- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Salaam Wakuu,
Nimekutana na hii Taarifa ya The Chanzo inadai Chama Cha Demokrasia na Maendelea kimemsimamisha Uanachama Tundu Lissu.
Kuna ukweli?
Nimekutana na hii Taarifa ya The Chanzo inadai Chama Cha Demokrasia na Maendelea kimemsimamisha Uanachama Tundu Lissu.
Kuna ukweli?
- Tunachokijua
- Tundu Lissu ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA tangu mwaka 2019 alipochaguliwa kutumikia nafasi hiyo, pia alikuwa mbunge wa jimbo la Singida mashariki kuanzia mwaka 2010 mpaka mwaka 2020 ambapo wagombea wengi wa upinzani hawakufanikiwa kushinda nafasi mbalimbali wakati wa uchaguzi huo.
Mnamo tarehe 12 Novemba 2024 Lissu alizungumza na waandishi wa habari akiwa mkoani Singida (unaweza kuutazama hapa). Lissu alizungumza mengi lakini kubwa zaidi alizungumzia kasoro pamoja ukiukwaji wa taratibu za kidemokrasia katika michakato uliosimamiwa na TAMISEMI kuelekea uchaguzi wa Serikali za Miitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024. Zaidi ya hayo, Lissu pia alitumia Mkutano huo kukemea rushwa ndani na nje ya chama chake.
Tangu kufanyika kwa Mkutano huo zimeibuka Taarifa nyingi potofu sambamba na nukuu potoshi zikihusishwa na Mkutano huo soma hapa na hapa.
Wiki moja baadaye ya Mkutano wa Lissu Novemba 19, 2024 Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa CHADEMA) alifanya Mkutano na Waandishi wa Habari ambaye pia alieleza kutoridhishwa na Mwenendo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unavyoendeshwa na TAMISEMI. Baada ya Mkutano huo kulizuka Machapisho mengi yaliyokuwa nukuu za Uzushi wakizihusisha na Mkutano huo, nukuu nyingi zilitengenezwa kuonesha mahusiano mabaya kati ya Lissu na CHADEMA tazama hizi hapa zilizohakikiwa na JamiiCheck na kubainika kutokuwa na ukweli wowote.
Leo Novemba 20, 2024 Kumeibuka 'Post' ya mtandao wa X yenye nembo ya The Chanzo iliyobeba Taarifa inayodai Tundu Lissu Makamu amesimamishwa Uanachama wa Chama hicho (Taarifa hiyo imehifadhiwa hapa)
Uhalisia wa Lissu kusimamishwa CHADEMA upoje?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa Taarifa sio ya kweli, haijatolewa katika kurasa rasmi za CHADEMA na Wala haijawahi kuchapishwa katika kurasa za The Chanzo kama inavyoonekana
Aidha, kupitia kurasa rasmi za CHADEMA jana Novemba 20, 2024 wamechapisha video (hii hapa) ikimuonesha Mwenyekiti wa Chama Freeman Mbowe akielezea ratiba ya Lissu kuzindua kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa CHADEMA Ikungi na Tarime kuanzia Novemba 21, 2024