Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,193
- 299
- Thread starter
-
- #61
Acha Ujinga mkuu na acha kuwa kama wale wanao Chora Zombi, kwa hiyo vyama kama REPBLICAN Cha USA ni chama cha Kidini, Conservative, kwa kifupi viko vingi sana na orodha ni ndefu sana na nilisha wahi kuileta humu day one, so hata ODM ni chama cha Kidini? Na unajua ukiachilia IDU muungani mwingine unaitwa nini? ambao una vyama kama Democratic na kazalika,
Kuhusu kusapoti hiyo iko wazi kabisa, na inaruhusiwa kabisa na kila mtu anajua hilo, na hata CCM hawawezi ongea chochote maana wanajua na Mkuu kisicho ruhusiwa ni Nchi kusapoti Mgombea fulani wa chama fulani kwenye Uchaguzi, kufanya hivyo ni kujatafutia matatizo na hata kuvunjika kwa uhusiana pale ambapo mlio kuwa mnamtarajia hakushinda na kashinda mpinzani wake,
Kwa Vyama hakuna kitu kama hicho make Vyama na Setikali ni Vitu viwili tofauti kabisa
Chadema yambeba Odinga
JUMATATU, MACHI 04, 2013 06:21 NA ARODIA PETER, NAIROBI
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
*Kilimtumia magari, wasanii kuzunguka nchi nzima
WAKATI wananchi wa Kenya leo wanatarajia kupiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeonekana kumbeba mgombea urais kupitia Chama cha ODM ambacho kimo ndani ya Muungano wa CORD, Raila Odinga, kwa kupeleka magari na timu ya wasanii kumsaidia wakati wote wa kampeni zake.
Chadema ambao wanadaiwa kuwa rafiki mkubwa wa Odinga, kilituma magari mawili aina ya Fuso kwa ajili ya kumpigia kampeni ambazo zimedumu kwa mwezi mmoja.
Mbali ya kutuma magari hayo, Chadema walituma kikundi cha wasanii kikiongozwa na mwimbaji maarufu wa chama hicho, Fulgance Mapunda 'Mwanakotide.
Habari kamili: Chadema yambeba Odinga
Hivi huu ni mchezo mzuri kwa CHADEMA na Tanzania kwa ujumla kujiingiza katika siasa za mataifa mengine? Je kuna faida gani na hasara zipi za vitendo kama hivi? Ni nani anayefaidika na uingiliaji huu, CDM, Odinga au viongozi wa CDM? Je hii haihatarishi usalama wa mataifa yetu yote kwa kushabikia <50% ya waKenya?[/QUOTEI
ID yako tu tosha..
Mnapojenga hoja hapa, jaribuni kuangalia pia athari zake.
Kwa hiyo mnataka kutuaminisha kuwa CHADEMA inafanya kile ambacho CCM walikifanya kwa Malawi?.
Kama hivyo ndivyo, Sasa kipi ni tofauti ya CHADEMA na CCM kama vyote vinafanya vivyo hivyo kwa maana kwamba hata madudu ya CCM nao CHADEMA kikiingia madarakani kina ruhusa kuyafanya pia kwa vile CCM kiliyafanya.
Tunasubiri kuona CCM wakipiga kelele kuhusu hili na mwanasheria mkuu awafungulie mashitaka CHADEMA.Kuhudhuria na kusaidia kwenye kampeni ni vitu viwili tofauti kabisa. Kuhudhuria hakumaanishi kuwa active kwenye maswala ya huyo aliyewaalika zaidi ya kuwa mtazamaji. Kujihusisha kwenye maswala ya kampeni ni kuvuka mipaka ya kuwa mtazamaji na kuwa ni muhusika hai. Katika macho ya mahusiano ya kimataifa na dipromasia, hili ni kosa.
Nilikujibu kutokana na counter argument yako kwa kubwajinga pale uliposema,
CCM walifanya makosa makubwa kufanya hivyo hasa ikizingatiwa kuwa ni chama ambacho kilikuwa kinaongoza serikali. Hii pia haiwapi CHADEMA tiketi ya kufanya madudu ya waliyofanya CCM.
Kweli kabisa mkuu, tena baada ya hizo kampeni Komba akapewa zawadi ya shule. Kuna Shule hipo kule mbweni inaitwa Bakili Muluzi Sec. inamilikiwa na huyu komba...
Kwa hiyo Islamic Coalition Party ya Iran ikiwatumia CCM helcopta 20 na pesa $100,000,000 ili washinde uchaguzi 2015 wewe utajisikiaje?
Kwa sababu uko UK ni lazima useme kwamba unayajua magari ya Odinga. Pfyuuuuuuuuuuuuuuuu
unashangaa?chadema ndo zao hizo,yaani wameshaweka mia kwa mia kuwa odinga anashinda.VIPI AKISHINDA UHURU?si ndio mambo ya aibu hayo.Kama habari hii ni ya kweli, CDM wamefanya kitu cha kipuuzi na kipumbavu.
Wewe umefurahi watoto woote nchi nzima SIXTY % kufeli, kwa hiyo CHADEMA ni mazumbukuku??? Unataka waziri aendelee kutuletea matahira kwenye system ya nchi yetu, na kwa nini asijiudhuru????unashangaa?chadema ndo zao hizo,yaani wameshaweka mia kwa mia kuwa odinga anashinda.VIPI AKISHINDA UHURU?si ndio mambo ya aibu hayo.
Juzi hapa wanampa kawambwa siku 14,aache kazi au la kitawaka.siku zimeisha nasikilizia watafanyaje .
kwahiyo mtu akitaja iran tu tayari amekua mdini?.Wewe mbona ni mugumu sana kuelewa? kwa nini unashindwa kukubali baada ya kugundua kuwa uliweka hii post yako pasipokuwa na utafiti na watu wanaojua wameshakujibu kuwa hiki ni kitu ambacho kinakubalika kimataifa!
Wewe umebaki na na mambo ya uisilamu tu, hivi ni kwanini mifano yako yote inalenga huko? Au ndo udini unakusumbua mwenzetu!
Jibu ni kwamba kama CCM wana uhusiano na vyama hivyo basi wako huru kupokea lakini!
Mkuu hujanielewa siwezi kuipinga M4C abadani,masisiem ndo nilikuwa nayapa kubwa kila siku yanakurupuka na Chadema utafikiri ndio matatizo ya hii nchi...Meza nyembe Mkuu hiyo ndiyo M4C, inaonekana umekereka!!!
kwahiyo hao kufeli kasababisha shukuru?kama ndiyo HOW?.Wewe umefurahi watoto woote nchi nzima SIXTY % kufeli, kwa hiyo CHADEMA ni mazumbukuku??? Unataka waziri aendelee kutuletea matahira kwenye system ya nchi yetu, na kwa nini asijiudhuru????
Wewe mbona ni mugumu sana kuelewa? kwa nini unashindwa kukubali baada ya kugundua kuwa uliweka hii post yako pasipokuwa na utafiti na watu wanaojua wameshakujibu kuwa hiki ni kitu ambacho kinakubalika kimataifa!
Wewe umebaki na na mambo ya uisilamu tu, hivi ni kwanini mifano yako yote inalenga huko? Au ndo udini unakusumbua mwenzetu!
Jibu ni kwamba kama CCM wana uhusiano na vyama hivyo basi wako huru kupokea lakini!
KINGMAKER Rostam nae alikuwepo hapo.Mkuu na waziri Makufuli nasikia alikuwa huko akihamasisha wapiga kura, basi na yeye sasa amegeuka CHADEMA???