Leta ushahidi halisi! kwa maswali ya haraka haraka! Kwanini unafikiri kwamba chadema wamegeza ODM na sio ODM kugeza chedema? Nikisoma taafira yako naona imeandikwa Monday, October 08, 2007, nilipoangalia mtandao nagundua Bwana mbowe aliongelea majimbo policy 2005-10-17.
Mbowe defends 'majimbo' policy
Inawezekana kabisa mtandao unanidanganya, kwahiyo wewe nipe huo ushahidi wako wa word to word, pia nipatia tarehe za maandiko hayo. Halafu ndio tufuate swala la hoja yako ya madhara ya kuigilizia!
Ushahidi
Soma maelezo haya ya ODM:
MAJIMBO POLICY IN KENYA (FEDERALISM IN KENYA)
Sera ya majimbo' ni siri ya maisha bora kwa kila Mkenya
Monday, October 08, 2007
Daniel Ochieng' Obunga (Kitengela, Nairobi)
danobunga at yahoo dot com – 0725-408720
Sera hii ya majimbo ni swala nyeti sana wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka huu 2007 kwa vijembe vya majukwaani.
Hoja kuu ya kufahamu ni kwamba chimbuko la sera ya majimbo nchini ni falsafa ya ODM ya nguvu ya umma, shirikisho pia iliunga mkono sera hii.
Kwani umma ndio unapaswa kuwa na mamlaka lakini pia umma ndio unapaswa kunufaika na rasilimali za nchi.
Majimbo ni moja kati ya sera za chama cha ODM nchini Kenya ambacho kitapewa kipaumbele.
Jinsi vigogo vya chama walivyo ongea siku ya jumamosi Uhuru park Kuzindua kampeni ya Urais Mheshimiwa Raila Odinga, waligusia zera muhimu ni ya Majimbo, na mheshimiwa Wiliam Ruto Pia aliongelea hapo awali kinaganaga kwenya radio kuhusu sera ya majimbo.
Wananchi wanataka mfumo mpya wa utawala. ODM waliongelea masuala matatu, kwanza, uongozi mpya kwa maana ya wananchi kuwaondoa viongozi walioko madarakani kwa maana wameshiriki ufisadi wa nyuma, hivyo hawawezi kufanya mabadiliko yoyote ya maana.
Pili; kusafisha mfumo wa utawala kwa maana ya kupambana na rushwa na ufisadi, na tatu, kutengeneza muundo mpya wa utawala ikiwamo kuanzisha muundo wa majimbo.
Lakini kwa kuwa suala la majimbo lilipata ladha zaidi na mashambulizi mengi yanatoka kwa wapinzani wetu, wakenya wengechagua chama cha ODM ili sera hii ya majimbo lipewewe jaribio katika taifa letu pia,
Suala la sera ya majimbo ni suala la kikatiba. Chama chochote cha siasa kinauza kwa wananchi matakwa yake kama kikipewa ridhaa na wananchi.
Matakwa hayo yanaweza kutokana na misingi ya chama husika ama matakwa ya wananchi ama matakwa ya viongozi wa chama husika.
suala la kuundwa kwa majimbo ni suala la mabadiliko ya katiba hivyo kwa vyovyote vile ODM itabadilisha katiba kwa haraka sana wakati watakapochukua utawal mwacka ujao.
Maelezo yanaendelea ukibonyeza hapa:
MAJIMBO POLICY IN KENYA (FEDERALISM IN KENYA) , Dan Ochieng' Obunga
Halafu Soma maelezo haya ya CHADEMA:
14 Machi 2007
'Sera ya majimbo' ni siri ya maisha bora kwa kila Mtanzania
na John Mnyika
HIVI karibuni pameanza kujitokeza tena mjadala kuhusu ‘majimbo' na masuala kadhaa yameibuliwa.
Huu ni wakati mwafaka nami nichangie hoja kadhaa katika mjadala huu muhimu.
Nikumbushe tu kwamba mjadala huu ulishika kasi sana wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2005 kwa vijembe vya majukwaani.
Hoja kuu ya kufahamu ni kwamba chimbuko la sera ya majimbo nchini ni falsafa ya CHADEMA ya nguvu ya umma.
Kwani umma ndio unapaswa kuwa na mamlaka lakini pia umma ndio unapaswa kunufaika na rasilimali za nchi.
Niweke pia bayana kwamba katika uchaguzi CHADEMA haikuwa na ajenda ya majimbo kama ajenda inayosimama peke yake. Ilikuwa ni sehemu ya ajenda nyingine.
Tulisema wazi kwamba tatizo la CCM ni kwamba huwa inakuja na ilani ya kuahidi kila kitu na hatimaye kutofanya chochote.
Sisi tulisema pamoja na kuwa na sera nyingi lakini tutakuwa na vipaumbele vitano tu:
Mosi, mfumo mpya wa utawala, pili; elimu, tatu, kilimo, nne, uchumi, tano, afya. Na hata katika vipaumbele hivi bado tulichagua maeneo machache mahususi.
Mathalani katika uchumi tulilenga kodi (kupunguza ukubwa wa kodi na kuhakikisha kuwa kodi zinakusanywa ipasavyo).
Ajira na rasilimali hususan madini katika mfumo mpya wa utawala.
Hapa tulikuwa na masuala matatu, kwanza, uongozi mpya kwa maana ya wananchi kuwaondoa viongozi walioko madarakani kwa maana wameshiriki ufisadi wa nyuma, hivyo hawawezi kufanya mabadiliko yoyote ya maana.
Pili; kusafisha mfumo wa utawala kwa maana ya kupambana na rushwa na ufisadi, na tatu, kutengeneza muundo mpya wa utawala ikiwamo kuanzisha muundo wa majimbo.
Lakini kwa kuwa suala la majimbo lilipata ladha zaidi na mashambulizi mengi; sera, ajenda, maana ya mfumo mpya wa utawala ikafunikwa kabisa.
Sina nia ya kujadili katika makala ya leo kwa nini hali hii ilijitokeza.
Kwa kuwa wengi wamezoea kutumia jina ‘Sera ya majimbo' nami katika mjadala huu nitatumia jina hili ili twende pamoja.
Suala la sera ya majimbo ni suala la kikatiba. Chama chochote cha siasa kinauza kwa wananchi matakwa yake kama kikipewa ridhaa na wananchi.
Matakwa hayo yanaweza kutokana na misingi ya chama husika ama matakwa ya wananchi ama matakwa ya viongozi wa chama husika.
Lakini baada ya uchaguzi zipo sera ambazo utekelezaji wake lazima urudi tena kwa wananchi kupata ridhaa ya pamoja, mathalani CCM wamejikuta suala la mahakama ya kadhi linapaswa kurudi kwa wananchi, ingawa liko katika ilani ya chama chao.
Lakini mambo mengi ya chama hutekelezwa kwa kwenda kwa wawakilishi wa wananchi yaani Bunge.
Kadhalika, suala la kuundwa kwa majimbo ni suala la mabadiliko ya katiba hivyo kwa vyovyote vile CHADEMA ingepaswa kurudi kwa wananchi.
Maelezo hayo yanaendelea ukibonyeza hapa:
http://www.chadema.net/makala/mnyika/mnyika_18.html
HUONI KWAMBA MAELEZO YAO YANAFANANA? Sasa unadhani kati ya Mbowe na Raila Odinga nani ni mkongwe katika siasa? Nani ameanza kuzungumzia majimbo? ndio maana nasema CHADEMA wameiga toka ODM
.....ndiyohiyo