CHADEMA yaisadia CCM kuvua GAMBA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yaisadia CCM kuvua GAMBA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohamedi Mtoi, May 6, 2012.

 1. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #1
  May 6, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Chama makini ambacho kwa sasa ndicho pekee kilicho beba matumaini ya watanzania kimedhihirisha kuwa ndio chama pekee kinacho weza kuvunja majabali ya vikwazo na mikwamo inayo wakabili watanzania. Hapa tukumbuke kuwa watanzania wanapambana na vikwazo na mikwamo iliyo sababishwa na maadui 4 ukiachilia mbali wale maadui 3 walio zoeleka miaka nenda miaka rudi, (ujinga, umasikini na maradhi) ameongezeka adui namba 4. Na kwenye vita ya kuwaondoa maadui hao, adui namba 4 akiondolewa itakuwa sawa na nchi kupata uhuru mpya kutoka mikononi kwa mkoloni mweusi, adui huyo anaitwa MAGAMBA. Nitaeleza.

  Ndani ya chama cha mapinduzi kumekuwa na kauli mbiu sarakasi na falsafa ambazo zimefaulu kushindwa kwa viwango vya kimataifa, kumbuka falsafa na kauli mbiu za siasa ya ujamaa na kujitegemea, kilimo ni kazi, kilimo cha kufa na kupona, maralia haikubaliki, kilimo kwanza, ari mpya, nguvu mpya, kasi mpya, kumbuka ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi. Usikumbuke maana bado hujasahau ile kauli ulimbo ya juzijuzi, Tu'methubutu, Tu'meweza na Tu'nasonga mbele kumbe walikuwa wanathubutu wao, kuweza wao na kusonga mbele wao kutuibia raslimali zetu na kujaza matumbo yao.

  Hizi sarakasi, ita falsafa au kauli mbiu zote hazina ushahidi wa kufaulu kubadilisha hali za watanzania. Watanzania bado wamepigika na hawana tena matumaini kwa serikali ya ccm kama waliyokuwa nayo enzi za Mwl na sasa matumaini yao yako mikononi mwa chama makini chenye m-busi mkubwa unaosubiri usajili wa plate namba T2015CDM.

  Kwa sasa ccm wote ni magamba! Nape amekuwa anatuambia wanaotoka ccm wamepoteza mvuto na wanavua gamba, kwa maana hiyo, ki mantiki anae baki ndani ya ccm ni GAMBA. Lakini simple logic, unaweza kukosa mvuto ndani ya gamba na ukaupata nje ya Gamba kwa kuvaa gwanda.

  Chadema imeamua kufungua milango kwa kuanzisha harakati za mabadiliko kwa kuwahimiza, kuwapokea, kuwashauri na kuwasihi wanachama walioko ndani ya gamba (ccm) ambao wana nia ya dhati ya kuipigania nchi yao kuvua gamba na kuvaa magwanda na kuungana na makanda kuhakikisha kuwa magamba haya ikamati dola mwaka 2015.

  Chadema kinawasaidia wana ccm (magamba) kulivua gamba, (hii imewashinda ccm wenyewe) wanapo vua gamba wana tawazwa na kupewa mavazi rasmi yaitwayo Magwanda ili kuingia rasmi kwenye mapambano ya kuirejesha Tanzania ya maziwa na asali pamoja na raslimali zake mikononi mwa Watanzania.

  VUA GAMBA, VAA GWANDA. Mwanangu nae ananiambia wajomba zake kule pwani wavue kanzu wavae magwanda lakini wabaki na imani zao.
   
 2. M

  Makupa JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  kuanzia sasa wale wana ccm wote wanaojiunga cdm wanastahili kuitwa gwanda gamba a.k.a gama
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Vua gamba


  Vaa GWANDA FLUU!


  Tuna hasara sana na hii serikali tawala lakini mwisho wao waja hakika.
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Tatizo lenu hamna ubunifu, mnangoja jitihada za wabunifu kuzzifanya ndio hoja zenu. Hamfiki mbali kwa hayo.
   
 5. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sikio la kufa....., watasema ni upepo tuu, utapita. na tuone kama ni upepo ama ni kimbunga, dhoruba ama sunami??
   
 6. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe na brain coccussiion ni pete na kidole
   
 7. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Like !!! Like!! Like!!!!
   
 8. M

  MTENGE Member

  #8
  May 6, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wamethubutu Kutuibia, wakaweza wakasongambele, maadamu hakuna kikimbiacho kisichosimama sasa ndio muda wao wakuondoka na kurejeshe mali ya watanganyika
   
Loading...