CHADEMA yafutika Kigoma

CHADEMA yafutika Kigoma

Act haina mpango wa kugombana na chama chochote bana. Nyie cdm ndio mna chuki ya kike kuona chama kingine kipya kwani kwa ujinga wenu mnadhani nyie ndio wenye kura ya turufu ya kuwa wapinzani. Act ni wazalendo kama unatambua maana ya wazalendo na wewe unajiamini ni miongoni mwa wazalendo basi jiunge sasa usipoteze muda

Nikiingiaga huku jf ndio nakutana na hichi kisakosi lakini mtaani ukimuuliza act ni nini? huenda akakujibu ni sumu ya mende.
 
WanaCHADEMA watabaki, walioondoka ni wanaZITTO na waliokuwa na kadi za chama kiitwacho ZITTO ambacho hakijasajiliwa kwenye ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa!!!!
 
hivi act vision yenu ni ipi? Mission yenu nini?


Nyie kama chama cha siasa malengo yenu makuu n yapi?


Kushindana na ccm? Kushindana na cdm? Au kushindana na vyote kwa pamoja??
hiki ni chama pinzani cha upinzani
 
ukiondoa kigoma mjini na baadhi ya maeneo machache sana ya mkoa wa kigoma,act inafahamika zaidi kwenye mitandao ya kijamii.yaani mikoa mingine hata hawajui act ni mdudu gani tanzania.

usije ukajiharishia kwa woga wa kuigopa act
 
Na hii ni dhahiri na thabiti kabisa
adui mkubwa wa Zitto na ACT yake ni CCM hawatakuwa tayari kuona Zitto anachomoza tena na huu ndio mwisho wake.

Zitto hawezi kuishi unavyotaka wewe maana we mwenyewe ni mbulula
 
Hivi ikitokea Zito akashindwa uchaguzi huko Kigoma mjini mtasemaje?

Ina maana mkoa mzima msomi wa kiwango cha Zitto ni yeye tu?
 
Mmeishiwa sera, cuf nao mliwaambia hivyo hivyo ccm b, Leo mpo pamoja tuwaelewe vipi?

Mpwa mimi sio mwanachama wa chama chochote KTY,Chama chochote kinakuwa na itikadi,mlengo na malengo makuu ambavyo vinapambanua chama kimoja na kingine.nilichofanya ni kulinganisha itikadi na malengo ACT na CCM, naona kama vinafanana,sasa wewe mwanachama unieleze tofauti ili nielewe tu,hayo ya CUF na yaliyotokea waachie wenyewe.Angalizo; siyo wote wanaochangia ni partisans,sisi wengine tuko kwenye utaifa zaidi.
 
Mbowe Kamtapeli Nani??, Angalia Ndani ya CCM Utawakuta Matapeli wa Kimataifa bro...

kawatapeli wengi ukiwemo wewe. Kabadili katiba abakie kwenye uenyekiti, kaweka sheria za kidikteta kwenye katiba ya chadema, kawauzia mafuso mabovu na maspika mabovu, kajipa tenda ya kuagiza pikipiki za chama toka Japan bila kutembeza quotation wa zabuni!
 
kwa hili ndugu umepotea kigoma ya sasa haichagui chama wala m2 2taangalia amefanya nn na ata2fanyia nn maswala ya ushabiki wa vijiwe vya kahawa hakuna yalishapitwa na wakati.
 
Waha kwa muha mwenzao. Zitto ni mashine lakini Shida yake kubwa anajiona yeye ndio yeye. Bila yeye hakuna chama. Asipo jirekebisha mwisho wake ni ubunge tu
 
Tatizo la Chadema wanajiona wao ndio wana monopoly ya upinzani wengine wote ni wafuata upepo au wasaliti.
 
Baada ya aliyekuwa mbunge wa kigoma kaskazini kwa tiketi ya chadema zitto kabwe kuondoka ndani ya chama hicho sasa ni dhahiri shahiri kuwa chama hicho kimepotea rasmi ndani ya mkoa wa kigoma,
Hali hiyo inatokana na kundi kubwa la vijana waliokuwa wanakiunga mkono chama hicho kuamua kumwaga manyanga na kujiunga na chama cha ACT na baadhi kuamua kurudi CCM,huku wakisema wamechoka kuwatumikia wachaga,.
Aidha ni dhahiri kuwa jimbo la kigoma kaskazini sasa limeisha toka mikononi mwa chadema,iwapo mgombea anayetaka nafasi hiyo bwana yered fubusa atapitishwa na chama Hicho kupeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu ujao,
jimbo hilo la kigoma kaskazini limeonekana kukamiwa sana na chama cha mapinduzi,huku makada wake maarufu hamisi betese,robinson lembo,paschal mahwago,peter serukamba wakiliwinda kwa udi na uvumba huku nyota anga'avu ikionekana kumwangukia peter serukamba,

1. ACT ni chama cha Kigoma???

2. Serukamba ni CCM au ACT

Siasa ina kazi...
 
Ukinukuu gazeti unatakiwa uweke wazi ni Gazeti Namba ngapi, na la tarehe ngapi. Kinyume na hivyo ni habari ya kutunga.

Wewe nadhani ni mmoja wao kati ya wale misukule wa CDM wanaofuata upepo na kuamini kila wanachoambiwa na Mbowe bila kuhoji? Hiyo habari ya Mbowe kupewa hlela na Mkono wewe ndio leo unaisikia? Mbona hata hapa JF imeongelewa sana?
 
Wewe nadhani ni mmoja wao kati ya wale misukule wa CDM wanaofuata upepo na kuamini kila wanachoambiwa na Mbowe bila kuhoji? Hiyo habari ya Mbowe kupewa hlela na Mkono wewe ndio leo unaisikia? Mbona hata hapa JF imeongelewa sana?

Mara nyingi watu ambao hawana hoja ndio wanaotumia lugha chafu kama unayotumia!

Mimi nazungumzia habari ya quotation ya gazeti, badala ya kujibu unaropoka Mbowe!! Huna lingine la kuongelea zaidi ya Mbowe?!

Siyo lazima mtu aone kila habari inayoongelewa JF. Kama unaona ni muhimu kunielewesha ungeweka Link!
 
kawatapeli wengi ukiwemo wewe. Kabadili katiba abakie kwenye uenyekiti, kaweka sheria za kidikteta kwenye katiba ya chadema, kawauzia mafuso mabovu na maspika mabovu, kajipa tenda ya kuagiza pikipiki za chama toka Japan bila kutembeza quotation wa zabuni!

utakuwa umevurugwa wewe, kasome katiba ya cdm ujue in kina nani wenye mamlaka ya kutunga katiba.ulivyo Mpuuzi unadhani no wajibu was mwenyekiti
 
Back
Top Bottom