Chadema yalaani kuzuiwa mikutano........................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
225,247
856,556
Gazeti la Majira leo lina kichwa cha habari kisemacho.....................Chadema yalaani kuzuiwa mikutano....................................

Huku gazeti la Tanzania Daima nalo lasema.............................Chadema;Hatukubali kunyamazishwa.......................................Yote haya yatokana na polisi kuwazuia kufanya mikutano ya kuwashukuru wapigakura wao na kuwaelezea mkasa mzima wa jinsi NEC ilivyowapora ushindi wa Uraisi................................

Kwa nchi inayofuata demokrasia hii ni aibu kwa serikali ya CCM iliyopo madarakani kuwazuia Chadema kufaidi haki yao ya kimsingi ya kufanya mikutano ambayo ni haki ya kikatiba...........................
 
Bila shaka wanafanyia kazi hili na hawakomei kulalama, kelele za mlango hazimzui mwenye nyumba kulala, zinaweza kama huo mlango utapigishwa kwa nguvu na kutishia kuvunjika kwa huo mlango
 
mhhh JK bana na serikali yako..sasa ukifanya hivo ndo nini au ndo utahalalishwa kuwa hujaiba kura
 
Kuna mikutano muhimu sana hapo baadae kidogo ambayo itabidi ikubaliwe kwa njia yoyote iwe kwa amani au kwa kumwaga damu potelea mbali,ila kwa sasa tuwape Polisi nafasi ya kutekeleza amri ya bosi wao.
Tuwe na subira wananchi.uamuzi wa Mwenyekiti na chadema kwa ujumla wa kukaa kimya maana yake kuna jambo la kubwa ambalo linatakiwa lifanyike kabla ya uchaguzi 2015.
subira yavuta heri....!!!!
haraka haraka haina baraka
mwenda pole hajikwai.na akijikwaa keshapata kama CUF ZENJ....teh...teh....teh...
 
mi nazani kelele zao zitawafanya polisi kujuwa kuwa wao ni kikwazo cha chadema kutokufanya kile walichokusidia,lakini pia ni kufikisha ujumbe kwa jamii tz kutambuwa kuwa jeshi letu la polisi lipo kwa maslahi ya chama kimoja kwani tayari sehemu nyingi ccm wamepewa nafasi ya kuwashukuru wapiga kura wao,ila chadema wakiomba ili wawashukuru wapiga kura kwa kuwaunga mkono,polisi wanadai kuwa bado nchi haipo ktk hali nzuri kiusalama,sasa hatuelewi kwanini iwe kwa chadema tu na sio ccm?

mapinduzii daimaaaa
 
Gazeti la Majira leo lina kichwa cha habari kisemacho.....................Chadema yalaani kuzuiwa mikutano....................................

Huku gazeti la Tanzania Daima nalo lasema.............................Chadema;Hatukubali kunyamazishwa.......................................Yote haya yatokana na polisi kuwazuia kufanya mikutano ya kuwashukuru wapigakura wao na kuwaelezea mkasa mzima wa jinsi NEC ilivyowapora ushindi wa Uraisi................................

Kwa nchi inayofuata demokrasia hii ni aibu kwa serikali ya CCM iliyopo madarakani kuwazuia Chadema kufaidi haki yao ya kimsingi ya kufanya mikutano ambayo ni haki ya kikatiba...........................

CHADEMA wamejichanganya wenyewe, POLISI walitaka kujua dhamira ya mikutano yao. Wao wakasema ni kwa ajili ya kupongezana, sasa Polisi wakasema kama kupongezana ni lazima kwa maandamano ? kwa nini wasifanye hafla za kupongezana kwenye kumbi za ndani ?. Hapo ilionyesha kabisa wanacho kisema sio wanacho dhamiria
 
Jamani nendeni mahakamani, ili mpate hiyo haki. kazi ya LISU. Hiyo kesi ipo wazi muipeleke kama hati ya dharura.
 
Polisi hawapaswi kuwazuia CHADEMA kufanya mikutano. Lakini labda CHADEMA wanataka kuendelea na harakati za Uchaguzi wakati Uchaguzi umekwisha. Conservatives waliposhinda Uingereza,jambo la kwanza lililotokea,David Cameron aliunda Cabinet,pamoja na Lib Dems.
Labour waliposhindwa,jambo la kwanza kabisa,Ed Millerband,kiongozi wa Labour,aliunda Shadow Cabinet. Hawaendelei na Kampeni za Uchaguzi. Ile Shadow Cabinet inaipinga Serikali,siyo tu katika Bunge,lakini,kila wakati.
Yaani wao wana politics ambayo Shadow Cabinet itapingana na Real Cabinet,mpaka siku ya election. Hiyo diyo politics yao. Kwa hiyo mikutano ambayo CHADEMA wanayotaka kufanya sasa hivi siyo politics,ni kukengeua from real politics kama inavyofanywa katika Nchi nyingine zote. Katika Uchaguzi Mku wanabishana hilo tu,kwamba kama watafanikiwa kuunda Real Cabinet,au kama itawabidi kuridhika kuunda Shadow Cabinet.
Waunde Shadow Cabinet wabishane na Serikali ndani na nje ya Bunge. Hawahitaji kufanya mkutano wa hadhara.
 
Jamani nendeni mahakamani, ili mpate hiyo haki. kazi ya LISU. Hiyo kesi ipo wazi muipeleke kama hati ya dharura.

CDM wasjaribu kwenda mahakamani kwa swala kama hilo kwani hiyo hukumu itachukua miaka 4 unajua tena mahakama zetu, na ndo itakuwa sababu kuwa hawazungumzii swla ambalo liko mahakamani au wanasubiri maamuzi ya mahakama :angry:
 
To follow legal redress is always the good option hata kama haki itacheleweshwa, kukaa kimya ni dalili ya aidha kukubaliana au cowardice, na CDM si wa aina hiyo....Mandela alikaa 27 years in prison bila kukata tamaa wala kukubaliana na mfumo wa apartheid, je mwishowe hakupata alichokipigania na kukuamini miaka yote?
 
Polisi hawapaswi kuwazuia CHADEMA kufanya mikutano. Lakini labda CHADEMA wanataka kuendelea na harakati za Uchaguzi wakati Uchaguzi umekwisha. Conservatives waliposhinda Uingereza,jambo la kwanza lililotokea,David Cameron aliunda Cabinet,pamoja na Lib Dems.
Labour waliposhindwa,jambo la kwanza kabisa,Ed Millerband,kiongozi wa Labour,aliunda Shadow Cabinet. Hawaendelei na Kampeni za Uchaguzi. Ile Shadow Cabinet inaipinga Serikali,siyo tu katika Bunge,lakini,kila wakati.
Yaani wao wana politics ambayo Shadow Cabinet itapingana na Real Cabinet,mpaka siku ya election. Hiyo diyo politics yao. Kwa hiyo mikutano ambayo CHADEMA wanayotaka kufanya sasa hivi siyo politics,ni kukengeua from real politics kama inavyofanywa katika Nchi nyingine zote. Katika Uchaguzi Mku wanabishana hilo tu,kwamba kama watafanikiwa kuunda Real Cabinet,au kama itawabidi kuridhika kuunda Shadow Cabinet.
Waunde Shadow Cabinet wabishane na Serikali ndani na nje ya Bunge. Hawahitaji kufanya mkutano wa hadhara.

Mkuu,

Hii exclusive ya kwamba wanataka kuendelea na kampeni za uchaguzi unaitoa wapi? Uchaguzi gani huu usiotambulika na tume?

Unasema "Hawahitaji kufanya mikutano ya hadhara"? Swala hapa si wanahitaji au hawahitaji, swala ni, wana haki hiyo au hawana haki hiyo? Ukimkuta mtu anachezea hela yake kamari unawezaje kusema "hahitaji kucheza kamari" ? Swala siyo kwamba anahitaji au hahitaji, anaweza kuwa mpumbavu na hana busara, watoto wanalala njaa na yeye anacheza kamari, unaweza kusema "kucheza kamari si busara" lakini kusema "hahitaji kucheza kamari" ni kama umeingia kichwani mwake na kujua ana addiction gani, pengine kamari ndiyo ulevi wake na anahitaji kucheza kamari, sasa utasemaje hahitaji kucheza kamari ? This is a question of constitutional rights, and once you are talking about constitutional rights, these rights are blanketing, provided you do not break the law.

Ninachoona hapa ni kwamba polisi wanahukumu kabla sheria haijavunjwa. Wananikumbusha Saddam Hussein alikuwa na msemo wake mmoja "I know a traitor even before he betrays me". Saddam alituambia akikutana na wewe tu, mkisalimiana tu, anaweza kukujua kwamba wewe siku moja utamsaliti au la, hivyo aliweza hata kutoa order ya kukuua based on this divination. Is our police divining in this Saddam Hussein style?

Nangojea ripoti za mwaka za mashirika ya kimataifa (Amnesty International etc) nione Tanzania imepanda ngazi za udhalimu kutokana na jambo hili.This is not a good look.

Siamini kwamba polisi pekee wana uwezo wa kuzuia mikutano, kuna amri kutoka juu yao.

Hatuwezi kuwa na polisi inayokataza watu wasitumie haki zao za kikatiba kukutana just because kuna a possibilities watavunja sheria, what's next? Polisi watazuia watu wasitoke nje ya nyumba zao kwa sababu watavunja sheria?

Narudia msemo wa Ben Franklin "Those who sacrifice their freedom for security deserve neither"
 
CDM wasjaribu kwenda mahakamani kwa swala kama hilo kwani hiyo hukumu itachukua miaka 4 unajua tena mahakama zetu, na ndo itakuwa sababu kuwa hawazungumzii swla ambalo liko mahakamani au wanasubiri maamuzi ya mahakama :angry:

Hili ndilo linalosababisha tukwame nchini mwetu, attitudes za kuogopa legal battles za miaka minne.

Hivi hujui hata kama hili litachukua miaka minne, lita set precedent kwa vizazi vyote vijavyo? Miaka minne ni nini kwa maelfu ya miaka yajayo? Tusiwe na mawazo ya kuangalia kesho tu.

CHADEMA kila siku inasema kwamba utawala wa CCM ni dhalimu na unatumia vyombo vya dola kuinyanyasa CHADEMA. Mpaka sasa ushahidi ni anecdotal zaidi, hii issue inaweza kwenda kutoa ushahidi unaotakiwa ama katika mahakama ya sheria ama kama watashindwa katika mahakama ya sheria kwa kuwa mnasema mahakama ni za CCM (by the way mahakama za juu zinajitahidi siku hizi kuwa impartial) wanaweza kushinda mioyo ya watu na katika mahakama ya public opinion.

Lakini ili kushinda squarely katika either court, that of law or that of public opinion, inabidi wafungue kesi na kuipigania kwanza. Ama sivyo wataonekana walalamishi tu wasio na facts za kuwa back up wala passion na wanachokisema.
 
Kufanya mikutano ni haki ya msingi,serikali ya chama cha mapinduzi iache ubabe,igp mwema awaruhusu chadema wafanye mikutano yao kwani ni haki yao ya msingi.
 
Kiranga;1316148]Hili ndilo linalosababisha tukwame nchini mwetu, attitudes za kuogopa legal battles za miaka minne.

Hivi hujui hata kama hili litachukua miaka minne, lita set precedent kwa vizazi vyote vijavyo? Miaka minne ni nini kwa maelfu ya miaka yajayo? Tusiwe na mawazo ya kuangalia kesho tu.

CHADEMA kila siku inasema kwamba utawala wa CCM ni dhalimu na unatumia vyombo vya dola kuinyanyasa CHADEMA. Mpaka sasa ushahidi ni anecdotal zaidi, hii issue inaweza kwenda kutoa ushahidi unaotakiwa ama katika mahakama ya sheria ama kama watashindwa katika mahakama ya sheria kwa kuwa mnasema mahakama ni za CCM (by the way mahakama za juu zinajitahidi siku hizi kuwa impartial) wanaweza kushinda mioyo ya watu na katika mahakama ya public opinion.

Lakini ili kushinda squarely katika either court, that of law or that of public opinion, inabidi wafungue kesi na kuipigania kwanza. Ama sivyo wataonekana walalamishi tu wasio na facts za kuwa back up wala passion na wanachokisema.

Heri kubaki walalamishi kuliko kwenda mahakamani CDM, Mahakama ya kweli ya CDM ni kwenda kwa wananchi maana ndio majaji wasiokula rushwa na watoaji maamuzi sahihi.
 
Heri kubaki walalamishi kuliko kwenda mahakamani CDM, Mahakama ya kweli ya CDM ni kwenda kwa wananchi maana ndio majaji wasiokula rushwa na watoaji maamuzi sahihi.

Utasemaje majaji wanakula rushwa wakati hujapeleka kesi mahakamani? Tanzania high courts siku hizi zinaendeshwa kwa some semblance of integrity, wanajua watu wanawaangalia, weka ushahidi wazi, peleka mahakamani.

Zaidi ya hapo utaonekana mzushi tu, na labda unaogopa kwenda mahakamani kwa sababu huna ushahidi wala vifungu vya kukutetea. Wakati una katiba inakutetea.

Court of public opinion nayo hamuwezi, mnatoka bungeni, ina backfire mpaka mnasema "wananchi hawajatuelewa". Nyie CHADEMA vipi ?
 
Kufanya mikutano ni haki ya msingi,serikali ya chama cha mapinduzi iache ubabe,igp mwema awaruhusu chadema wafanye mikutano yao kwani ni haki yao ya msingi.

IGP kashakataa, swala sasa haliko kwa IGP, lipo kwa CHADEMA, watauchukuliaje uamuzi huu? Watafanya nini?
 
IGP kashakataa, swala sasa haliko kwa IGP, lipo kwa CHADEMA, watauchukuliaje uamuzi huu? Watafanya nini?
kiranga nafikiri ulizaliwa wakati watu wanabishana ndo maana unabisha kuhusu rushwa Tz! Leo nenda sehemu yeyote halafu waulize wananchi kama kuna haki inatendeka mahakamani! Siyo lazima uchemshe yai kwa dakika 5 ndipo ujue yai huiva kwa dakika 5.
 
Kwa hiyo CHADEMA itaiondoa rushwa mahakamani kwa kususia mfumo wa sheria au kwa ku expose mfumo wa sheria?

Unaelewa distinction niliyoitoa kati ya mahakama za chini na mahakama za juu? Unaijua Mahakama ya Rufaa Tanzania na historia yake kuhusu kesi za kisiasa? Umeona precedents za watu kama majaji Francis Nyalali, Kahwa Lugakingira na Robert Kisanga, nikiwataja wachache tu, katika kutoa rulings na findings zilizo sema kweli kwa watawala ?

Tatizo hapa ni kwamba mna defeatist attitudes, na huwezi kushinda hata siku moja kama ukiwa na defeatist attitude. You gotta play to win. Peleka kesi mahakamani, tuonyeshe ushahidi, hata kama ni wa kimazingira tu, kwamba CCM inatumia mahakama kuwaminya CHADEMA. Tupe vifungu vya katiba vinavyovunjwa na Polisi, tuonyeshe kwamba polisi hawana nguvu wala haki ya kuzuia political association, wananchi si wajinga, tutaona. Wajuzi wa sheria watachambua mambo, mta expose hilo.

Sio hata kabla hamjapeleka kesi mahakamani mshaanza kuji defeat wenyewe kwa hypothetical situations, wananchi tutawaona walalmishi mnao argue theoretically bila factual backing.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom