CHADEMA yafunika Mang'ula kwa mkutano wa kihistoria

Joined
Dec 11, 2010
Posts
3,321
Reaction score
6,331
Leo mwenyekiti Taifa amefanya mikutano mitano kwenye majimbo matatu ya Ulanga Magharibi, Ulanga Mashariki na Kilombero.

Mikutano yote ilikuwa mikubwa sana na yenye hamasa kubwa huku wenyeviti saba wa CCM wa vijiji kwenye jimbo la Ulanga Mashariki wakirudisha kadi za CCM na kujiunga na CHADEMA na kuahidi kuongeza nguvu zaidi kwenye Operation Delete CCM ambapo watasaidia wagombea watakao simamishwa na Chadema pamoja na vyama vingine vya UKAWA.

Kesho itafanyika mikutano minne ambapo mkutano wa mwisho utafanyika jimbo la Morogoro mjini na kuhitimisha ziara ya mwenyekiti wa chama Taifa (Mh Mbowe); baada ya mwenyekiti Taifa kuhitinisha ziara mkoa wa Morogoro, katibu mkuu wa chama (Dr slaa) atampokea kijiti na kuendeleza ziara ya kanda ya kati kwenye mikoa ya Dodoma na Singida.

Ziara za chama ndio zimeanza rasmi na zitakuwa endelevu bila kukoma mpaka 2015.
 
Attachments

  • 1416077379537.jpg
    1416077379537.jpg
    120.9 KB · Views: 3,271
  • 1416077467461.jpg
    1416077467461.jpg
    152.2 KB · Views: 2,636
  • 1416077560605.jpg
    1416077560605.jpg
    144.3 KB · Views: 2,024
  • 1416077672076.jpg
    1416077672076.jpg
    138.3 KB · Views: 2,818
  • 1416077818536.jpg
    1416077818536.jpg
    146.4 KB · Views: 2,555
Hata Kalenga mlifanya "mikutano ya kihistoria" kisha mkaangukia pua.

Kinana anaanza ziara ya siku 16, mtaipata fresh!
 
Vipi kwa maoni yako ni mgombea gani wa CCM atakiweza kimbunga cha Dr Slaa kwenye uchaguzi mkuu 2015?
 
Kinana mtoto Mdogo tu Hongera. Chadema kwa kutafuta Uhuru wakoloni weusi wamezidi kututafuna tumechoka
 
Vipi kwa maoni yako ni mgombea gani wa CCM atakiweza kimbunga cha Dr Slaa kwenye uchaguzi mkuu 2015?

Mzee Slaa zama zake zilishapita, labda akagombee ubunge tena.

Hujasikia ya TWAWEZA juzi?

au hukumbuki maneno ya kamanda mwezio? Msome hapo chini!

quote_icon.png
By Yericko Nyerere

Ukija kwenye upinzani kati ya wagombea wote vinara wa UKAWA bado mgombea mwenye nafuu ni Dr Slaa tu, Pamoja na kuporomoka kwa Slaa kutoka 2010 hadi 2015 bado ndio mtu sahihi ukilinganisha na Mh Mbowe au Mbatia au Lipumba kwasababu mbalimbali ambapo nitazichambua nipatapo wasaa,

Kwa upande wa cdm, Slaa angegombea uenyekiti na John Mnyika akawa katibu mkuu, Mbowe awe mwenyekiti bodi ya wadhamini. Itamsaidia Slaa kupumzika.
 
Leo mwenyekiti Taifa amefanya mikutano mitano kwenye majimbo matatu ya Ulanga Magharibi, Ulanga Mashariki na Kilombero.

Mikutano yote ilikuwa mikubwa sana na yenye hamasa kubwa huku wenyeviti saba wa CCM wa vijiji kwenye jimbo la Ulanga Mashariki wakirudisha kadi za CCM na kujiunga na CHADEMA na kuahidi kuongeza nguvu zaidi kwenye Operation Delete CCM ambapo watasaidia wagombea watakao simamishwa na Chadema pamoja na vyama vingine vya UKAWA.

Kesho itafanyika mikutano minne ambapo mkutano wa mwisho utafanyika jimbo la Morogoro mjini na kuhitimisha ziara ya mwenyekiti wa chama Taifa (Mh Mbowe); baada ya mwenyekiti Taifa kuhitinisha ziara mkoa wa Morogoro, katibu mkuu wa chama (Dr slaa) atampokea kijiti na kuendeleza ziara ya kanda ya kati kwenye mikoa ya Dodoma na Singida.

Ziara za chama ndio zimeanza rasmi na zitakuwa endelevu bila kukoma mpaka 2015.

werawera, ama zao ama za chadema/ ukawa. Kusema ukweli inatia hamasa sana, mungu ibariki chadema mungu ibariki ukawa
 
Huyo Kinana ndio tuna mtaka ajipime ubavu kama atakuwa na uwezo wa kupambana na Dr Slaa.

Lakini pia itakuwa faraja kwa tembo wetu maana atakuwa busy na kazi za chama.
Mzee Slaa na Kinana ni kama kichuguu na Mlima KILIMANJARO,

Afisa wa chama kama wewe kuanza propaganda za kitoto kama hizo(highlighted) inaonyesha ni jinsi gani chama chenu kilivyokosa hazina ya viongozi.
 
Chadema kwa nini msijenge chama kuanzia ngazi ya shina na matawi mjini na vijijini? Hiyo mikutano ya Mbowe haina tija yoyote kwa Chama. Viongozi walioko mikoani wanalia njaa ruzuku haifiki Mbowe anatanua tu na Chopa. Ni matumizi mabaya ya ruzuku.
 
Unapenda kujenga majengo au kujenga Ubongo utakao jenga majengo?!
 
Back
Top Bottom