CHADEMA yaishukia Ikulu...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yaishukia Ikulu...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Matola, Apr 23, 2012.

 1. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeishambulia Ofisi ya Rais Ikulu juu ya kauli yake kwamba Rais Jakaya Kikwete alikuwa hajakutana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kumjulisha kile kilichotokea bungeni wiki jana, kinadhihirisha ombwe kubwa la uongozi katika ofisi ya Rais na udhaifu wa kiuongozi wa Rais na serikali kwa ujumla.

  Taarifa ya CHADEMA iliyotolewa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika, ilisema kuwa Ikulu imeonyesha bayana kuwa Rais Kikwete ni mzito wa kuchukua hatua kwa kuwa masuala ambayo yamezuka bungeni anayafahamu kwa kuwa yamepitia kwenye Baraza la Mawaziri ambalo yeye analiongoza na pia yapo kwenye taarifa mbalimbali ambazo mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali amemkabidhi nakala kwa nyakati mbalimbali.

  Aidha CHADEMA imesema taarifa hiyo ya Ikulu imedhihirisha namna ambavyo safari za mara kwa mara za Rais zinavyolifanya taifa likose uongozi wake katika masuala ya msingi yanayoikabili nchi; hivyo ni muhimu asitishe safari ili kupunguza matumizi ya fedha wakati huu ambapo serikali ina ufisadi na matumizi makubwa hatua ambayo itamwezesha kubaki nchini kushughulikia masuala muhimu yanayolikabili taifa.

  Kwa upande mwingine, CHADEMA imesema taarifa hiyo ya Ikulu iliyokuwa ikikanusha habari zilizoandikwa na Tanzania Daima juzi, inadhihirisha kwamba hakuna mawasiliano ya karibu na ya mara kwa baina ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu Pinda wakati kwa mujibu wa ibara ya 52(3) na 53 (1) Waziri Mkuu ndiye msimamizi wa utekelezaji wa maagizo ya Rais anayewajibika kwa Rais.

  "Hali hii imekuwa ikijirudiarudia katika matukio kadhaa kwenye kipindi cha kati ya mwaka 2008 mpaka 2011; ikiwemo matukio ya kashfa ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, David Jairo.

  "Baraza hili la mawaziri kuendelea mpaka sasa kwa hali hii ni ishara ya udhaifu wa mamlaka ya uteuzi ambayo ni Rais Kikwete kwa kuwa ibara ya 57 (1) (c) ya Katiba imempa madaraka kufuta uteuzi na kuwaondoa madarakani mawaziri; hivyo Rais Kikwete athibitishe kwa matendo badala ya maneno matupu kuwa hawalindi mawaziri kwa kuwafukuza waliotajwa kwa kukiuka sheria," ilisema taarifa ya CHADEMA.

  Juzi Ikulu ilikanusha habari kuwa Rais alikuwa amewasiliana na Waziri Mkuu Pinda kuhusiana na suala la kujiuzulu kwa mawaziri, ikidai kuwa tangu awasili kutoka Brazil, Kikwete alikuwa hajakutana wala kuzungumzia suala hilo na waziri wake.


  CHANZO: Tanzania Daima
   
 2. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kikwete abaki nchini au asibaki hana impact yoyote kwa maendeleo ya nchi. Labda sema tu atapunguza matumizi ya hela ambazo zinatumika kwenye safari. Akibaki nchini atatuchelewesha tu kwenye shughuli zetu kutokana na kutusimamisha anapokwenda kusalimia misiba.
   
 3. LOWE89

  LOWE89 Senior Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kazi tunayo, hadi tutokemo mmh!! sijui
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Mnyika/ CHADEMA wanapiga chembe, right on the spot.

  Yaani Salva aliona anamtetea Kikwete kwa kusema Kikwete hajakutana na Pinda, kumbe ndio anazidisha kuonyesha upumbavu wa Ikulu.
   
 5. L

  Leonard Akaro JF Gold Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  JF kiboko hata silali..... Nabofya tuuuuu... Usingizi hauji
   
 6. rasmanyara

  rasmanyara Senior Member

  #6
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Watanzania 2badilike,2chague chama chenyekutetea watanzania wote nacho ni CDM
   
 7. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Jk dhaifu na uongoz wake dhaifu
   
 8. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sasa utakuwa ni mchezo wa Ikulu kujibu tuhuma kila siku toka Tanzania Daima maana ukiangalia inatisha na jamaa wanaspoti mapungufu wazi wazi na kumuweka JK uchi zaidi.
   
 9. JS

  JS JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  2015 mbaaali kweli lakini tutafika tu.....
   
 10. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  kifo chake kinaweza kuja kuwa cha ajali ya ndege!limbukeni wa ndege
   
 11. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,683
  Likes Received: 638
  Trophy Points: 280
  Kwani ilitakiwa akutane nae lini?
  Mambo mengine ni ushabiki tu!
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Umeisoma ile communique ya Kurugenzi ya habari ya Ikulu?

  Kwamba rais hakukutana wala kuwa na mawasiliano yoyote na PM ni sawa na baba mwenye nyumba kusikia nyumba inawaka moto halafu asijali hata kupiga simu nyumbani kuona hali ikoje.

  Kama hili ni ushabiki tu, na wewe kwa kuliongelea unaleta ushabiki tu.

  Nuff said.
   
 13. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Sio wewe, tupo wengi. hapa pembeni mama watoto kanuna usipime teh teh teh!
   
 14. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hujui kinachozungumzwa hapo umekurupuka. soma posts za wenzio vizuri. mashavu yako!
   
 15. O

  Original JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani kukaa kimya ni hekima. Jakaya hana la kusema hivyo anaona ni hekima kukaa kimya. Asije kuongea vitu vya ajabu mkaanza tena kumsema vibaya mtoto wa Kikwere.
   
 16. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,683
  Likes Received: 638
  Trophy Points: 280
  Tatizo lenu mnakurupuka!!
  JK kutuletea mawaziri wazembe ni kosa ambalo yeye inatakiwa awajibishwe. Lakini siyo kila kinachozungumzwa leo basi rais anapewa taarifa. Rais hapewi taarifa kwa kunong'onezana, bali kwa ripoti ya maandishi, na akipata hiyo ripoti ya kikao ndipo huzungumza na waziri. Kabla ya hapo, ni maneno tu ambayo gazeti la CDM sijui liliyapata wapi.
  Yaani wamesema rais kamwambia waziri mkuu "huu ni upepo tu!". Hayo maneno kayasema lini?
  Na hapo ndipo unapoona kurugenzi ya uenezi CDM inavyojaribu kuikingia kifua taasisi nyingine.... Tanzania Daima.
  Cheap freakin' politics. What a waste!!!
   
 17. Endangered

  Endangered JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 929
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  It's amazing how you still got the energy to say that. As if you are one of Ikulu workers, keep it up, only to find out sometimes later that you were wasting your time!
   
 18. Mama Yeyoo

  Mama Yeyoo Senior Member

  #18
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 25, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hahaaaa!!!i can imagine...!!!kweli hii Jf inanifanya niwe teja lake kuubwa...duh,macho yanataka kulala lakini vidole vimegoma kuacha kubofya....mweeehh
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,708
  Trophy Points: 280


  ....Naam tutafika JS lakini na nchi nayo itakuwa hoi bin taabani maana speed ya ukwapuaji wa pesa za walipa kodi itaongezeka kwa kasi ya kutisha kwa wizi au mikataba ambayo haina maslahi na nchi maana wanajua pale Ikulu kuna msanii kazi yake ni kukenuakenua tu hata siku moja hawezi kufanya maamuzi mazito ili kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania.
   
 20. s

  sirghanam JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  unaweza ukadhani unamtetea kumbe unamuangamiza
   
Loading...