CHADEMA yaishika pabaya CCM Kinondoni

Dieufem

Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
7
Reaction score
6
Habari Taifa stars, CHADEMA imeishika pabaya CCM kupitia operetion yake safisha Kinondoni baada ya mkutano mkuu wa jimbo, mbele ya katibu mkuu ndg Dr. Slaa kuuondoa uongozi wa awali na k uweka kikosi cha mauaji kwa CCM.

Viva CHADEMA, Viva M4C
 
Jimbo la Kinondoni ni weak point kwa CCM, hivyo 2015, Chadema inayo nafasi kulitwaa kiulani!. Ilala bado ni ngome ya CCM, Temeke na Kigamboni CUF ikijiimarisha inayakomba. Kawe ni hatihati linaweza kurejeshwa CCM. Ubungo kwa Mnyika ni ngome imara ya Chadema, Ukonga pia inaweza kuchukuliwa kiulaini!.

Tatizo la ndugu Chadema ni dogo tuu "kujipanga!".
Pasco.
 

Kwa hapa mkuu Pasco nitakuunga mkono,ila kwa Jimbo la Kawe bado Halima Mdee ana nguvu kubwa.
 
Last edited by a moderator:
Kigamboni ni kweli maana kuna wapemba wa kumwaga huku na kwa vyovyote cuf ikijipanga vzr inapachukua
 
Chadema imeishika vipi pabaya ccm? hebu fafanua na toa habari kamili, wote hatupo kinondoni hadi tukuelewe kwa sentensi yako moja
 
Kwa hapa mkuu Pasco nitakuunga mkono,ila kwa Jimbo la Kawe bado Halima Mdee ana nguvu kubwa.

Mkuu Molemo,
Taarifa za chini chini zimeshaanza kuenea kuwa mnataka kulitoa Kawe sadaka kama mlivyolitoa sadaka Tarime kwa kumuengua Charles Mwera?!.

Sio siri, hata wale posible candidates wanaounga mkono upinzani, hawathubutu kabisa kuliwazia jimbo la Kawe kwa sababu, Halima Mdee ni kama Komandoo!, hata kitendo cha Mbatia kutia pua was a mistake na aliijutia. Nilimshauri Dr, kwa ajili ya 2015, msisubiri kipenga cha NEC, anzeni ground work mapema ya head hunting posible serious candidates hata ikibidi ku groom, fanyeni grooming!. Muhakikishe mnaanza na uchaguzi wa serikali za mitaa 2014, simamisheni mtu kila kiti!. Kuna sehemu CCM imechokwa mpaka basi kiasi kwamba hata mkisimamisha jiwe litapita!.

Ila uchaguzi wa 2015 utakuwa mgumu kidogo kwa upande wenu, wenzenu CCM watasimama na track record ya visible developments wakati nyinyi mtasimama na ahadi za tumaini jipya!. Ahadi hizo lazima ziwe solid with justification: mfano mkisema Elimu bure mpaka chuo kikuu, mnakuja na data how much does it cost, na indication budget hiyo itotoka wapi au mpunguza matumizi gani that will save this much tutakayo itumia kwenye elimu bure etc!.

Merry X-mass
Pasco.
 

Mzee wa vibahasha siku hizi umeanza kuongea point, au Eddo amekutoa kwenya payroll yake?
 

Ubungo sawa lakini jimbo la Kinondoni bado
 
Mzee wa vibahasha siku hizi umeanza kuongea point, au Eddo amekutoa kwenya payroll yake?
Kwenye payroll bado nipo na vibahasha kama kawa, ila pia nimeishaijua jf, mtu ataongea point pale tuu anapoisifia Chadema!, akiikosoa inakuwa ni pumba, katumwa, gamba etc!.
Merry X-mass
Pasco.
 

Point taken Mkuu Pasco.Nikuhakikishie tena na naomba niamini kwamba Halima Mdee ni chuma cha Pua na Chadema kamwe haitathubutu kufanya majaribio Kawe.Ingawa kwa kusema hivi hatukumbatii udikteta wala kuwaogopesha wanachama wengine.Lakini ukweli ni lazima usemwe kwamba Halima Mdee ni kete ya Chadema Kawe kama Dr Slaa alivyo kete ya Chadema kwenye urais 2015.
 
Last edited by a moderator:
Ubungo sawa lakini jimbo la Kinondoni bado
Kinondoni, mbona Azan anamsukuma kama unasukuma mlevi!. Hata mimi ningekuwa Chadema nikasimama Kinondoni, CCM Chali!.
Merry X-mass
Pasco.
 
Kwenye payroll bado nipo na vibahasha kama kawa, ila pia nimeishaijua jf, mtu ataongea point pale tuu anapoisifia Chadema!, akiikosoa inakuwa ni pumba, katumwa, gamba etc!.
Merry X-mass
Pasco.
sio jf tu hata mtaani ni hivi hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…