CHADEMA yachangiwa mamilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yachangiwa mamilioni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JOB SEEKER, Mar 25, 2012.

 1. JOB SEEKER

  JOB SEEKER Senior Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Juzi usiku CHADEMA ilizindua kampeni ya ‘Vuguvugu la Mabadiliko’ ambapo wapenzi wa harakati za mabadiliko nchini walikichangia chama hicho sh milioni 150.
  Viongozi wa CHADEMA akiwamo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, walisema kupitia ‘Vuguvugu la Mabadiliko’, chama hicho kinakwenda kuanzisha elimu ya uraia na elimu ya Katiba mpya nchi nzima.
  Walisema CHADEMA inataka kupigania mabadiliko ya kweli ya kuondoa utawala mbovu miaka 50 baada ya uhuru, hasa kwa kupiga vita ufisadi na kudai uwajibikaji wa viongozi kwa maendeleo ya watu.
  Viongozi hao walisema mkakati wa chama hicho ni kukiweka mikononi mwa wananchi wa kila kada, ambapo kila Mtanzania mwenye machungu na nchi yake ataweza kuchangia fedha ili kukisaidia chama hicho kuchukua dola kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
  Mbowe alisema mabadiliko ya kweli nchini yatafanikiwa kwa Watanzania waadilifu kuunganisha nguvu zao dhidi ya ufisadi wa watawala walioko madarakani, chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
  Aliwaambia mamia ya marafiki wa CHADEMA waliokusanyika katika Hoteli ya Naura Springs kwa ajili ya uzinduzi huo kuwa chama hicho hakitakuwa na masihara katika kulinda na kupigania haki na utu wa Mtanzania katika kulinda rasilimali za taifa ili zitumike kwa masilahi ya watu wote.
  “Leo tunakwenda kujenga historia mpya, tena ya kufanya siasa za uwazi na ukweli, tunataka chama hiki kwa vitendo kabisa kiwe chama cha watu, kitakachosimamiwa na watu, kitachangiwa na watu na kitaongozwa na viongozi wanaotokana au kuchaguliwa na watu,” alisema.
  Taifa la hofu, woga
  Kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema kuwa wakati akifanya maandalizi ya uzinduzi wa M4C, aligundua kitu kilichomsikitisha kuwa Watanzania wengi wamejengwa utii wa hofu na woga badala ya kuheshimu misingi ya kudai haki na wajibu.
  “Wananiambia Mbowe bwana sisi tunawasapoti sana na tuko pamoja na ninyi lakini kutokea pale Naura Springs aah tuna hofu, tunaogopa, kuna TRA hapo oooho, kuna polisi hapo ohooo. Lakini kupitia hapa leo tunataka kuwathibitishia wengine wote ambao bado wana hofu na woga katika kupigania masilahi ya Watanzania, sisi CHADEMA tulishamaliza woga na hofu siku nyingi, tunatangulia watatukuta mbele ya safari.
  Slaa anena
  Dk, Slaa alisema kuwa chama hicho kinataka kudhihirisha kauli yao ya ‘People’s Power’ (nguvu ya umma) kwa matendo, si kwa maneno, ambapo aliwataka Watanzania wote wapenda demokrasia na maendeleo kote waliko kutumbukiza chochote walichonacho.
  Akizungumzia juu ya uchaguzi wa Arumeru Mashariki, alisema kuwa wanazo taarifa za kutoka kikao cha ndani cha CCM ambako Rais mstaafu Benjamin Mkapa aliagiza kuwa chama tawala kishinde kwa ‘vyovyote vile’ ikibidi kuvunja haki, sheria na taratibu ili watakaoshindwa waende mahakamani.

  SOURCE : Tanzania Daima
   
 2. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Hii habari ni KIPORO!
  Ilishachacha siku nyingi sana!
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WaTanzania tumekwishaamua, ni nani tena wa kutuzuia katika safari zetu hizi zenye mantiki na haja ya msingi ki-utawala kwa manufaa ya walalahoi kote nchini????????
   
 4. P

  PolisiB52 Member

  #4
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  safi sana hiyo makamanda viva chadema
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  BAVICHA SASA KIPENGA PIEEEEEEEEEEE MPAKA USHINDI MURUA WA HAKI NA UTETEZI WA UTU WA KILA MTANZANIA UPATIKANE BILA ZENGWE ARUMERU MASHARIKI TANGU SASA!!!!!!!!!!!!!

  Askari wetu wa miavuli BAVICHA,

  katika hii wiki ya lala salama Arumeru ni vema kuliko kawaida 'Dozi ya Siasa za Kistaarabu' mkanyunyiza mtindo wa Igunga kutwa mara tatu kufikisha ujumbe wa ukombozi katika kila lango la kila mpiga kura katika kila kijiji jimboni hapo na hatimaye kuhitimisha kwa mkakati wa kufa mtu katika kudhibiti usalama wa kila kura itakayopigwa siku hiyo.

  Kamanda Heche tunahitaji kuona organisation skills na usimamizi wa kitimu kwa kushirikiana kwa karibu sana na machalii wote wa Arumeru Mashariki (kama Kamanda Vincent Nyerere tangu alivyofanikiwa na msaidizi wake Mchungaji) tangu sasa.

  Kipenga pieeeeee, pipoz pawaaaaa mpaka ushindi kuubeba mbeeeele kama tai huku sote tukishirikiana kwa kila hali kila mahali na kila waka!!!!!!!!!
   
 6. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Hivi kumbe hata TRA wanatumiwa kama mawakala wa mafisadi kunyonga demokrasia?? Hii ni aibu ya hali ya juu kwa kamishna wa TRA kwani inaonyesha kuwa SUBJECTIVITY katika kukusanya kodi ni kubwa. Ndo maana wafanyabiashara wengi wanapandisha bendera za ccm ili kukwepa kodi
   
 7. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Safi makamanda ntaendelea kuchangi chama changu makini maana najua ninachokifanya na tena kwa hiari yangu,kwa uwezo wangu,kwa akili zangu timamu na bila kurubuniwa na anybody.People let us make changes in this country attacked by mafisadi!,mim naamin kuwa mpiganaji hashndwi hata kidogo hata akishindwa atarud kujipanga upya na kurud kwenye scene kama kawa.Magamba aka ccm hawana lolote zaid ya kutishana,kuwanunua polis na kuiba rasilimali za watu!!.Kwa sasa nataka niongeze nguvu kwa makamanda japo kaz yangu ni kusukuma mkokoteni na maguta na nnamachungu na nch hii mwanzo mwisho!.I gonna fight to the end till the end of my distination.Namalizia hv sumu ya magamba ni pipooooz pawaaaaaa! Over!!
   
 8. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Lete ya kwako mpya.
   
 9. d

  dada jane JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unanichekeshaga kweli unakihelele kama pua yako.
   
 10. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Shikamoo mwalimu!
  Lindi na mtwara wazima? Lini CDM wanakuja kufanya fund rising huko?
   
 11. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Leo sina mudi ya kuchakachua sreadi!
   
 12. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  meno yale....
   
 13. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Hela zote zinaingia counter ya Bills.
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Siasa za Tanzania bwana,zina mvuto kweli kwenye majukwaa na magazetini. Sijui katika utekelezaji mambo yanakuwa vipi
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Chadema nawapongeza kwa harambee yenu mliyofanya Arusha, cha msingi ni kufahamishwa matumizi ya michango yenu imetumikaje.
   
 16. m

  mr who Member

  #16
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  mmechangishana sana, kwa mbwembwe nyingi, je matumizi nao ytatolewa star tv, au ndio kimyakimya
   
 17. P

  Pelege Senior Member

  #17
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana makamanda tupo pamoja katika mapambano haya ya kuwang'oa hawa CCM majambazi
   
 18. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,105
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  ndo maana wafanyabiashara wengi wanakimbilia kwenye siasa ili kuua ndege wawili kwa jiwe moja. Kukwepa kodi na kupata ulaji! Hivi unaweza kuamini nchi hii wafanyakazi ndo wanaongoza kwa kulipa kodi? Mtu ambaye pato lake halizi 20000 kwa siku anamzidi mtu mwenye faida ya m1 kwa siku? It is only in tz where inawezekana.
   
 19. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #19
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ilichacha Kama wewe ulivyochacha
   
 20. L

  Lalida New Member

  #20
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 25, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chadema kaz yetu ni moja ya kureta mabadiliko
   
Loading...