CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

Kwenye fedha ndiko tunataka kusikai watasema nini maana Mbowe katuhumiwa kula pesa nk .Kwenye fedha tunataka kuona Changes na signatories wanakuwa watu ambao ni watendaji na Mbowe aachie sahihi . Chadema wawe na Accountant ambaye hataliliwa kwamba ni mchaga .

Inategemea katiba yao inasema nini juu ya hilo. Kumbuka mapandikizi wako wengi na hapo ndo wanajua nguvu ya chama imeegema hapo!!! si masihara signatories kuwateua bila kutumia umakini.
 
Please wenye updates za yaliyojiri na yanayojiri kama bado kikao kinaendelea tafadhali tuleteeni hapa.
 
Mkuu mbona agenda ya Kafulila & Juju sijaiona? au mtawajadili/mliwajadili kwenye mengineyo? au sisimizi hawajadiliwi? na hili la zitto kuwapa nccr mageuzi magari kwa ajili ya kampeni ya kafulila mmeliangaliaje?
ni hayo tu mkuu.
Kupanga shughuli za kutekeleza Mpango Mkakati wa chama kuelekea uchaguzi wa mwaka 2010.
Hiyo ndiyo ajenda itakayobeba kila kitu; utakuwa si ukomavu wa kisiasa kuweka ajenda inayosema 'kujivua uanachama Kafulila na Juju'
 
Kwenye Mwanahalisi la 165 inasema, CHADEMA: Chuki na visasi vya mawifi. Kwenye hitimisho anasema " Wanajiondoa au wanaojiandaa kujiondoa chedema wanafanya kazi moja nzuri - ile ya kujisafisha kwa njia ya kusafisha chama. Hata hivyo wasinyee kambi kwani hizo ni siasa za visasi vya mawifi; kwani siku moja waweza kujikuta wakirejea nyumbani. wamuulize Guninita". I LOVE IT, Thanks Ndimara
 
Nilipoona tuu headline, nikaingia kichwa kichwa!, du!, kumbe nimeingia chaka!.
Enzi hizo jf, taarifa ya kikao muhimu kama hiki, page mbili tuu, sasa hivi pandisha lolote kuhusu Chadema!, thread inagombewa kama mpira wa kona!, na ikimhusu ZZK, then inavamiwa lundo kama mainzi kwenye utumbo wa jana!
Happy New Year Wanachadema wote!.
Ni mimi nisiye na chama, ila nawafuatilia kwa karibu sana kufuatia ni fedha zangu zinazoiendesha Chadema!.
Nawatakia kikao chema hiyo 04/01/2014.
Pasco
 
Mbona wameandika '' imetolewa tar 2 Disemba 2009 ? Is this a typo error? Or this meeting took place five years ago?
 
Ivi pale kwa mfipa hakunaga ukumbi wa mikutano.

Mimi hupata tabu sana si kiduchu,
Kwani hawa watu wao ndio wa kwanza kuleta mambo yao ya chama humu mtandaoni na katika mitandao mingine hasa kwa kumlenga mtu / watu fulani ,

Na mara tu mlengwa naye aanzapo kujibia mapigo, huambiwa kwanini anapeleka mambo mitandaoni....?

Acheni mbichi hizo bana,

Na hizo tarehe ulizoweka hao ni sahihi mlitafutia sababu tangu miaka hiyo ama tukupe nafasi ya kujitetea?
 
Pasco unawatafuta watu, nikiangalia post yako na 27 hapo juu, naona kabisa post na 26 ni ya tar 4 Dec, 2009. Hakuna uwezekano wa kwamba umekuta kichwa cha habari hapo juu, sema umeitafuta hii thread.

By the way naona michango mingi inayolalamikia mabo yale yale ya leo, usaliti, unafiki, signatories etc. Na hizi nyimbo haizitakaa zichuje CDM as long as waanzilishi na matajiri wa chama ndio wenye maamuzi. Tutaisikia tena na tena, leo kwangu, kesho kwako.
 
Last edited by a moderator:
Na hizi nyimbo haizitakaa zichuje CDM as long as waanzilishi na matajiri wa chama ndio wenye maamuzi. Tutaisikia tena na tena, leo kwangu, kesho kwako.

Sijaona ile korasi ya magamba ya Udini, labda ilisahaulika kidogo!
 
Unatoa pole kwa huyo mwa sisi wako unasahau kutoa pole kwa msiba wa Mgimwa Waziri aliye kuwa anakulipa ruzuku ulizo kuwa unajikopesha??? Shame on youuuuuuu Slaaaaas
 
wanafiki watupu hawa..,wanadiscuss nini...watu wanazulumiwa kura zao wanashindwa kutoa hata mchango wa wakili ati jichangisheni muende mahakamani...dems chama....ndio maana kafulila maneno yake yasipoaminiwa hivi sasa yataaminiwa na wajukuu wa chadema ipo siku

Jitahidi kuwa mwangalifu!!!!!!!!!!!!!!!!!
Hii taarifa ya December 2,2009 na sio Jananuary 2,2014.
 
Back
Top Bottom