CHADEMA yachangiwa mamilioni

Mapato na matumizi yatatolewa kwa wananchi kupitia mikutano zitakazokuwa zinafanyika, either kupitia STARTV ama mikutano ya moja kwa moja.
Chadema nawapongeza kwa harambee yenu mliyofanya Arusha, cha msingi ni kufahamishwa matumizi ya michango yenu imetumikaje.
 
Chadema nawapongeza kwa harambee yenu mliyofanya Arusha, cha msingi ni kufahamishwa matumizi ya michango yenu imetumikaje.

hata ilivyoanza opareshen sangara mlikuwa mnakebehi hivi hivi. Mlivyokosa majimbo yote ya shinyanga ndipo mkajua umuhimu wake. Thanks to teachers vijana wanaoendelea kutoa elimu ya kujitambua kwa wanafunzi.
 
Mapato na matumizi yatatolewa kwa wananchi kupitia mikutano zitakazokuwa zinafanyika, either kupitia STARTV ama mikutano ya moja kwa moja.

Kuna thread imeanzishwa wanasema Chadema wamepata mil 150 ni kweli?
 
Chadema nawapongeza kwa harambee yenu mliyofanya Arusha, cha msingi ni kufahamishwa matumizi ya michango yenu imetumikaje.

harambee ilikua kwaajili ya kupata kupata pesa ya kusaidia kutoa elimu ya uraia kwa wananchi kuanzia taifa,mkoa,wilaya,mpaka kitongoji juu ya katiba mpya ikienda sambamba na ufunguzi wa ofisi za chama kila kata nchi nzima.
 
Tutachanga mpaka Magamba wahame inchi hii.CHADEMA M4C Towards the next presidencial race 2015
 
juzi usiku chadema ilizindua kampeni ya ‘vuguvugu la mabadiliko’ ambapo wapenzi wa harakati za mabadiliko nchini walikichangia chama hicho sh milioni 150.
Viongozi wa chadema akiwamo mwenyekiti wa taifa, freeman mbowe, na katibu mkuu, dk. Willibrod slaa, walisema kupitia ‘vuguvugu la mabadiliko’, chama hicho kinakwenda kuanzisha elimu ya uraia na elimu ya katiba mpya nchi nzima.
Walisema chadema inataka kupigania mabadiliko ya kweli ya kuondoa utawala mbovu miaka 50 baada ya uhuru, hasa kwa kupiga vita ufisadi na kudai uwajibikaji wa viongozi kwa maendeleo ya watu.
Viongozi hao walisema mkakati wa chama hicho ni kukiweka mikononi mwa wananchi wa kila kada, ambapo kila mtanzania mwenye machungu na nchi yake ataweza kuchangia fedha ili kukisaidia chama hicho kuchukua dola kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mbowe alisema mabadiliko ya kweli nchini yatafanikiwa kwa watanzania waadilifu kuunganisha nguvu zao dhidi ya ufisadi wa watawala walioko madarakani, chini ya chama cha mapinduzi (ccm).
Aliwaambia mamia ya marafiki wa chadema waliokusanyika katika hoteli ya naura springs kwa ajili ya uzinduzi huo kuwa chama hicho hakitakuwa na masihara katika kulinda na kupigania haki na utu wa mtanzania katika kulinda rasilimali za taifa ili zitumike kwa masilahi ya watu wote.
“leo tunakwenda kujenga historia mpya, tena ya kufanya siasa za uwazi na ukweli, tunataka chama hiki kwa vitendo kabisa kiwe chama cha watu, kitakachosimamiwa na watu, kitachangiwa na watu na kitaongozwa na viongozi wanaotokana au kuchaguliwa na watu,” alisema.
taifa la hofu, woga
kiongozi huyo ambaye pia ni mbunge wa hai na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, alisema kuwa wakati akifanya maandalizi ya uzinduzi wa m4c, aligundua kitu kilichomsikitisha kuwa watanzania wengi wamejengwa utii wa hofu na woga badala ya kuheshimu misingi ya kudai haki na wajibu.
“wananiambia mbowe bwana sisi tunawasapoti sana na tuko pamoja na ninyi lakini kutokea pale naura springs aah tuna hofu, tunaogopa, kuna tra hapo oooho, kuna polisi hapo ohooo. Lakini kupitia hapa leo tunataka kuwathibitishia wengine wote ambao bado wana hofu na woga katika kupigania masilahi ya watanzania, sisi chadema tulishamaliza woga na hofu siku nyingi, tunatangulia watatukuta mbele ya safari.
slaa anena
dk, slaa alisema kuwa chama hicho kinataka kudhihirisha kauli yao ya ‘people’s power’ (nguvu ya umma) kwa matendo, si kwa maneno, ambapo aliwataka watanzania wote wapenda demokrasia na maendeleo kote waliko kutumbukiza chochote walichonacho.
akizungumzia juu ya uchaguzi wa arumeru mashariki, alisema kuwa wanazo taarifa za kutoka kikao cha ndani cha ccm ambako rais mstaafu benjamin mkapa aliagiza kuwa chama tawala kishinde kwa ‘vyovyote vile’ ikibidi kuvunja haki, sheria na taratibu ili watakaoshindwa waende mahakamani.

source : Tanzania daima

hapo kwenye red umeharibu mtiririko mzuri wa mada yako kwani hapo panahitaji dk. Slaa atuambie kikao hicho kilifanyika wapi na tarehe ngapi angalau kuongeza nguvu kwenye ukweli wa tuhuma hizi.
 
Harambee imeonyesha mwanzo mzuri kwa CDM kuongeza mapato yake lakini wasiwakamue sana wananchi bado hali yao ni maskini wamepigika
 
Kuna thread imeanzishwa wanasema Chadema wamepata mil 150 ni kweli?

Ndiyo. Nimethibitisha toka Katibu Mkuu, Dr Slaa, kwamba michango iliyotolewa pale pale ukumbini ilifikia zaidi ya TSh. 150m. Bado kukisia na kupokea zilizoahidiwa katika Mtandao.
 
Back
Top Bottom