisky na nyama choma kwa ajili ya viongozi waandamizi wa kitaifa chadema Taifa.

Jamaa wanataka mgao wao kabla suala la udini halijalipuka nje ya mahakama 🐒
 
Wanaenda mahakamani lakini wanajificha! Ukitaka ucheke ufe, utaona hiyo kesi itatolewa hukumu harakaharaka, wakati ya covid19 ilichukua muda kibao, na hukumu ikatoka isiyoeleweka.
Hizi ni njama na woga wa Samia. Anajua kabisa CHADEMA ya sasa ndicho chama cha kweli cha upinzani. Hapa watu tunazidi kuamini kuwa Mbowe alikuwa ni mtu wa mkakati ndani ya chama. Unajua hawa watu wana akili ndogo sana kwa sababu wanadhani wakizuia au kuyumbisha vyama halali vya upinzani basi watatawala kwa raha na kuiba bila bughdha.
 
Kabisa👍
 
chadema haijawahi kupata hata mwenyekiti wa kitongoji zanziba r lakini jamaa wanadai wanapunjwa.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeomba siku 21 ili kujibu hoja zilizowasilishwa Mahakamani na waleta maombi Saidi Issa Mohammed na wenzake watatu (3) waliofungua kesi kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam wakiiomba Mahakama hiyo kutoa amri ya kusimamisha shughuli zote za kisiasa za chama hicho zinazoendelea hadi hapo shauri lao la msingi litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi

Shauri hilo namba 8323 la mwaka 2025 linalowahusisha pia baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa CHADEMA kutoka Zanzibar iliitwa leo, Alhamisi Aprili 17.2025 chini ya Jaji Hamidu Mwanga, ambapo inaelezwa kuwa pande zote mbili zilihudhuria

Hata hivyo, Jambo TV imefanya jitihada za kuwasiliana na Mawakili wa pande zote mbili ili kujuwa kile kilichojili kwenye 'kikao cha ndani' baina yaa pande hizo mbili na Jaji, lakini Mawakili wa pande zote hawakutoa ushirikiano hitajika kwa wanahabari

Mawakili wa waleta maombi wakiongozwa na Gido Simfukwe na Shabaan Marijan inadaiwa kuwa walitumia 'mlango wa nyuma' kuingia Mahakamani hapo ili kukwepa waandishi, na hata walipotafutwa kwa simu kwa kutumiwa ujumbe mfupi wa maandishi (sms) au kupigiwa simu hawakupokea, na baadaye hawakupatikana hewani kabisa

Hata hivyo kwa upande wa utetezi (CHADEMA) waliwakilishwa na Mawakili wawili (2) mmoja kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu na mmoja kutoka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa chama hicho

Mawakili hao ambao 'waligoma' kutaja majina yao wamesema wamepokea maelekezo kutoka kwa wakuu wao kwamba wawakilishe chama Mahakamani kisha wapeleke mrejesho, baada ya hapo chama kitatoa msimamo wake rasmi, hivyo wao kugoma kuongea na vyombo vya habari, hata hivyo Jambo TV imenukuu sehemu ya maelezo yao wakisema:

"Kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa, CHADEMA wanapokea nyaraka ambayo ni mashtaka au madai ya msingi kuhusiana na shauri husika baada ya hapo CHADEMA wameomba siku 21 kama kwa mujibu wa sheria ilivyo ili kujibu hayo madai au hayo mashtaka, kwahiyo wameambiwa wawasilishe majibu yao kabla au kufikia tarehe 09/05/2025, na kesi itakuja tarehe 12/05/2025 saa 3 asubuhi kwa ajili ya kutajwa na kuangalia some oders kama zimezingatiwa", ameeleza Wakili kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Sheria wa CHADEMA

Ikumbukwe kuwa, waleta maombi ambao ni Saidi Issa Mohammed (aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar) na wenzake Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu (Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini kutoka Zanzibar) wamefungua shauri hilo dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA ambayo ni mdaiwa wa kwanza na mdaiwa wa pili na Katibu Mkuu wa CHADEMA

Waleta maombi wanaiomba Mahakama itamke kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekiuka sheria inayohusiana na vyama vya siasa na Katiba ya chama hicho, kutokana na kile wanachodai kuwa uwepo wa mgawanyo usio sawa wa raslimali za chama na raslimali fedha kati ya Tanzania Bara na Zanzibar

Pia wanadai kuwa kuna ubaguzi wa kidini na kijinsia, pamoja na kutoa maoni na matamko yaliyo na nia ya kuvuruga Muungano kati ya pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Awali kabisa kabla ya kwenda Mahakamani, Jambo TV ilifanya mahojiano kwa njia ya simu na Wakili Gido Simfukwe anayewakilisha upande wa waleta maombi, ambapo akizungumza akiwa Zanzibar amenukuliwa akisema:

"Hili jambo ni kwamba kuna hawa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya hicho chama (CHADEMA) wamekuwa wakitengwa hawa wanaotoka upande wa Zanzibar, kwa sababu bodi ile inaundwa na Wajumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, sasa wao hawajaridhika na mgao wa raslimali za chama kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, kwa mfano mathalani kule Tanzania Bara kuna majengo, na wamenunua jengo jipya hivi karibuni lakini huku Zanzibar hakuna jengo lolote hata ofisi wamepanga, kuna magari ambayo yapo mengi tu wanatumia, kuna mashamba ambayo yapo maeneo mbalimbali ambayo ni mali za chama lakini kwa upande huu (Zanzibar) hakuna kitu chochote ambacho wanacho" -Wakili Simfukwe

"Hata ukiangalia katika mgao wa ile ruzuku, matumizi ya pesa yaani huku inaletwa Tsh. 4,000,00/- (Laki nne), pengine wanaweza wakaleta Tsh. 2,000,00/- (Laki mbili) kwa mwezi, hata mishahara ya wafanyakazi imekuwa ni shida, wengine wanadai mishahara yao hawajalipwa, sasa hii imewafanya hawa (wataja wake) wakasema hapana inatosha, tumepunjwa sana, kuna mapunjo ya mgawanyo wa raslimali za chama kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.

"Kwahiyo hilo ndio limepelekea wakasema sisi twende Mahakamani tufungue kesi tudai mapunjo yote ambayo tumekuwa tukipunjwa na pia Mahakama itoe tamko juu ya mapunjo haya kwamba yanakwenda kinyume na sheria ya vyama vya siasa, yanakwenda kinyume na Katiba yenyewe ya CHADEMA

"Yanakwenda kinyume na miongozo ya Msajili wa Vyama vya Siasa pamoja na mustakabali mzima wa Muungano wetu kwa sababu, kwa sababu chama chochote kinachoanzishwa ni lazima kiwe chama cha kimuungano," -Wakili Simfukwe.

Chanzo: Jambo TV

Pia soma ~ CHADEMA waburuzana mahakamani, kesi kuanza leo
Kwamba 4,000,000/- ni laki nne?
2,000,000/- ni laki mbili?
 
Wenye akili wachache sana na wale waliojaliwa maono na Mungu ndio wataweza kuona dhahama itakayoletwa na hii kesi. Kuna watu wanafikiri hiyo kesi inaenda kukikomesha chama fulani lakini ukweli ni kuwa kuna hisia ya kundi fulani kama nchi inakwenda kuamshwa juu ya Muungano.

Ombi langu kwa wenye mamlaka ya nchi hii fanyeni juu chini hiyo kesi iondolewe mahakamani kwa sababu kuna kitu kitakwenda kuzalishwa hapo na madhara yatakuwa hayaponyeki kwa muda mrefu ujao na hasa iwapo mwenendo wa hiyo kesi itakuwa inaripotiwa neno kwa neno kwa umma wa watanzania.

Kuna vitu vingine vipo wazi jamani lakini watu hawavioni sijui ndio tumekuwa mnara wa Babeli au tumekuwa kama yule mnyama ambaye hasikii mpaka apigwe atoke damu masikioni.

Ombi langu kwa viongozi mliopo madarakani tumieni busara zenu kwani huu muungano pamoja na mapungufu yake bado ni nguzo muhimu sana nchi yetu na unahitaji marekebisho kadhaa ili ukae sawa. Lakini ukiachiwa uende majaribuni mahakamani kwa ninavyo mfahamu Kibatala na timu yake ya mawakili hakika hakuna jiwe litakaloachwa kufunuliwa juu ya huu Muungano. Tukumbuke kuwa watanzania wa sasa wanafuatilia sana mambo na hasa hizi simu janja zimewaraishia sana kupata habari.

Kwa mtizamo wangu nafikiri hizi kesi za namna hii ambazo zinautia majaribuni Muungano na zinaweza hata kuamsha hisia za upande mmojwapo wa Muungano zisipewe nafasi badala yake serikali ijikite kuendelea kupunguza kero za Muungano ili kuwaleta watanzania pamoja.

Ni mtizamo tu.
 
A cha wachokonoe mambo ili waje watwambie ni kwa namna gani mbunge mwenye kura elf tatu anakuwaje sawa na mbunge mwenye kura laki moja na nusu.
 
Hapo kwenye mawakili wanaotetea CHADEMA mmoja kutoka ofisi ya mwaasheria mkuu wa serikali na mwingie kutoka mkurugezi wa sheria wa chadema. Huyo wa ofisi ya mwanasheria wa serikali waaruhusiwa kutetea vyama?
 
Halafu aliyefungua kesi mmojawapo ni Maulida Komu😂😂😂 Mbowe arudishe pesa za ccm maana zitamtokea pabaya.
Huyo mama nilikua namuona wa maana sana sikujua ni mjinga hivi. Ukabila unawatesa sana hawa jamaa hawataki kabisa kuamini chama kimehama kaskazini na kuwa cha kitaifa.
 
Yaani nchi nzima ya Zanzibar inapewa mgao wa ruzuku laki mbili aiseee

CHADEMA mnatisha
 
Huyo mama nilikua namuona wa maana sana sikujua ni mjinga hivi. Ukabila unawatesa sana hawa jamaa hawataki kabisa kuamini chama kimehama kaskazini na kuwa cha kitaifa.
Hawa wajinga ndio walikuwa wanachafua taswira ya chama kuonekana ni cha wachaga. Maslahi yao binafsi yamepotezwa wanaanza kuhujumu chama.
 
Inawezekana Mbowe hata hahusiki ni usumbufu tu
##Kuna 85% possibility ya kuhusika kwake...

##Hawa kumbuka walikuwa wasaidizi (right hand) wake wa karibu chini ya uongozi wake kwa miaka karibu 22....

1. Said Issa Mohamedi ndiye aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wake upande wa Zanzibar

2. Huyu Maulida Komu ni ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa BAWACHA na pia ni mke wa ambaye amewahi kuwa mbunge wa Moshi Vijijini somebody Komu na baadaye kutimukia CCM...

##Ni ngumu kidogo kuamini kuwa huyu mtu (Saidi Issa Mohamedi) ambye alikuwa right hand wa Freeman Mbowe miezi isiyozidi minne iliyopita kabla hawajashindwa kwenye uchaguzi anaweza kuchukua uamuzi wa kukipeleka chama mahakamani bila kushauriana na aliyekuwa Mwenyekiti wake kwanza na walioshindwa pamoja kwenye uchaguzi...
 
Back
Top Bottom