CHADEMA Yaanikwa Bungeni Jioni Hii!

CHADEMA Yaanikwa Bungeni Jioni Hii!

Waziri wa Kilimo Mhandisi Chiza ameichambua HOTUBA ya waziri kilimo wa CHADEMA kuwa haina viwango ilijikita kutoa lawama badala ya majibu muafaka.

Kwa kweli ukifuatilia hotuba ya Waziri Chiza utagundua CCM ipo makini kutatua matatizo ya kilimo wakati CHADEMA wamebaki kupiga kelele kwa kutumia mawaziri vivuli wasio na viwango
We mpuuzi kweli! Taarifa za chakula zinasema kuwa mikoa 20 inakabiliwa na njaa kali Tanzania, nawe unaendekeza ujinga huu wa waziri Chiza juu ya kutatua matatizo ya kilimo. Waziri Anataka kutatua matatizo ya kilimo baada ya wananchi wote kufa kwanza kwa njaa? Mbona hukujiuliza kuwa mpango wa serikali wa kilimo kwanza umeleta faida gani Tanzania wakati watu wanakabiliwa na njaa kuu kiasi hicho? Tanzania haitaki bla bla, inataka vitendo.. upulika veve!!
 
Kama ndo hivi ccm lazima itafilisika tu. Kama uzi wa aina hii nao mtu analipwa! Mna bahati kwa kuwa mnalipwa pesa zetu za kodi.
 
Hawa Wabunge wa CDM walifukuzwa Bungeni na Spika Makinda kwa siku tano. Ni vema wawaeleze hasa wapiga kura katika majimbo yao, kukosekana haki hata Bungeni. Kauli mbiu ya CDM "Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke"!!!!!!!!!!!!!!

Sidhani kama wananchi wanahitaji kuhubiriwa kwenye mikutano wakati kinachoendelea bungeni kinaonyeshwa live.
 
Kazi ya Chadema ni kukosoa siyo kupigia makofi serikali ndo maana ya vyama vya ushindani/upinzani duniani kote. Kazi ya Serikali ni kuwaletea wananchi maendeleo kwa kutumia kodi za watanzania wote , wakiwepo wanachadema, na siyo kwa kutumia mishara yao. kukoselewa siyo kulaumiwa.

Na unapokosoa huna budi kutoa solution sio uwe unakosoa tuuuuuuuu kama "wifi"
 
Nadhani watanzania wengi hatuna akili au upeo wa kuona au kufanya kitu kwa ajili ya maisha ya watoto wetu au wajukuu......ndio maana inakuwa rahisi kwetu kuhongwa kwa vitu vidogo vidogo.
 
Sidhani kama wananchi wanahitaji kuhubiriwa kwenye mikutano wakati kinachoendelea bungeni kinaonyeshwa live.

Mheshimiwa Maboso, ni wananchi wachache sana wanaona 'live' shughuli za Bunge zikiendelea. Hasa katika majimbo ya Wabunge waliosimamishwa kwa siku tano na Spika Makinda, hakuna wananchi wengi wenye runinga. Hata redio wengi hawana.

Nikiwa Muasisi na Mwenyekiti Taifa mstaafu wa Chadema nawahimiza hawa Wabunge kuendelea kuwaelimisha wananchi ili watambue jinsi haki na demokrasia vinavyoathiriwa na misimamo ya Chama tawala na Serikali, wakiungwa mkono na Spika Makinda.

Narudia kauli mbiu ya Chama chetu: Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke. Waheshimiwa Wabunge wetu :Uzi ni Huo Huo !!!!!!!!
 
Unaelewa ulichokiandika? huo umakini upo wapi? unapima kwa vigezo gani? hadi sasa kilimo cha umwagiliaji tanzania ni asilimia 1% ya fursa za umwagiliaji zilizopo, je huo ndiyo umakini au unjifurahisha tu? kwangu mimi kauli za wanasiasa kwenye sector kama ya kilimo ni mbinu tu ya kupata kura.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Chiza ameichambua HOTUBA ya waziri kilimo wa CHADEMA kuwa haina viwango ilijikita kutoa lawama badala ya majibu muafaka.

Kwa kweli ukifuatilia hotuba ya Waziri Chiza utagundua CCM ipo makini kutatua matatizo ya kilimo wakati CHADEMA wamebaki kupiga kelele kwa kutumia mawaziri vivuli wasio na viwango
 
mI LABDA NIISOME HOTUBA YENYEWE.... MAANA KAMA WAZIRI ANALALAMIKA IMEJAA LAWAMA ANATAKA ISIFIWE BASI SERIKALI YA CCM INA MACHIZI... HIVI KUNA NINI CHA KUSIFIWA KWA WIZARA YA KILIMO JAMANI...
KILA MKULIMA ANALALAMIKA MAMBO HAYAENDI SASA WANATAKA WASIFIWE KWA LIPI?
HAWA WATU NI WAPUUZI KABISA BADO WANAAMINI WAKULIMA NI WALE WA ENZI ZILE TU AMBAO HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA, AMBAO WAKIPELEKEWA MBOLEA KILO 1 WANAHISI WAMEPWEA MSAADA????
CCM NA SERIKALI YENU ... HEBU RUDINI KWA WANANCHI MUWASOME KWANZA MASWALA YA KU COPY NA KU PASTE KILA MWAKA YATAWAPONZA.... HAMNA LA KUSIFIWA HATA MOJA NA NYIE WENYEWE MNAJUA... TUTAWAFUATA HUKO BUNGENI NA PIS...TO MSITULETEE MCHEZO
 
Tatizo la mawaziri na ccm wanazani kukosolewa ni upinzani, sasa kama bajeti haikosolewi unazani imeenda bungeni kujadiliwa ili iweje wakati ingekuwa inapita tuu, hata wabunge wa ccm wana wajibu wa kuikosoa bajeti na nazani kuna tofauti ya lawama na kukosoa....... makampuni binafsi yanawalipa wataalam wawafundishe watumishi wao kukubali kukosolewa na ukosoaji ulio na manufaa na ziko training nying za mrejesho na jinsi ya kuutoa
 
Waziri wa Kilimo Mhandisi Chiza ameichambua HOTUBA ya waziri kilimo wa CHADEMA kuwa haina viwango ilijikita kutoa lawama badala ya majibu muafaka.

Kwa kweli ukifuatilia hotuba ya Waziri Chiza utagundua CCM ipo makini kutatua matatizo ya kilimo wakati CHADEMA wamebaki kupiga kelele kwa kutumia mawaziri vivuli wasio na viwango

wewe kwa ufinyu wa akili yako unaona serikali ya chama chako ccm iko makini,kama ndivyo je malalamiko ya wabunge wa ccm hiyohiyo kutoka nchi nzima yanatokana na nini kama sio uduni wa huduma mbovu zaa serikali.

mfano halisi ni kuendelea kudumaa kwa maisha ya mwananchi wa kijijini yanavyoendelea kuwa magumu kila uchao, na kusababisha wakimbizi wa ndani ya nchi waliojazana mjini wakikimbia shida vijijini.

wewe endelea na ajira yako mpya humu ndani ya jukwaa ambayo umeajiriwa hivi majuzi na mwigulu,ila elewa shda zako hazitaisha kwa kuajiriwa ili kuuhadaa umma./
 
Waziri wa Kilimo Mhandisi Chiza ameichambua HOTUBA ya waziri kilimo wa CHADEMA kuwa haina viwango ilijikita kutoa lawama badala ya majibu muafaka.

Kwa kweli ukifuatilia hotuba ya Waziri Chiza utagundua CCM ipo makini kutatua matatizo ya kilimo wakati CHADEMA wamebaki kupiga kelele kwa kutumia mawaziri vivuli wasio na viwango

Inashangaza sana kila bajeti mbadala wana wa magamba wanaponda,labda ni ulize swali walitaka wapinzani wasemeje?wakirudi kwa wananchi kuishitaki serikali mnalalamika hata hivi sasa nawe pia una lalamika,rais naye ana lalamika labda mlitaka CDM waingie msituni ndiyo mjue wako serious!

Matatizo yanayo pigiwa kelele ni matatizo ya Watanzania wote hakuna wapinzani wala CCM,isipokuwa unafiki ndiyo uliowagubika makanjanja wa madaraka na kutaka Watanzania wafumbi macho.Hakuna asiyejua kuhusiana na voucher za pembejeo hususani mbolea,makada wa chama ambao ni wakuu wa wilaya ndiyo mabingwa waliokumbwa na kashfa ya kufanya biashara hiyo leo mkiambiwa mnapiga kelele,piga keleleeeeeeeeeeeeeee lakini mabadiliko yapo mlangoni kwako.
 
Ila ccm mnahangaika lol!! mmechuja jamani kwanini hamtaki kukubali matokeo? wabeze kila kitu lakini sisi ndio waamuzi wa mwisho.
 
Bahati nzuri huyu Mafilili tumeshamtambua ni kilaza na mada zake ni -----. Magamba mtimizieni ujira wake (Chakula cha mchana (3,000) na buku mbili viroba aende home kesho aje kuchangia JF. Kwenye msafara wa Mamba hata kenge wapo: Kwani ni lazima kuchangia kwenye JF kama huna data?
 
Back
Top Bottom