Chadema yabeza V4C ya CUF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yabeza V4C ya CUF

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Sep 18, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jumanne, Septemba 18, 2012 05:43

  Na Benjamin Masese, Dar es Salaam


  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimebeza mkakati wa kisiasa uliozinduliwa na Chama cha Wananchi (CUF). Chadema imekejeli mkakati huo kwa kusema kuwa CUF haina uwezo wa kuendesha Operesheni ya Dira ya Mabadiliko (V4C) nchi nzima.

  Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya CUF kufanya matembezi ya hisani ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwezesha operesheni hiyo kuzunguka nchi mzima.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi, Msafiri Mtemelwa, alisema CHADEMA inasikitishwa na kauli za CUF za kuwahadaa Watanzania.

  Mtemelwa alisema chama hicho hakina uwezo wa kuzunguka nchi nzima kunadi mkakati wao na kwamba kusema kinakwenda kubomoa ngome ya CHADEMA jijini Arusha ni siasa za kitoto.

  "CHADEMA hatuendeshi kampeni zetu kwa kubomoana, tunapeleka sera zetu kwa wananchi pamoja na mipango ya kuwakomboa wananchi kutoka kwenye umasikini.

  "Pia tunapeleka hoja zetu kwenye vyombo vya maamuzi, tunawaomba CUF kuwa makini wasiige, ili wasije wakaaibika mbele ya safari. Moto wa Chadema hawauwezi," alisema.

  Mtemelwa aliongeza: "CUF wanapaswa kujitathimini kwanza, wanakwenda Arusha kwa mtaji upi na wana hoja zipi za kuwaeleza wananchi.

  "Ndani ya CUF hakuna mtu mbunifu wa kupanga na kufanikisha operesheni nchi nzima, hawana mikakati imara, hawana nyenzo wala mtaji.

  "Tunawaomba wasiige kinachoanzishwa na CHADEMA na kujigamba kuwa wanaweza, tumeanzisha M4C nao wameanzisha V4C, itakufa kabla ya kufika mikoa 10," alisema.

  Mtemelwa alisema CHADEMA haitasita kushirikiana na taasisi na watu wenye nia nzuri ya kutafuta ukombozi wa kweli katika kujenga demokrasia.

  Mbali na suala la kuzunguka nchi nzima, CUF pia kilisema hakipo tayari kupokea fedha zozote au msaada kutoka kwa matajiri, akiwamo mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo, kama ilivyo kwa CHADEMA.

  Akizungumzia kauli hiyo, Mtemelwa alisema. "Sabodo ni raia wa Tanzania ingawa ana asili ya Kihindi, hivyo basi CHADEMA tutaendelea kupokea misaada kutoka kwa Mtanzania mwenzetu mwenye uzalendo, ila hatupo tayari kupokea fedha kutoka kwa mtu mchafu hata kama ni Mtanzania.

  "Sabodo anatoa fedha kwa CHADEMA baada ya kuona mwenyewe kazi inayofanywa na chama ya kupambana na ufisadi, tunawatetea Watanzania katika masuala muhimu ya kijamii.

  "Wanasema Sabodo anatoa fedha CCM na CHADEMA na kudai ana jambo la siri juu ya misaada hiyo, niwahakikishie CUF kwamba kama wanakerwa au hawajapata misaada hiyo wajue hawajafanya jambo la maana kwa jamii," alisema.

  Mtemelwa alisema CCM na CUF wamekuwa wakiiga mikakati inayoanzishwa na CHADEMA, lakini imekuwa ikiishia njiani na kushindwa kuleta mafanikio kama walivyokuwa wamekusudia.

  Alisema baada ya vyama hivyo kushindwa kuhimili mikiki ya CHADEMA, wameamua kutumia vyombo vya dola, likiwamo Jeshi la Polisi kuzuia operesheni zao kwa lengo la kukidhoofisha.

  Mtemelwa alisema Serikali ya CCM imekuwa na mikakati ya kukichafua CHADEMA na kueneza propaganda chafu kwamba ni chama cha fujo na vurugu.

  Pamoja na mambo mengine, alitoa wito kwa CUF kuwa makini katika kueneza sera zao kwa wananchi na kuongeza kwamba hakuna siasa za kubomoana kwa vyama vya upinzani.

  Alisema ikiwa CUF itaendesha operesheni zao za kukibomoa CHADEMA haitafanikiwa kufika mbali, badala yake chama hicho kitaaibika.

  Juzi CUF ilifanya matembezi ya hisani ya kukichangia chama hicho na kufanikiwa kukusanya Sh milioni 129, huku Sh milioni 325 zikitajwa kama ahadi.

  Matembezi hayo yaliongozwa na Mwenyekiti wa wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba, ambaye alichangia Sh 110,000.
   
 2. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,743
  Likes Received: 6,018
  Trophy Points: 280
  Haya bana. All the best CUF ila kuweni wabunifu badala ya kuiga vya wenzenu. Hawa wakianzisha operesheni Sangara na nyie mnaanzisha Zinduka; wakianzisha M4C na nyie V4C! Hamuwezi kubuni vyenu? Mna vichwa au nazi?
   
 3. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  ".....Mtemelwa alisema chama hicho hakina uwezo wa kuzunguka nchi nzima kunadi mkakati wao na kwamba kusema kinakwenda kubomoa ngome ya CHADEMA jijini Arusha ni siasa za kitoto."

  Hapo mimi ndiyo huwa nachoka na CUF,kuweka upinzani kwa vyama vya upinzani,kweli ukiishaolewa kazi kweli kweli.
   
 4. K

  KANA KA NSUNGU J Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbe mbio zote hizo ni kuibomoa CHADEMA na si kuhubiri sera zao. kuwatafsiria wananchi habari za maendeleo, elimu ya uraia na kufichua ufisadi.
  Kweli CUF hakuna wabunifu na ndo kina kwisha hivyo
   
 5. K

  KANA KA NSUNGU J Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbe mbio zote hizo ni kuibomoa CHADEMA na si kuhubiri sera zao kama vile kuwatafsiria wananchi habari za maendeleo, elimu ya uraia na kufichua ufisadi.
  Kweli CUF hakuna wabunifu na ndo kina kwisha hivyo
   
 6. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Yale yale, vyama visivyo na vision hata ya miezi sita hujikuta kikicopy na kupaste kila afanyacho jirani, thou nashawishika Bi.Mkubwa CUF kaagizwa na mumewe ccm aanzishe hizo movement, tusishangae mfadhili wao akawa jamaa wa M.soga
   
 7. K

  KANA KA NSUNGU J Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema walipo omba waonane na Rais Ikulu kwa ajili ya kutoa duku duku zao juu ya sheria ya uendeshaji zoezi la katiba, tukashangaa nao CUF kesho kutwa wameomba ombi hilo hilo.Mara tukaona akina mtatiro wakicheka na vikombe vya kahawa mkononi wakiwa ikulu.
  Poleni sana CUF. Kesho CDM wakisema wanakula kinyesi basi utasikia CUF nao wanataka kula kinyesi kisa CDM wamekula
   
 8. K

  KANA KA NSUNGU J Member

  #8
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliye mpa mtatiro nafasi kubwa namna ile alokosea sana.Huyu bwana mdogo ana utoto mwingi na ndo maana ana leta bifu hata katika harakati za kukomboa nchi.
  Hii ina dhihirisha aliposhindwa ku solve matatizo ya CUF pale Lipumba alipokuwa hayupo.

  Kwa CDM tunajua wapo wengi wa kuongoza hata kama Slaa na Mboye hawatakuwepo.Hivi jamani tufikirie, asipokuwepo Lipumba je kutakuwa na CUF?
   
 9. B

  Ba'mdgo JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nilisikia walvyoponda pale jangwani kuhusu M4C na kudai ni ya muda tu lakini V4C ni endelevu kwajili ya kuikomboa nchi
   
 10. M

  Mr.Mpugusa Member

  #10
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 11, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka acha wivu, kwani kama wameiga wao ni wakwanza? Mbona cdm inaiga mengi tu na hauyasemi? CCM ilikuwa imejikita kufungua matawi huko ulaya wana cdm wakaongea sana humu Jf na matokeo yake sasa hivi cdm ndio imeshika kasi hilo ni moja, CUF ndio chama cha kwanza kuanzisha move ya kudai katiba mpya mbona cdm walivyoiga hukusema? CUF ndio walioanzisha sera ya wanafunzi kuweza kusoma bure na ccm wakaiiga pia cdm nao huwa wanaipigia debe mbona hilo pia hulisemi. Mie binafisi sijaona ambalo nyie hamkopi kwa ccm.
   
 11. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hivi kampeni za mabwana wa CUF ziliishia wapi baada ya jangwani!? "Vua gwanda, Vua gamba Vaa Uzalendo"
   
 12. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,216
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Siasa ni ngumu ccm hawalii na cuf tena hii kitu m4c inawaumiza kichwa hizi movement nyingine hawana habari nazo.
   
 13. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Daaaaaaah kumbe mchakamchaka wa Cuf ni kuibomoa chadema! Kazi wanayo
   
 14. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #14
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,736
  Likes Received: 1,447
  Trophy Points: 280
  Hii ni aibu sana kwa chama chochote cha siasa chenye nia ya kushika dola.

  Ni wazi CUF wamepotea njia, hawana hata dira kuwarudisha walikotoka! Ndio maana huwa nasikitika nikimwona yule prof. wao akijichanganya kwenye hili tope najisemea 'kweli njaa ni utumwa, huondoa akili kichwani mwa mwenye nayo'
   
 15. wijei

  wijei JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Ndoa tamu,CUF ilishaonja mjebere wa NYINYIEM,lazima isaidie mme wake kwa hali na mali ili kuidhoofisha CDM.
   
 16. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hizi ndio siasa za bongo bana
   
 17. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #17
  Sep 18, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  CUF nao sasa kazi ni kuibomoa CHADEMA. Wiki mbili zilizopita ilikuwa ADC kupitia Hasan akisema wamejipanga kuibomoa CHADEMA. Majuzi kukatokea CCK, n.k., Sasa unajiuliza swali kwamba je hivi vyama vinavyojiita vya upinzani vina malengo gani na CHADEMA? Je CHADEMA ndiyo inashikilia DOLA? Hapa kuna jibu moja tu rahisi kwamba vyama vyote hivi vinavyojiita vya upinzani tofauti na CHADEMA vinatumiwa na CCM ili kudhoofisha upinzani nchini.
   
 18. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #18
  Sep 18, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu Dudus,
  Hawa jamaa wana Vichwa vya kufugia Nywele.

  TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),
  tumbiri@jamiiforums.com
   
 19. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #19
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mtetezi wa Muungano wa wapinzani wa Tanzania kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kweli ya Tanzania. Kufika wakati vyama vya upinzani vinahangaika kubomona, kuonana maadui wao kwa wao na kumwacha adui wao wa pamoja anadunda, sioni hatima ya upinzani madaraki Tanzani. Naomba Mungu niwe nimekosea katika dhana yangu hii. Ni wakati ndio utakaoamua.
   
 20. s

  sapal kihava Member

  #20
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikifuatilia sana mikutano ya CUF nimegundua kinacho wasumbua CUF nipamoja na: chama hiki cuf kinazidi kuwa changa, kimekosa wasomi, kimejaza udini ndani yake ndomana walitaka kumfukuza mtatiro wakidai ni kibaraka wa chadema, pia chama hiki hakina mtu mashuhuri zaidi ya Lipumba,chama hiki hakina mtaji wa kutosha na ndo maana kipindi cha uchaguzi kilipewa pesa naCCM ili kuwalipa Makarani wake. CUF bado sana mjiunge na wenzenu ADC labda mta badilika lakini kuisambaratisha CHADEMA nyie bado sana Tambueni tatizo lililopo kwa sasa ni namna ya kuiondoa CCM madarakani Fungukeni CUF !
   
Loading...