CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John Mnyika, Dec 2, 2009.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Dec 2, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Issued exclusively through JF; press corps, feel free to use it in your stories tommorrow:  TAARIFA KWA UMMA

  Taarifa inatolewa kwa umma na kwa vyombo vya habari kwamba Kamati Kuu ya CHADEMA inaendelea na kikao chake cha kawaida kilichoanza saa 5 asubuhi Dar es salaam katika Hoteli ya Keys Mbezi leo tarehe 2 Disemba na kikao hicho kitamalizika kesho tarehe 3 Disemba 2009.

  Ajenda za kikao hicho ni: Yatokanayo na muktasari wa Kikao kilichopita; Hali ya Siasa Tanzania; Tathmini ya Uchaguzi wa Vijiji, Mitaa na Vitongoji; Kupanga shughuli za kutekeleza Mpango Mkakati wa chama kuelekea uchaguzi wa mwaka 2010; Kuthibitisha Makatibu wa Wilaya/Mikoa na sekretariati zao; Taarifa za Rufaa mbalimbali za uchaguzi wa ndani ya chama; Taarifa ya Zanzibar; Taarifa kuhusu Mfumo wa uanachama kwa njia ya kieletroniki (E-Membership); Taarifa ya Fedha; Uteuzi wa Bodi ya Wadhamini; Tarehe za mikutano ya Baraza Kuu na Mkutano Mkuu.

  Aidha tunasikitika kupokea kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini na mmoja wa waasisi wa CHADEMA Kanali (Mstaafu) Geofrey Marealle kilichotokea jana usiku. CHADEMA inatuma salamu za pole kwa familia ya marehemu na wanaCHADEMA wote duniani kutokana na msiba huo. Salamu za rambi rambi zitatolewa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe mara baada ya kutaarifiwa utaratibu mzima wa mazishi toka kwa familia ya marehemu.

  Imetolewa tarehe 2 Disemba 2009 saa 11 jioni na Katibu Mkuu; Dr Wilbroad Slaa.
   
 2. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sawa Bw. Mnyika

  Mbona hakuna agenda ya kina kafulila na mwenziwe Juju na hii habari ya wanachama wanaotaka kujitoa kwa wingi
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mkuu mbona agenda ya Kafulila & Juju sijaiona? au mtawajadili/mliwajadili kwenye mengineyo? Au sisimizi hawajadiliwi? Na hili la Zitto kuwapa NCCR Mageuzi magari kwa ajili ya kampeni ya Kafulila mmeliangaliaje?

  Ni hayo tu mkuu.
   
 4. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,897
  Trophy Points: 280
  Tutaomba uendelee kutupasha hata baada ya kikao
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hao wamejitoa wenyewe Chadema, na hawajakata rufaa ya kuvuliwa vyeo vyao sasa agenda ni ya nini ilihali Katibu Mkuu alishalimaliza kila kitu!

  Sana sana Katibu huyo atatoa taarifa tu juu ya hao sisimizi pale itakapobidi.
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CHADEMA kazi nzuri sana,
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  wanafiki watupu hawa..,wanadiscuss nini...watu wanazulumiwa kura zao wanashindwa kutoa hata mchango wa wakili ati jichangisheni muende mahakamani...dems chama....ndio maana kafulila maneno yake yasipoaminiwa hivi sasa yataaminiwa na wajukuu wa chadema ipo siku
   
 8. C

  Charuka Member

  #8
  Dec 2, 2009
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ni kikao cha kawaida, au cha dharula?
   
 9. Y

  Yetu Macho JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  RIP- Marialle

  Chadema songeni mbele, msiyape muda mambo ya kina Kafulila na Juju maana wameondoka kama walivyoingia. Ni haki yao, ila ni muhimu sana mkazungumzia sana maadili ya uongozi (Kwenye mengineyo) maana tusipo wekana sawa hatutaweza linda imani kubwa watanzania waliyoanza kutuonyesha.

  Mnyika:- Tafadhali kwenye mengineyo hoji hatma ya chama hasa viongozi wa chama wanapojitokeza wazi wazi kuunga mkono mahasimu wa chama tena wale wanaotukana chama na viongozi wenzao. Nini mipaka ya uongozi na ushabiki wakiswahiba.

  Yetu macho
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Dec 2, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Naitakia kamati kuu kikao chema na chenye mafanikio katika kujenga na kuimalisha Chama chetu.
  Nawaaminia viongozi wetu kuwa mtafanya yaliyo kweli. Achana na propaganda za kijani, songeni mbele tuijenge nchi yetu kwa faida ya watoto na wajukuu wetu.
   
 11. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Vipi kikao cha kawaida inakuwa 'BREAKING NEWS!' kunani Chadema?
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Dec 2, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mimi ndiyo maana nasema members hapa ama JF tumepoteza mwelekeo . Yaani Kafulila kujiondoa kwenye Chama inatakiwa kuwa agenda ?Jamani waacheni watu wafanye kazi .Hiyo ni issue itakuja kwenye yatokanayo . Sasa kama kuna mtu anaka kujiondoa Chadema naye iwe agenda kwamba wawazuie ama iweje ?

  Kwenye fedha ndiko tunataka kusikai watasema nini maana Mbowe katuhumiwa kula pesa nk .Kwenye fedha tunataka kuona Changes na signatories wanakuwa watu ambao ni watendaji na Mbowe aachie sahihi . Chadema wawe na Accountant ambaye hataliliwa kwamba ni mchaga .
   
 13. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #13
  Dec 2, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Kakalenda aliye leta habari hii kama breaking news ni Chadema ama wao wametoa taarifa za Kikao ? Haya hayafanywi na CCM ama ndiyo mwelekeo wenyewe tumepoteza ana kwa huwa tunaweza kubonyeza hapa na ku hoji ?
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Dec 2, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  acha wajitoe kwa wingi maana wataingia wengine kwa wingi so hiyo sio hoja ya kujadili wala kuifanya ajenda
   
 15. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #15
  Dec 2, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280


  asante sna kiongozi kwa maneno hayo..hayo ndo ya msingi kuzungumza katika kikao hicho ili akina Ngoma Nzito na mwenzie Kanda2 watafute mengine ya kuongea
   
 16. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #16
  Dec 2, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo Mangi wanyang'anywe fursa ya kuwa wahasibu au
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Dec 2, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Unasema uko serious ama unapunguza uchovu ? Unadhani kwenda mahakamani kudai kuibiwa kura ndiyo jibu la shida ya uchaguzi TZ ? Kesi ngapi TZ hadi sasa nilienda Mahakamani na CCM wakashinda ? Hii si issue hapa ya kwenda Mahakamani mie nataka Chadema na wapinzi wote na sisi tuwaunge mkono na si kuwafunga kengele mnakimbilia JF kuandika kuunda Tume ya Uchaguzi ya wote ambayo JK haiteuwi hii ndiyo jibu na mwisho wa CCM . Lakini JF kama wakazi wa Dar .NI wajanja sana na husema sana wanaujua ukweli lakini serikali za mitaa wameipa CCM tena sasa akili hii ? Mnataka hao wapinzani mnaowapigia kelele waje kupiga kura hadi mitaani kwenu ?

  Issue si Mangi kutolewa kwenye Pesa ni kwamba Mbowe kama kweli anatuhumiwa kutumia vibaya pesa basi aondolewe ama aache kwa utashi wake ajiondoe awaachie wengine ndiyo maana ya mgawanyo wa kazi na madaraka. Wafanya siasa waendelee na watu wa pesa ambao ni Professionals wakiwa ni wanachama waaminifu waachwe wafanye kazi. Haiwezekani Komu awe accountant na kesho anasimama jukwaani huko mikoani pesa anatembea nazo ama inakuwaje? Chadema liangalieni hili.
   
 18. M

  Masatu JF-Expert Member

  #18
  Dec 2, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Lunyungu,

  Maneno yako ni sawia kabisa, na uzuri wako wewe unasimama kwenye ukweli hufuati upepo wa bendera.
   
 19. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #19
  Dec 3, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Mkuu, Kamati kuu ya chama haiwezi jadili individuals hiyo issue alishalizwa zamani na katibu mkuu wake basi.

  By the way hao watu ni kina nani as far as Chadema is concerned? nafikiri hata kuendelea kuwaongelea hapa kwenye JF ni makosa its like we dont have crucial issues to put fowared for discussions....tuna mambo ya maana kujadili si kafulia na wenzake.

  Mnyika asante sana kutuhabarisha na tunawatakia kheri katika mkutano wenu kamanda.

  Aluta...
   
 20. M

  Mchili JF-Expert Member

  #20
  Dec 3, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Too low
   
Loading...