GE2025 CHADEMA yamsimamisha Odero Charles kupisha uchunguzi

GE2025 CHADEMA yamsimamisha Odero Charles kupisha uchunguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Kaskazini kimemsimamisha Katibu wa Kamati ya Sheria na Haki za Binadamu wa chama hicho, Odero Charles Odero kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

1753947187599.png
Odero ambaye alikuwa miongoni mwa wagombea wa nafasi ya uenyekiti ndani ya Chadema, majukumu yake kama mjumbe sekretarieti ya kanda pia yatasimama

Katika uchaguzi wa ndani wa Chadema uliofanyika Januari 21, 2025 alikuwa akichuana na Freeman Mbowe aliyekuwa akitetea nafasi ya uenyekiti na Tundu Lissu ambaye mwisho wa uchaguzi aliibuka mshindi

Odero alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura moja. Lissu alipata kura 513 na Mbowe akipata kura 482. Jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 999 na halali zikiwa 996 huku tatu zikiharibika

Taarifa ya kusimamishwa kwa Odero ndani ya Chadema Kanda ya Kaskazini imetolewa jana Jumatano, Julai 30, 2025 na Katibu Kanda ya Kaskazini, Ndonde Totinan baada ya kupokea tuhuma dhidi ya kada huyo kuwa mwenendo usioridhisha

Asubuhi ya leo Alhamisi, Julai 30, 2025, Mwananchi limemtafuta Odero ambaye amesema barua ya kusimamishwa kwake aliipokea usiku wa jana Jumatano. Hata hivyo, hakueleza kwa kina tuhuma hizo zinazoelezwa iwapo anazifahamu

Chanzo: Mwananchi
 
Chadema itabaki na watu loyal tu inayoyapitia itawajenga zaidi na zaidi.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Kaskazini kimemsimamisha Katibu wa Kamati ya Sheria na Haki za Binadamu wa chama hicho, Odero Charles Odero kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

Odero ambaye alikuwa miongoni mwa wagombea wa nafasi ya uenyekiti ndani ya Chadema, majukumu yake kama mjumbe sekretarieti ya kanda pia yatasimama.

Katika uchaguzi wa ndani wa Chadema uliofanyika Januari 21, 2025 alikuwa akichuana na Freeman Mbowe aliyekuwa akitetea nafasi ya uenyekiti na Tundu Lissu ambaye mwisho wa uchaguzi aliibuka mshindi.

Odero alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura moja. Lissu alipata kura 513 na Mbowe akipata kura 482. Jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 999 na halali zikiwa 996 huku tatu zikiharibika.

Taarifa ya kusimamishwa kwa Odero ndani ya Chadema Kanda ya Kaskazini imetolewa jana Jumatano, Julai 30, 2025 na Katibu Kanda ya Kaskazini, Ndonde Totinan baada ya kupokea tuhuma dhidi ya kada huyo kuwa mwenendo usioridhisha.

Asubuhi ya leo Alhamisi, Julai 30, 2025, Mwananchi limemtafuta Odero ambaye amesema barua ya kusimamishwa kwake aliipokea usiku wa jana Jumatano. Hata hivyo, hakueleza kwa kina tuhuma hizo zinazoelezwa iwapo anazifahamu.

Chanzo: Mwananchi
 
Odero amefanyaje? Mnaleta habari nusu nusu. Watu wameruhusiwa kuondoka ila Hawataki wamebaki CHADEMA ili waendeleze usumbufu.
 
Inaelekea uongozi wa sasa unaendekeza fitna na majungu. Upuuzi huu unaota mizizi kwenye kanda na matawi na ulitumiwa sana dhidi ya G-55. Sio mwenendo mzuri na hauna afya kwa chama.

Amandla...
 
Chadema hawana akili mda huo Yericko Nyerere anatamba
 
Back
Top Bottom