CHADEMA yaanza mikakati mizito ya ushindi

• Mikakati mizito ya ushindi yaanza

na Tamali Vullu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kitachukua hatamu za uongozi wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa madiwani, ubunge na urais wa mwaka 2015.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, katika mkutano maalumu wa viongozi wa Kanda ya Dar es Salaam wa chama hicho, ambapo Dk. Willibrod Slaa alikuwa mgeni rasmi.

Dk. Slaa alisema kwa sasa chama hicho kimeanza kuandaa mikakati mizito yenye mbinu za kisasa na za uhakika ili kiweze kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambayo hata hivyo, hakuweza kuitaja.

Hata hivyo, aligusia kuwa hivi sasa chama hicho kimefanya marekebisho ya ratiba ya uchaguzi wake wa ndani, ili kuweza kujipanga vizuri kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.

"Nimetoa waraka wa kufanya marekebisho ya ratiba ya uchaguzi ndani ya chama. Badala ya kufanyika kila baada ya miaka mitano ambayo huwa karibu na mwaka wa Uchaguzi Mkuu tumerudisha nyuma, hivyo chaguzi ndani ya chama zitaanza mwakani katika ngazi mbalimbali na kukamilika mwaka 2013.

"Tunaamini tukifanya uchaguzi mapema tutaweza kumaliza makovu ya uchaguzi huo, hivyo kuingia katika Uchaguzi Mkuu tukiwa kitu kimoja," alisema Dk. Slaa.

Alisema sasa CHADEMA kimepokewa vema na kukubalika kuwa chama cha Watanzania wengi, hivyo ni muhimu viongozi kuanza kufikiri tofauti, ili waendane na matakwa ya wananchi.

"CHADEMA ni tumaini jipya, hivyo haiwezi kuwa na mbinu zilezile zilizotumika mwaka 2010, hivyo viongozi hamtakiwi kuacha fikra kwa ngazi moja. Fikra za mbinu mbalimbali zinatakiwa zitoke kuanzia ngazi ya kata, wilaya, mkoa na hata taifa, kwani tunahitaji mabadiliko ya kifikra," alisema.

Aiwataka viongozi hao kusambaza waraka huo kwa wanachama na kufanya kazi ya kuwaelimisha. Aliongeza kuwa kiongozi atakayeshindwa kufanya hivyo atakuwa ameshindwa kwenda na kasi ya chama hicho.

"Muda wa kubebana sasa umekwisha, atakayeshindwa kutekeleza haya itafika mahala tutachapana, ni lazima waraka huo ufike chini kwa wananchi. Nitapita eneo kwa eneo kuhakikisha kama hilo limefanyika na kwa watakaoshindwa kufanya hivyo nitatumia katiba kuwaondoa na kuwaweka viongozi wa muda. Hatuwezi kuendelea na viongozi wa aina hii," alisema Dk. Slaa huku akishangiliwa na viongozi hao.

Dk. Slaa aliwataka viongozi hao kukutana naye Januari 5, mwakani ambapo watatoa taarifa ya utekelezaji wa waraka huo pamoja na ushahidi.

"Chama si kitu cha mchezo. Watu tunahangaika nchi nzima na tumeweka rehani maisha yetu, wengine mnakaa tu, nawaambieni sasa tutachukua maamuzi magumu," alisema.

Alisema chama hicho kitaweza kufanikiwa zaidi iwapo watainua sauti za wanyonge, hivyo viongozi wabadilike katika utendaji kazi.

Dk. Slaa alisema CHADEMA kinatarajia kutumia njia ya ‘database' kuwasiliana na wanachama wake kama walivyofanya viongozi wa chama hicho mkoani Arusha.

"Kwa kutumia mfumo huo, ukituma ujumbe mfupi wa maandishi (sms) moja inaweza kufika kwa wanachama zaidi ya 5,000, hivyo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa viongozi kusanyeni namba za wanachama wetu ili tuingize kwenye utaratibu wa aina hiyo,"alisema.

Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alionesha kukerwa kwake na mgogoro unaotaka kuibuka katika Jimbo la Segerea, huku ikijulikana kuwa aliyekuwa mgombea wao, Fred Mpendazoe, amefungua kesi ya kupinga matokeo ambayo inaendelea vizuri mahakamani.

"Segerea nianze na ninyi, nimewapa maelekezo hamjayafanyia kazi. Chama kimetumia sh milioni 12 katika kesi ya kupinga matokeo ya jimbo hilo na inaendelea vizuri, sasa viongozi mmeanza migogoro.

"Mmeanza kueleza mabaya ya Mpendazoe. Mpendazoe si mtu wa kawaida. Nawapa wiki mbili mgogoro huo uwe umeisha, kwani ni mgogoro wa kipuuzi," alisema.

Aliwashauri viongozi hao kuanzisha matawi na kusimika mabalozi wa nyumba tano, kwani huo ni mtaji wa kisiasa na kuongeza kuwa ni lazima chama kifanye kazi kisayansi.

Akizungumzia mchakato wa Katiba mpya, Dk. Slaa alisema ni lazima mchakato huo urudi kwa wananchi ili waweze kutoa maoni yao na kuongeza kuwa CCM inahofia suala hilo kwa kuwa hawakubaliki kwa wananchi.

"Tukiruhusu Rais Kikwete aunde tume hakuna cha maana kitakachofanyika. Mimi nina uzoefu, nilikuwa mbunge na najua uovu wote na pia nilikuwapo kwenye Tume ya Jaji Kisanga. Wakati ule tume inakusanya maoni, CCM ilituma mawaziri wake waende kwa wananchi na kuwafundisha jinsi ya kujibu hata kabla tume haijaenda, hivyo tume ile iliyoundwa ilikuwa ni geresha tu," alisema.

Alisema rais akishaunda tume wananchi hawana mamlaka, ndiyo maana wanaipinga na kwamba ikiwapo hata maoni yatakayotolewa na wananchi hayatafanyiwa kazi.

Kwa upande wake, Mbunge wa Ubungo John Mnyika, alisema kinachofanyika sasa ni kuwaelimisha viongozi wao kuhusu sheria ya mabadiliko ya Katiba na baada ya hatua hiyo watakwenda kwa wanachama wa kawaida.

Alimshauri Rais Kikwete asiunde tume ya kukusanya maoni kuhusu Katiba mpya, kwani akifanya hivyo atasababisha mgogoro. "Pamoja na rais kusaini muswada huo tunamshauri sheria hiyo isianze kutumika mpaka yatakapofanyika marekebisho ya msingi. Akiunda tume, hatutashiriki, bali sisi tutakwenda kwa wananchi na kuwaeleza kuhusu jambo hilo, njia tutakazotumia tutazieleza baadaye iwapo jambo hilo litatokea," alisema.

CDM bado, wajiimarishe mno vjjn huko wakati huu, illiterate people vjjn humo wanakawia sana kuelewa habari ya mabadiliko though wakisha ikubali it steaks in them forever
 
Huu ndio Mfumo wa Uandishi habari nisioupenda, 'amesema' 'amaeeleza' hakuna hata sehemu ambayo Mwandishi amefanya analysis ya hali ya kisiasa nchini ili kupima uhalisia wa Maelezo ya Dr. Slaa au vipi..Habari nzima imejaa quotes za Dr. Slaa halafu ati anaiita Habari. Waandishi wetu vilaza kwelikweli. Si angerekodi crip ya sauti atusikilizishe!
 
Nadhani mwandishi alilenga kutoa taharifa tu na uchambuzi wa taharifa yenyewe haikuwa focus yake..wapo wengine wanaoweza kufanya analytical presentation

Kwa mikakati hii naamini ndege itapaa tu,safi sana General Secretary
 
Swala analysis ni la mtu mwingine, kama unaweza siufanye wewe? Mbona kumekaa kilawama lawama. Ujumbe wa mwandishi ni kuatoa taarifa ya nini Dr. Silaa kasema, na hicho ndicho alichokisema. Nasubiri analysis yako.
 
dr slaa aka mze ambaye ana mchumba mke wa mtu amechoka sana.ivi mbona amepotezea ile kunywa juice ikulu.aliogopa nn?
 
Nakukumbuka tulijadili hili sana hapa JF wakati Dr alipoteuliwa kuwa mgombea Urais. It was too late na hakupata muda wa kijinadi. Hata kufanya uchaguzi 2013 halafu uchaguzi mkuu ni 2015, bado naona atakayechaguliwa atakuwa na muda mfupi sana wa kutandaza zege. Kwa nini wasifanye kama wanavyofanya in the West? Kwamba baada ya Uchaguzi mkuu, kama mgombea urais hakufanikiwa kushinda, then chama kinafanya uchaguzi immediately after the general election. Hapo atakuwa na at least miaka minne ya kujijenga na kuzunguka nchi kunadi sera za chama.

Having said that sidhani kama ni sahihi kwa Chadema kusema kuwa kitachukua hatamu ya uongozi katika uchaguzi ujao. The ultimate decision itakuwa kwa Watanzania kama kweli wanataka mabadiliko. Are Tanzanians ready for a change? Few but not all.
Pengine mkuu wangu umesahau leo.. Dr.Slaa alikuja wakati muafaka kabisa maana ni baada ya uchaguzi tu ndipo hizi habari za Chadema chama cha Kikristu, Dr.Slaa Padre aliyemwacha mkewe na kuzini nje yalikuja kuwa hoja na pandikizi kubwa la hofu kwa wapiga kura. Bahati lilikuja ota mizizi baada ya uchaguzi lakini kama inngekuwa mapema CCm wangemmaliza Dr. Slaa kwa sababu nimegundua kwamba kujibu maswala ya Udini unataka moyo mkubwa sana na Dr. Slaa si mtu wa kujiingiza kichwa kichwa ktk migogoro kama hiyo.

Kilichofanyika Dr. Slaa aliibiwa kura nyingi sana na ushahidi upo wazi kabisa isipokuwa chama kijifunze zaidi sababu kubwa zilizowafanya kushindwa mwaka 2010. Binafsi yangu Chadema wanashindwa sii kwa sababu ya kutokuwa na mbinu ama walikuwa na mapungufu makubwa mwaka 2010, bali mfumo mzima wa uchaguzi toka katiba hadi usimamizi wake ndio hasa sababu ya kushindwa vyama vya upinzani nchini tumeyaona haya toka Mrema, Maalim Seif (Zanzibar) Lipumba, Na hata ndani ya CCM yaliyomkuta Salim A. Salim na mzee Malecela..

Sasa hivi inatakiwa tuwe tumeshajifunza..Maadam vyombo vya kusimamia upigaji kura sii vyombo huru, wakuu wa mikoa, wilaya na Polisi ni wateule wa rais hamuwezi kushinda kura hata kama wananchi wote wamekichagua Chadema...Fanya mtakavyofanya bila katiba hii kubadilika kabla ya mwaka 2015 Chadema haiwezi kushinda...labda tutegemee mwaka 2015 kuwa mwaka wa machafuko nchini...Nimeyasema leo na nitayarudia mwaka 2015 - InshaAlaah tukijaliwa Uzima..
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Pengine mkuu wangu umesahau leo.. Dr.Slaa alikuja wakati muafaka kabisa maana ni baada ya uchaguzi tu ndipo hizi habari za Chadema chama cha Kikristu, Dr.Slaa Padre aliyemwacha mkewe na kuzini nje yalikuja kuwa hoja na pandikizi kubwa la hofu kwa wapiga kura. Bahati lilikuja ota mizizi baada ya uchaguzi lakini kama inngekuwa mapema CCm wangemmaliza Dr. Slaa kwa sababu nimegundua kwamba kujibu maswala ya Udini unataka moyo mkubwa sana na Dr. Slaa si mtu wa kujiingiza kichwa kichwa ktk migogoro kama hiyo.

Mkuu kwa hiyo Chadema waliogopa kuntangaza Dr Slaa mapema kwa kuogopa kuwa atachafuliwa na CCM? Na hata kama ni hivyo Dr Slaa ndie atakuwa mgombea pekee wa Urais in future? Au wagombea wengine nao watakuwa na issues alizokuwa nazo Dr Slaa? Bado naona kuna umuhimu mkubwa kwa wapiga kura kumjua mgombea Urais mapema. Kumjua mgombea Urais miezi mitatu kabla ya uchaguzi ni muda mfupi both kwa huyo mgombea kujitangaza vya kutosha na kwa wapiga kura kumjua kiundani.

Kilichofanyika Dr. Slaa aliibiwa kura nyingi sana na ushahidi upo wazi kabisa isipokuwa chama kijifunze zaidi sababu kubwa zilizowafanya kushindwa mwaka 2010. Binafsi yangu Chadema wanashindwa sii kwa sababu ya kutokuwa na mbinu bali mfumo mzima wa uchaguzi toka katiba hadi usimamizi wake. Maadam vyombo vya kusimamia upigaji kura sii vyombo huru, wakuu wa mikoa, wilaya na Polisi ni wateule wa rais hamuwezi kushinda kura hata kama wananchi wote wamekichagua Chadema...Fanya mtakavyofanya bila katiba hii kubadilika kabla ya mwaka 2015 Chadema haiwezi kushinda...labda tutegemee mwaka 2015 kuwa mwaka wa machafuko nchini...Nimeyasema leo na nitayarudia mwaka 2015 - InshaAlaah tukijaliwa Uzima..

Kwa kuongezea tuu kama Chadema wanataka washinde itabidi walekeze kampeni zao kwenye grass root zaidi tena from now. Huku mijini watu wana maneno mengi tuu lakini huwa hawapigi kura. Unaona mtu kama Dr Slaa anaweka status fesibuku, comments kibao, lakini ni wangapi kati ya hao wanaocomment watampigia kura? Tena wengi wao inawezekana wanaishi abroad. Na wale watakaopiga kura, they always take into account their future interests as well. Tofauti na watu wa mijini, watu wa vijijini have got nothing material to worry about kama ikija system mpya.

Kama Chadema wanataka kuchukua uongozi wa hii nchi waache kujikita mijini. Inawabidi wakatifue vumbi huko vijijini. Pia itawabidi wabadilishe strategy. Hii mikutano ya hadhara haitawafikisha mbali.
 
Nakukumbuka tulijadili hili sana hapa JF wakati Dr alipoteuliwa kuwa mgombea Urais. It was too late na hakupata muda wa kijinadi. Hata kufanya uchaguzi 2013 halafu uchaguzi mkuu ni 2015, bado naona atakayechaguliwa atakuwa na muda mfupi sana wa kutandaza zege. Kwa nini wasifanye kama wanavyofanya in the West? Kwamba baada ya Uchaguzi mkuu, kama mgombea urais hakufanikiwa kushinda, then chama kinafanya uchaguzi immediately after the general election. Hapo atakuwa na at least miaka minne ya kujijenga na kuzunguka nchi kunadi sera za chama.

Mkuu EMT,

Nadhani unachanganya mambo. Dr. Slaa anaongelea uchaguzi wa ndani wa chama, yaani kuchagua viongozi kuanzia ngazi za matawi, kata, wilaya, mkoa na hatimaye taifa.

Wewe unaongelea uteuzi wa mgombea wa urais kupitia chama. Sina hakika kama Katiba ya Nchi inaruhusu kuteua mgombea wa urais miaka 4 kabla ya mwaka wa uchaguzi. Ndiyo maana Tume ya Uchaguzi kwa kufuata Sheria ya Uchaguzi huwa inatangaza ratiba ya kuchukua na kurudisha form za uteuzi. Pia ratiba hiyo huwa inatumika kuvi-guide vyama vya siasa kupanga ratiba za primaries na nominations za wagombea wa ngazi zote za udiwani, ubunge na urais. Kwa hiyo kuteua mgombea miaka 4 kabla inaweza kuwa ni kuvunja sheria. Pia kuna mabadiliko mengi ambayo yanaweza kutokea along the way, mfano, magonjwa, vifo na mengineyo.

Hata kama sheria inaruhusu kuteua mgombea miaka 4 au 3 kabla ya mwaka wa uchaguzi, inaweza kuwa rahisi sana kuwekewa pingamizi kwa kuwa hatakiwi kufanya mikutano ya hadhara ambayo ina taswira ya kampeni. Kwa hiyo mgombea huyo anatakiwa kuwa makini sana na kauli zake kwenye vyombo vya habari na hata kwenye mikutano ya hadhara, akiteleza kidogo tu inakuwa ni mwanya wa kuwapa nafasi ya kuweka pingamizi kwamba kuna mtu alianza kufanya kampeni kabla ya muda. Kama unakumbuka ile mikutano ya Dr. Slaa ya kusaka wadhamini na kujitangaza, CCM walitaka kuitumia kumuwekea pingamizi Dr. Slaa. Baadaye hiyo hoja sijui iliishia wapi, nadhani labda walikuwa wanajiamini, lakini baada ya matokeo ya 2010 na haya ya uchaguzi mdogo wa Igunga, CCM hawawezi ku-risk kutotumia mwanya wowote wa kuweka pingamizi dhidi ya mgombea wa upinzani ambaye anaonekana ni tishio kwao.

Mimi ninachofikiria ni kwamba kuteua mgombea urais mwaka wa uchaguzi siyo mbaya, na wanaweza kuteua hata mwezi March au mapema kidogo [iwapo sheria inaruhusu].

Marekani wanaingia kwenye uchaguzi mwakani, lakini mpaka sasa Republican bado hawajajua ni nani atapambana na Obama. Primaries zinaanza mwakani mwezi January, so may be mpaka mwezi March/April wanaweza kuwa wanajua ni nani atakuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Republican.
 
Mkuu kwa hiyo Chadema waliogopa kuntangaza Dr Slaa mapema kwa kuogopa kuwa atachafuliwa na CCM? Na hata kama ni hivyo Dr Slaa ndie atakuwa mgombea pekee wa Urais in future? Au wagombea wengine nao watakuwa na issues alizokuwa nazo Dr Slaa? Bado naona kuna umuhimu mkubwa kwa wapiga kura kumjua mgombea Urais mapema. Kumjua mgombea Urais miezi mitatu kabla ya uchaguzi ni muda mfupi both kwa huyo mgombea kujitangaza vya kutosha na kwa wapiga kura kumjua kiundani.
Hapana mimi nadhani ilikuwa mbinu na sii kuogopa na mbinu hiyo ilifanikiwa kutokana na historia za nyuma. Mrema na NCCR - chama cha Wachagga, Seif aliitwa Mpemba - CUF chama cha Waislaam, Salim mwarabu sana hafai na hizi tuhuma zote zilichukua muda kuweza kuzaa matunda yake. Kama kujulikana mapema mbona JK alijulikana mapema kuwa mgombea mwaka 2010 lakini hakuweza kutamba kama mwaka 2005 ambapo walichelewa..Lipumba na wengineo walijitokeza mapema kabisa mwka 2010 lakini mbona hawakufanya vizuri?.. swala ni chama kinasimamia maslahi ya wananchi wapiga kura... focus ni watu wenyewe unawapa ahadi gani, kuweza kutoa sera bora na mgombea mwenye kuaminiwa zaidi. Kumbuka Imani za watu TZ ktk kuaminiana ni chini ya asilimia 20,chama kikiweza kumpata mgombea anayeaminika kwa asilimia kubwa na chama kinatangaza wazi nia yake kwa dhati, wananchi watamchagua mtu huyo bila kujali muda ama kawafikia au laa!.

Kwa kuongezea tuu kama Chadema wanataka washinde itabidi walekeze kampeni zao kwenye grass root zaidi tena from now. Huku mijini watu wana maneno mengi tuu lakini huwa hawapigi kura. Unaona mtu kama Dr Slaa anaweka status fesibuku, comments kibao, lakini ni wangapi kati ya hao wanaocomment watampigia kura? Tena wengi wao inawezekana wanaishi abroad. Na wale watakaopiga kura, they always take into account their future interests as well. Tofauti na watu wa mijini, watu wa vijijini have got nothing material to worry about kama ikija system mpya.

Kama Chadema wanataka kuchukua uongozi wa hii nchi waache kujikita mijini. Inawabidi wakatifue vumbi huko vijijini. Pia itawabidi wabadilishe strategy. Hii mikutano ya hadhara haitawafikisha mbali.
Mimi I wouldn't worry much kupelekea wajumbe vijijini kwa sababu naamini mjini ndiko kwenye kura na watu wengi wapiga kura. CDM imeshinda uchaguzi uliopita kutokana na kujitika mijini amini maneno yangu kwani agenda ya UFISADI ilikuwa na mvuto zaidi mijini.. Watu wengi ktk population yetu wapo mijini, kuanzia makao makuu ya tarafa, wialaya na mikoa sema tu kwamba tulikosa mpiganaji wa WAKULIMA vijijini..

CCM walipokuja na kampeni za Kilimo kwanza, sii tu waliweza kujitangaza vijijini bali waliweza kufikisha ujumbe wao kwa wahusika na wananchi walijua CCM ndicho chama kitakachowaokoa wakulima. Kura za wakulima zikapelekwa CCM. JK hakuwa na haja ya kuwatembelea wana vijiiji lakini aliweza kuwarubuni kama alivyoweza ktk swala la mahakama ya kadhi..

Mwaka 2000 niliwahi kusema atakaye wafuata wanawake na kuwapa ahadi kutokana namfumo ulopita kuwasahau ktk keki ya Taifa ndiye atakuwa mshindi na JK alitumia mbinu hiyo zaidi ya wagombea wote akaondoka na asilimia 80% moslty zikitoka kwa wanawake.. Leo hii narudia tena kusema wananchi wa vijijini hawana haja ya kuiona sura ya Dr.Slaa wala mgombea yeyote bali mkakati wenye ujumbe unaweza kuwaondoa ktk umaskini WAKULIMA ndiye ataweza kushinda!..swala la ardhi na kilimo litakuwa ujumbe mkubwa kwao na hawa ndio watakuwa the independent and deciding voters wa uchaguzi ujao..Lakini tu itawezekana kama vyombo nilivyotaja hapo juu vitakuwa huru, uwazi bila upendeleo.
 
Mkuu EMT,

Nadhani unachanganya mambo. Dr. Slaa anaongelea uchaguzi wa ndani wa chama, yaani kuchagua viongozi kuanzia ngazi za matawi, kata, wilaya, mkoa na hatimaye taifa.

Wewe unaongelea uteuzi wa mgombea wa urais kupitia chama. Sina hakika kama Katiba ya Nchi inaruhusu kuteua mgombea wa urais miaka 4 kabla ya mwaka wa uchaguzi. Ndiyo maana Tume ya Uchaguzi kwa kufuata Sheria ya Uchaguzi huwa inatangaza ratiba ya kuchukua na kurudisha form za uteuzi. Pia ratiba hiyo huwa inatumika kuvi-guide vyama vya siasa kupanga ratiba za primaries na nominations za wagombea wa ngazi zote za udiwani, ubunge na urais. Kwa hiyo kuteua mgombea miaka 4 kabla inaweza kuwa ni kuvunja sheria. Pia kuna mabadiliko mengi ambayo yanaweza kutokea along the way, mfano, magonjwa, vifo na mengineyo.

Hata kama sheria inaruhusu kuteua mgombea miaka 4 au 3 kabla ya mwaka wa uchaguzi, inaweza kuwa rahisi sana kuwekewa pingamizi kwa kuwa hatakiwi kufanya mikutano ya hadhara ambayo ina taswira ya kampeni. Kwa hiyo mgombea huyo anatakiwa kuwa makini sana na kauli zake kwenye vyombo vya habari na hata kwenye mikutano ya hadhara, akiteleza kidogo tu inakuwa ni mwanya wa kuwapa nafasi ya kuweka pingamizi kwamba kuna mtu alianza kufanya kampeni kabla ya muda. Kama unakumbuka ile mikutano ya Dr. Slaa ya kusaka wadhamini na kujitangaza, CCM walitaka kuitumia kumuwekea pingamizi Dr. Slaa. Baadaye hiyo hoja sijui iliishia wapi, nadhani labda walikuwa wanajiamini, lakini baada ya matokeo ya 2010 na haya ya uchaguzi mdogo wa Igunga, CCM hawawezi ku-risk kutotumia mwanya wowote wa kuweka pingamizi dhidi ya mgombea wa upinzani ambaye anaonekana ni tishio kwao.

Mimi ninachofikiria ni kwamba kuteua mgombea urais mwaka wa uchaguzi siyo mbaya, na wanaweza kuteua hata mwezi March au mapema kidogo [iwapo sheria inaruhusu].

Marekani wanaingia kwenye uchaguzi mwakani, lakini mpaka sasa Republican bado hawajajua ni nani atapambana na Obama. Primaries zinaanza mwakani mwezi January, so may be mpaka mwezi March/April wanaweza kuwa wanajua ni nani atakuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Republican.

Mkuu sikuwa na maana hiyo. Nilikuwa na maana ya kumuandaa mtu kwa ajili ya kugombea urais later. Japokuwa anakuwa hajatangazwa official kama mgombea lakini hata mpiga kura wa kaiwaida akimwangalia anaona kuwa is the likely person to stand for election.

Kwa mfano kwenye uchaguzi uliopita many people were taken by surprise pale Dr Slaa alivyotangazwa kuwa ndiye atakuwa mgombea. Watu wamezoea kuwa mwenyekiti wa chama ndie anayekuwa mgombea. Ile ya kwenda kuchukua fomu za kugombea in formality tuu but mgombea urais anakuwa tayari ameshajulikana.

Kuhusu kampeni sina maana ya kampeni za uchaguzi mkuu. Bali chama kujicemnet zaidi kwa watu na sio tuu kusubiri mpaka vyakati za uchaguzi. Tokea uchaguzi wa Igunga umalizike nani karudi Igunga? Hii mikutano ya hadhara waliyokuwa wanafanya hivi karibuni haikuwa ya uchaguzi but they need to move more than that.
 
Hiyo ni mipango ya kwenye makaratasi,, utekelezaji wake ni sehemu ingine tena, ina changamoto nyingi na mapito mengi, je? Ukomavu na uvumilivu wenu utawafikisha 2015 bila kupigana vikumbo ninyi kwa ninyi?.. mna lengo zuri lakini jipangeni kitaifa acheni siasa za kulipua mabomu waelezeni wananchi niya na madhumuni ya kutaka kuwaongoza kujenga kuheshimiana na kuaminiana ndani ya chama chenu na vyama vingine , serikari na vyombo vyake.
Hata Operation Sangara waliibeza hivi hivi matokeo ya operation hiyo ndiyo yanawahangisha leo hii.
 
Mkuu kwa hiyo Chadema waliogopa kuntangaza Dr Slaa mapema kwa kuogopa kuwa atachafuliwa na CCM? Na hata kama ni hivyo Dr Slaa ndie atakuwa mgombea pekee wa Urais in future? Au wagombea wengine nao watakuwa na issues alizokuwa nazo Dr Slaa? Bado naona kuna umuhimu mkubwa kwa wapiga kura kumjua mgombea Urais mapema. Kumjua mgombea Urais miezi mitatu kabla ya uchaguzi ni muda mfupi both kwa huyo mgombea kujitangaza vya kutosha na kwa wapiga kura kumjua kiundani.

Kwa kuongezea tuu kama Chadema wanataka washinde itabidi walekeze kampeni zao kwenye grass root zaidi tena from now. Huku mijini watu wana maneno mengi tuu lakini huwa hawapigi kura. Unaona mtu kama Dr Slaa anaweka status fesibuku, comments kibao, lakini ni wangapi kati ya hao wanaocomment watampigia kura? Tena wengi wao inawezekana wanaishi abroad. Na wale watakaopiga kura, they always take into account their future interests as well. Tofauti na watu wa mijini, watu wa vijijini have got nothing material to worry about kama ikija system mpya.

Kama Chadema wanataka kuchukua uongozi wa hii nchi waache kujikita mijini. Inawabidi wakatifue vumbi huko vijijini. Pia itawabidi wabadilishe strategy. Hii mikutano ya hadhara haitawafikisha mbali.
EMT
Kwenye bold, nakubaliana na wewe kuwa kuna umuhimu wa wapiga kura kumjua mgombea mapema ila nafikiri kinachotakiwa si jina bali ni utendaji na record ya mgombea, sasa basi hata leo mimi nikitangazwa mgombea nina kitu gani cha kuonyesha, je nionyeshe nilichofanya mwaka jana? au nianze kutafuta record ya kuonyesha wakati wa kampeni 2015. Nafikiri kama mimi ni mtendaji mzuri katika jamii hata nikitangazwa mwezi mmoja kabla jamii itanitambua, ila si rule out wazo la kumgombea kujulikana mapema.

Nakubaliana na wewe pia kuhusu watu wa vijijini that they have nothing to worry about or to lose ukilinganisha na watu wa mijini, sababu kubwa ni kuwa watu wengi wa vijijini wamejiajiri tofauti na wa mijini wanaotegemea mishahara mingi inayotoka kwa viongozi wa kisiasa, kwa hiyo ndio maana wanakuwa reluctant sana kujihusisha na siasa. Lakini mambo yanakwenda yanabadilika ukiangalia karibu majiji na miji yote iko chini ya upinzani.

Mwisho umesema inabidi CDM wabadili strategy ki vipi wakati mikutano ya hadhara ndiyo njia rahisi ya kuhamasisha wananchi.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Kwa hiyo muda wa kumchagua mgombea urais upo pale pale? Three months or so kabla ya uchaguzi?
Mgombea urais?..... si ameshachaguliwa? au hujui hilo?

quote_icon.png
By Mikael P Aweda
Kwa kuwa umejiita mwanachadema ni vizuri nikukumbushe kwamba umekwenda kinyume na kanuni za Chadema. Huwezi kutumia maneno hayo kwa kiongozi wa juu yako. Ni sawa na kuwatukana wajumbe wote wa kamati kuu, Baraza kuu na Mkutano mkuu waliosema anayefaa kuwa mgombea wa Chadema 2015 ni Dr Slaa na siyo Ntogwisangu.

Na kama wewe ni mwanachama na hujui kanuni ndogo kama hiyo, basi una tatizo. Ukitoka safari nitafute tuelekezane vizuri maana hiyo mmoja ya majukumu yangu wala hujanisumbua.

Pili, kama Dr Slaa hukumridhia wewe, uliandika barua yo yote ya malalamiko kama mwanchadema? Kama sivyo kulikoni kuja na mawazo hayo jf? ''
 
Mgombea urais?..... si ameshachaguliwa? au hujui hilo?

Sitaki kuamini kama kweli hukuelwe sentensi ya Aweda kuwa alikuwa ana refer kikao kilichopita na uchaguzi wa 2010.

quote_icon.png
By Mikael P Aweda
Kwa kuwa umejiita mwanachadema ni vizuri nikukumbushe kwamba umekwenda kinyume na kanuni za Chadema. Huwezi kutumia maneno hayo kwa kiongozi wa juu yako. Ni sawa na kuwatukana wajumbe wote wa kamati kuu, Baraza kuu na Mkutano mkuu waliosema anayefaa kuwa mgombea wa Chadema 2015 ni Dr Slaa na siyo Ntogwisangu.
 
Sitaki kuamini kama kweli hukuelwe sentensi ya Aweda kuwa alikuwa ana refer kikao kilichopita na uchaguzi wa 2010.
Nilivyoona mimi ni 2015, sasa kama wewe ndiye Aweda Poa!!, rekebisha basi.
 
Ni kweli mipango ni mizuri lakini tunataka utekelezaji zaidi na nafikili ni muhimu CDM Wangekuwa na mpango kazi mkakati kwa kila tukio na ratiba yake.Kwa sababu tumebakiwa na miaka mitatu tu ukiondoa mwaka wa uchaguzi.Pia nafikili kuna umuhimu wa kuwa na mpango kazi wanamna ya kushika majiji mengine kama DSM,MBEYA,ARUSHA NA TANGA. Na hii ifanyike kwa kuandaa wasomi na watu wengine wanaokubalika kugombea nafasi za udiwani. Katika DSM, MBEYA NA ARUSHA Hakuna ugumu wa kuyachukua majiji hayo kabisa kama wakijipanga vizuri labda Tanga ndiyo naona kutakuwa na kazi ngumu kwani chama cha CUF Kina nguvu zaidi.Katika Dar es Salaam,maeneo ya Temeke ndiyo kidogo yana ugumu.Chonde chonde CDM kianzishwe kitengo cha kupanga safu ya madiwani ili kuchukua majiji na Halimsahauri mbalimbali nchini.Kitengo hicho kifanye kazi ya kutafuta ,kuchagua,na kuhamasisha watu wenye sifa na kuermark maeneo ya kata mbalimbali za kugombea watu hao kwa kuangalia wanavyokubalika.Hili ni zoezi gumu linalotakiwa kuwa limeanza sasa.Pia ni muhimu CDM ikajua idadi ya wanachama wake hai Tazania nzima hii nayo itasaidia kujipanga vizuri.
 
Back
Top Bottom