CHADEMA yafutika kwenye ramani ya Serengeti

CHADEMA yafutika kwenye ramani ya Serengeti

Nyamtalakyono

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2015
Posts
795
Reaction score
479
Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) kimefutika kabisa kwenye Ramani ya Wilaya ya Serengeti baada ya Mbunge na madiwani takribani saba akiwemo Mwenyekiti wao wa Halmashauri kuhamia CCM.

Hata hivyo licha ya viongozi hao pia kumeripotiwa maeneo mbalimbali wenyeviti wa vijiji kupitia Chadema hapa Serengeti wameendelea kukihama chama chao na kutimkia CCM.

Nawapongeza sana.Mwisho naawabia viongozi wa Tarime mliochaguliwa kupitia Chadema njooni nyumbani kumenoga. Viva Serengeti.
 
Si kuna uzi umewashauri wote wajiunge, sababu ndio hizo hizo.

nataka kuwasaidia makamanda kujua tatizo liko wapi ili wa retain members wake...mpaka sasa sijui tatizo ni nini,kama ni kuunga juhudi za Rais mbona wananchi wanamuunga not necessarily kujiunga na chama chake ndio uunge jitihada zake..this makes me think may be kuna deeper issues ambazo bado hazijawa identified within CHADEMA..ambazo zinakimbiza wanachama wake...
 
kuna jimbo moja dodoma toka limeanzishwa linaongozwa na ccm, lakini wanafunzi wake wanasomea nje. Je huko dodoma kwenyewe hakujanoga

WANAFUNZI WASOMEA KWENYE VIBANDA VYA NYASI DODOMA: Tanzania leo imeadhimisha Siku ya Walimu Duniani ambapo moja ya changamoto wanayokumbana nayo walimu nchini ni mazingira magumu ya kufundisha na kufundishia ikiwemo uhaba wa madarasa kama ambavyo unaikabili shule ya msingi Misrey iliyopo wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Hali hiyo inawafanya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo kulazimika kusomea katika vibanda vya nyasi huku wengi wao wakikaa chini kwenye vumbi kwa kukosa madawati.

#SikuYaWalimu #AzamNews #AzamTVApp #AzamTVHabari #AzamTV
 
nataka kuwasaidia makamanda kujua tatizo liko wapi ili wa retain members wake...mpaka sasa sijui tatizo ni nini,kama ni kuunga juhudi za Rais mbona wananchi wanamuunga not necessarily kujiunga na chama chake ndio uunge jitihada zake..this makes me think may be kuna deeper issues ambazo bado hazijawa identified within CHADEMA..ambazo zinakimbiza wanachama wake...
Kuna nini zaidi ya rushwa na hongo ya vyeo?Ukweli mnaujua na ndio maana mnatumia dola kushinda uchaguzi.
 
Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) kimefutika kabisa kwenye Ramani ya Wilaya ya Serengeti baada ya Mbunge na madiwani takribani saba akiwemo Mwenyekiti wao wa Halmashauri kuhamia CCM. Hata hivyo licha ya viongozi hao pia kumeripotiwa maeneo mbalimbali wenyeviti wa vijiji kupitia Chadema hapa Serengeti wameendelea kukihama chama chao na kutimkia CCM. Nawapongeza sana.Mwisho naawabia viongozi wa Tarime mliochaguliwa kupitia Chadema njooni nyumbani kumenoga. Viva Serengeti.
So wananchi tutegemee maendeleo kama ya ulaya? Hongereni kwa kuing'oa CDM ...
 
Ningestuka kama wapiga kura wote wangehamia ccm, waweke uchaguzi huru akishinda mgombea wa ccm ndo nitajua kumenoga
 
kuna jimbo moja dodoma toka limeanzishwa linaongozwa na ccm, lakini wanafunzi wake wanasomea nje. Je huko dodoma kwenyewe hakujanoga
Halafu kuna wajinga wanaona fahari kuhamia huko.
 
Kuna nini zaidi ya rushwa na hongo ya vyeo?Ukweli mnaujua na ndio maana mnatumia dola kushinda uchaguzi.
Hivi Chadema hamna fedha za kuwahonga viongozi wa CCM? Yaani mmeshindwa kuwahonga hata wenyeviti wa vitongoji wa CCM?
 
Kuna nini zaidi ya rushwa na hongo ya vyeo?Ukweli mnaujua na ndio maana mnatumia dola kushinda uchaguzi.
Kijana siasa unazopiga zimepitwa na wakati.
Unachotakiwa ni kuweka sera za chama chako. Hayo unayoyaandika hata mtoto mdogo anaweza kuandika.
Siasa ni kueleza itikadi na sera ya chama chako. Lakini hizi siasa za kuchafua watu, mmejaribu lakini mwisho wa siku mmegeuka ninyi kwa ninyi kuramba matapishi tenu.

Niambie ile issue ya kumchafua Lowassa kuanzia 2008 - 2015 iliishia wapi!?

Siasa unazopiga zimepitwa na wakati. You need to update yourself.
 
Imechelewa sana kufutika,acha Mbowe ale ruzuku na ukoo wake
 
Back
Top Bottom