CHADEMA yachangiwa mamilioni kwa ajili ya uchaguzi Arumeru

Chadema vigeugeu kweli. Wa kwanza kusema wananchi wana maisha magumu, haohao wanakwenda kuwanyang'anya hata kile kidogo walichonacho kwa kuwatembezea bakuli. si usanii huo, ila ndiyo laana yao, walifanya hivyo uchaguzi mkuu, Igunda, Busanda lakini mwishoe chali.

IGUNGA CCM nasikia waliuwa askari mmoja wa polisi kwa kuwa alikataa kuchakachua matokeo.

kwani maskini huwa mwiko kusaidiana?
 
Hiyo figure mkuu ni kubwa sana (Milioni809,545,848) ni sawa na Bil. 809.5 sidhani kama CDM wanapata hizo,unazidi kujionyesha utupu wako, huwa nakuambia shule ndogo yale yale huwezi kupata Wikipedia hadi uwe na Google... poor boy, inawezekana huwa tunabishana na mtoto wa Form 1 hatujui.
Mkuu ukishamjua mtu kama huyu then unaacha kubishana nae
 
Chadema kimekusanya Sh8 milioni kutokana na harambee ya kukichangia iliyoanza juzi katika uzinduzi wa kampeni za jimbo hilo.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba alisema fedha hizo zimekusanywa kupitia michango ya papo kwa papo na simu. Alisema Sh2.2milioni zilikusanywa uwanjani na Sh5.7 milioni zilikusanywa kwa njia ya simu hadi kufikia juzi jioni.

Alisema chama hicho kimeandaa chakula cha jioni Ijumaa wiki hii kwa ajili ya kukusanya fedha za kugharamia kampeni hizo... “Nia ya kukusanya fedha hizi ni kutaka watu wajione ni sehemu ya Chadema katika shughuli mbalimbali za chama.”

Source:Mwananchi
Hala hala hayo ma M-pesa na ma tigo pesa wasije wakazifunga hizo namba kwa maelekezo ya magamba. Nakumbuka mwaka 2010 niliwahi kupata tabu sana kuchangia kwa njia ya M pesa. Mara unaambiwa namba haipo, mara haipatikani, mara.....yaani fitna kibao.

Otherwise hapo tulipo mwendo mzuri.
 
Chadema vigeugeu kweli. Wa kwanza kusema wananchi wana maisha magumu, haohao wanakwenda kuwanyang'anya hata kile kidogo walichonacho kwa kuwatembezea bakuli. si usanii huo, ila ndiyo laana yao, walifanya hivyo uchaguzi mkuu, Igunda, Busanda lakini mwishoe chali.
Nina amani kubwa moyoni, nimetuma kahamsini elfu kangu, nikapata ujumbe kuwa nimechangia CHADEMA ARUSHA - ukweli ni kuwa nimechangia mabadiliko Tanzania. Kila la heri CHADEMA, mjazwe na ulinzi wa mkono wenye nguvu kutoka kwa Muumba wetu, na Muumba awaoneshe CCM wategemea nguvu za giza kuwa yeye ni Mkuu kuliko shetani.
 
Inafanya shughuli nyingine. CCM wanaowaomba wahindi wanapata ruzuku kiasi gani?
Sio kweli hata kidogo. CCM haiwaombi wahindi kuchangia chama chao. CCM inawalazimisha tena kwa vitisho wahindi na wafanyabishara wazawa kutoa fedha katika style iliyosawa na unyang'anyi wa mchana kweupe.
Viongozi wa juu ndio vinara wa kuandika vimemo vya "TOA SHILINGI KAZAA KUKICHANGIA CHAMA"
Ila kwa sasa wachangiaji hao (wahanga wa unyang'anyi huo) wamepungua sana baada ya elimu ya uraia inayotolewa na CDM kuwaondoa woga. Watoaji waliobaki ni wale wenye maslahi na utoaji huo katika ufisadi wa aina fulani.
 
CDM ebu acheni kuwanyonya watanzania nyie wenyewe mnasema nchi ngumu watu hawana pesa bado hapo hapo mnazidi kuwakamua.
 
CDM ebu acheni kuwanyonya watanzania nyie wenyewe mnasema nchi ngumu watu hawana pesa bado hapo hapo mnazidi kuwakamua.

pata akili mkuu hapo chadema haiwanyonyi wananchi bali wanatoa kwa mapenzi yao wenyewe kwa kuipenda chama chao wenyewe na wanatoa chochote walichonacho lakini ccm WAMETUMALIZA WANATUNYONYA BILA YA HIARI YETU SISI.
 
Back
Top Bottom