John Heche ni makamu Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (
CHADEMA) Taifa, ambaye pia amewahi pia kuwa mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini. CHADEMA inaendelea kuendesha kampeni 'No reforms No election' ikiwa na lengo la kudai na kuhimiza mbadiliko mbalimbali kwenye mifumo ya uchaguzi ikiwemo sheria za uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2025 kuwa huru na haki.
Mnamo tarehe 12 Mei, 2025 Heche aliongoza muendelezo wa mikutano ya hadhara kanda ya ziwa ikiwa ni sehemu ya kuwafikishia wananchi ujumbe kuhusu kampeni hiyo.
Mkutano huo ulifanyika Igoma jijini Mwanza.
Madai
Kutokana na mkutano huo, kipo kipande cha video kilichochapishwa mtandaoni kikimuonesha Heche akifananisha kati ya Rais Samia na Tundu Lissu huku zikisikika sauti zinazosema 'mama'
Uhalisia
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa video hiyo imepotoshwa uhalisia wake kwa kuongezewa sauti zinazosema 'mama'
Katika hotuba yake sehemu hiyo Heche alikuwa akizungumzia baadhi ya wanachama waliolalamikia kukatishwa ndoto zao za Ubunge kwa sababu ya ajenda ya 'No reforms, No election' akisema chama hicho hakikuanzishwa kwa sababu ya ndoto ya watu fulani kuwa wabunge na madiwani bali ndoto ya wananchi kujikomboa kutoka kwenye umasikini.
"Hiki chama hakikuanzishwa kwa sababu ya ndoto ya watu fulani kuwa wabunge na madiwani, hiki chama kilianzishwa kama ndoto ya wananchi kuondoka kwenye umasikini na kwenda kwenye nchi ya ahadi. Kwa sasa tunataka kwanza maslahi ya wananchi yasimame." rejea
hapa
Vilevile aliongeza kuwa yeye mwenyewe ana ndoto ya kuwa mbunge, Lissu ana ndoto ya kuwa Rais, akaongeza kwa kuhoji akisema
"hivi kweli kama ni suala la ndoto, hivi Lissu akisimama hapa na huyu mama akasimama hapa ikagongwa dakika 90 ya kweli nani anasimama hapa?" (Zinasikika sauti za wananchi zikisema Lissu) Rejea
hapa
View: https://www.youtube.com/live/Cji0NY5Xbtw?si=o6DgBGnrjyfsJqrs