Polisi hawapaswi kuwazuia CHADEMA kufanya mikutano. Lakini labda CHADEMA wanataka kuendelea na harakati za Uchaguzi wakati Uchaguzi umekwisha. Conservatives waliposhinda Uingereza,jambo la kwanza lililotokea,David Cameron aliunda Cabinet,pamoja na Lib Dems.
Labour waliposhindwa,jambo la kwanza kabisa,Ed Millerband,kiongozi wa Labour,aliunda Shadow Cabinet. Hawaendelei na Kampeni za Uchaguzi. Ile Shadow Cabinet inaipinga Serikali,siyo tu katika Bunge,lakini,kila wakati.
Yaani wao wana politics ambayo Shadow Cabinet itapingana na Real Cabinet,mpaka siku ya election. Hiyo diyo politics yao. Kwa hiyo mikutano ambayo CHADEMA wanayotaka kufanya sasa hivi siyo politics,ni kukengeua from real politics kama inavyofanywa katika Nchi nyingine zote. Katika Uchaguzi Mku wanabishana hilo tu,kwamba kama watafanikiwa kuunda Real Cabinet,au kama itawabidi kuridhika kuunda Shadow Cabinet.
Waunde Shadow Cabinet wabishane na Serikali ndani na nje ya Bunge. Hawahitaji kufanya mkutano wa hadhara.
Mkuu,
Hii exclusive ya kwamba wanataka kuendelea na kampeni za uchaguzi unaitoa wapi? Uchaguzi gani huu usiotambulika na tume?
Unasema "Hawahitaji kufanya mikutano ya hadhara"? Swala hapa si wanahitaji au hawahitaji, swala ni, wana haki hiyo au hawana haki hiyo? Ukimkuta mtu anachezea hela yake kamari unawezaje kusema "hahitaji kucheza kamari" ? Swala siyo kwamba anahitaji au hahitaji, anaweza kuwa mpumbavu na hana busara, watoto wanalala njaa na yeye anacheza kamari, unaweza kusema "kucheza kamari si busara" lakini kusema "hahitaji kucheza kamari" ni kama umeingia kichwani mwake na kujua ana addiction gani, pengine kamari ndiyo ulevi wake na anahitaji kucheza kamari, sasa utasemaje hahitaji kucheza kamari ? This is a question of constitutional rights, and once you are talking about constitutional rights, these rights are blanketing, provided you do not break the law.
Ninachoona hapa ni kwamba polisi wanahukumu kabla sheria haijavunjwa. Wananikumbusha Saddam Hussein alikuwa na msemo wake mmoja
"I know a traitor even before he betrays me". Saddam alituambia akikutana na wewe tu, mkisalimiana tu, anaweza kukujua kwamba wewe siku moja utamsaliti au la, hivyo aliweza hata kutoa order ya kukuua based on this divination. Is our police divining in this Saddam Hussein style?
Nangojea ripoti za mwaka za mashirika ya kimataifa (Amnesty International etc) nione Tanzania imepanda ngazi za udhalimu kutokana na jambo hili.This is not a good look.
Siamini kwamba polisi pekee wana uwezo wa kuzuia mikutano, kuna amri kutoka juu yao.
Hatuwezi kuwa na polisi inayokataza watu wasitumie haki zao za kikatiba kukutana just because kuna a possibilities watavunja sheria, what's next? Polisi watazuia watu wasitoke nje ya nyumba zao kwa sababu watavunja sheria?
Narudia msemo wa Ben Franklin
"Those who sacrifice their freedom for security deserve neither"