Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,895
- 20,392

Wadau, amani iwe kwenu.
Kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, zimesambaa taarifa za CHADEMA kumuomba Dr Slaa kurejea chamani na kwenye nafasi yake ya Ukatibu Mkuu. Tafsiri ya ombi hilo la CHADEMA kwa Dr Slaa ni kwamba hawajapata mtu wa kuvaa viatu vya Dr Slaa ambavyo hakuna mwenye uwezo wa kuvivaa. Hapa maneno ya Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Tundu Lissu kuwa viatu vya Dr Slaa ni vikubwa na kwamba hakuna mwenye uwezo wa kuvivaa ndani ya CHADEMA yanapodhihiri.
Hata hivyo, sina hakika kama CHADEMA wametafakari kwa kina kabla ya kufanya maamuzi hayo. Sina hakika pia kuwa CHADEMA wameshughulikia kiini cha Dr Slaa kujiuzulu Ukatibu Mkuu na kutimkia Ughaibuni kabla hawajamuomba kurejea chamani. Kwa kujikumbusha tu ni kwamba, Dr Slaa aliamua kujiweka pembeni baada ya wenye chama kulazimisha kumteua Fisadi Lowasa kuwa mgombea Urais wa chama hicho na mwamvuli wa UKAWA. Hicho ndicho kiini cha Dr Slaa kujiweka pembeni. Hivyo kama CHADEMA wana dhamira ya dhati ya kurejea kwenye misingi yake, wanapaswa kwanza kudeal na chanzo na si kufunika kombe ili mwana haramu apite.
Aidha, wakati CHADEMA wakichukua hatua hiyo ya kumuomba Dr Slaa kurejea chamani, Fisadi Lowasa ambaye alisababisha Katibu Mkuu huyo kutimka, ametangaza kugombea tena nafasi ya Urais kwenye uchaguzi Mkuu wa 2020. Hii maana yake ni kwamba, kama ilivyotokea 2015, ndivyo itakavyokuwa 2020. Mgombea ni yule yule na mazingira yaliyomkimbiza Dr Slaa ni yale yale.
Taarifa za chini chini zinasema kuwa Dr Slaa amekataa wito huo wa CHADEMA huku akihoji haya niliyoweka hapa JF kwa faida ya Watanzania wengi. Pia kuna nyeti nyingine kuwa huenda fisadi Lowasa anataka kuelekeza hasira zake kwa Dr Slaa ikiwa ni ule mkakati wake wa kuwashughulikia wale wote waliokwamisha ushindi wake. Hivyo kitendo cha viongozi waandamizi wa CHADEMA kumuomba Dr Slaa arejee chamani ni kama mtego kwa Dr huyo wa Theolojia ili akishafika tu chamani aangukie mikononi mwa wabaya wake ambao wamejipanga kisawasawa kumshughulikia kwa namna watakayoona inafaa.
Hapa sasa ninapokumbuka misemo kadhaa ya kiswahili. USITUKANE MAMBA KABLA HUJAVUKA MTO; USITUKANE WAKUNGA WAKATI UZAZI UNGALIPO; SIZITAKI MBICHI HIZI nk. Kejeli, dharau, matusi, vitisho na kila aina ya upuuzi ulioelekezwa kwa Dr Slaa na wafuasi, viongozi, wapenzi na makada wa CHADEMA na UKAWA sikutegemea kama wangekuwa na ujasiri wa kumuomba Dr Slaa kurejea chamani.