CHADEMA yaitupa kapuni Rufaa ya Zitto

amakyasya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
3,480
Reaction score
918
Maombi ya rufaa ya ZITTO KABWE hayatajadiliwa hadi hatima ya uanachama wake kujulikana.

 
Kwani hili suala hatima yake ni nini?
Au limekuwa la kipolitiki zaidi? For whose advantage?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakitashughulikia rufaa iliyokatwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kwa Baraza Kuu kupinga uamuzi wa Kamati Kuu (CC) wa kumvua nyadhifa zake katika chama, hadi hapo itakapopitia utetezi wake na hatma ya uanachama wake katika chama hicho.

"Kuna kitu kikubwa mbele yake kabla ya kusikiliza rufaa, huwezi kuongea juu ya rufaa wakati hujajua uanachama wao kwanza" alisema Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Victor Kimesera.

Source: Gazeti la Nipashe.
 
Wasaliti wenzake amewaona huko Ukrine, Korea, China Na South Africa ataona hivi karibuni. Zitto has picked so early
 
Suala la Uanachama na Uongozi vilikuwa ni separate issues. Kila kimoja kilipaswa kijadiliwe kwa muktadha wake!.
Mpaka hivi sasa Zitto Kabwe ni mwanachama halali wa Chadema
Anakata rufaa kwa sababu ya Kuvuliwa uongozi wake, Then Mwingine aakuja anasema No No No, Subiri kwanza tuone kama utavuliwa uanachama au La!!- SIJAWAHI KUONA CHAMA AMBACHO KILA MTU ANAJITAFSIRIA KATIBA APENDAVYO!
Sijui Kimesera ametumia kifungu gani cha sheria/katiba ya Chama kuzuia Mchakato huru wa Rufaa
 
Zitto sijui hata shuleni alikuwa anafaulu vipi..kapewa tuhuma anatakiwa azijibu yeye anakata rufaa?huyo dongo pimbi nini
 
Ni suala ambalo daima hufanywa kwa umakini
mkubwa hasa kuepusha manung'uniko
tatizo baadhi tunapenda maamuzi ya haraka.

Ambayo huwa yanakuwa na mitazamo tofauti
tuwe na subira kila kitu kitajulikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…