CHADEMA wazuru Kaburi la Baba wa Taifa Butiama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wazuru Kaburi la Baba wa Taifa Butiama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Regia Mtema, Feb 27, 2011.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Baada ya kuingia Musoma na kufanikiwa kufanya maandamano kwa amani na utulivu mkubwa leo vikosi vitatembelea Wilaya za Mkoa huu. Lakini kabla ya kwenda kwenye wilaya, Viongozi wote tukiongozwa na Kamanda Mbowe tutaelekea kuzuru kaburi la baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere na kuweka mashada ya maua.

  Vikosi leo vitaelekea Tarime, Rorya, Bunda, Serengeti, Mwibara na Musoma Vijijini.

  Hauna Kulala Mpaka Kieleweke.

  Aluta Continua

  Kutoka Musoma

  Regia E Mtema
  Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
   
 2. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,978
  Likes Received: 6,621
  Trophy Points: 280
  nakutakieni kazi njema.Mungu awasaidie watanzania wote kutambua haki zao kupitia wanaharakati wa CDM.
   
 3. m

  mohermes Senior Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  peopleeeeeeeeeees Poweeeeer
   
 4. m

  mgalisha Member

  #4
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Safi sana nimeipenda fateni Baraka za Baba wa Taifa
   
 5. Ole

  Ole JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2011
  Joined: Dec 16, 2006
  Messages: 751
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Good work CDM, CCM wamewakumbatia mafisadi wataokwenda nao kuzimu.
   
 6. U

  Uswe JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mi CDM lakini pia born again christian, kwamba kuna baraka makubirini, i don't know
   
 7. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Dada Regia tunawategemea sana Cdm ktk kulikomboa taifa ili. Tuizunguke tanzania mpaka kieleweke. Msisahau kagera pita bukoba mjini,kamachumu,buganguzi ,nshamba,muleba,karagwe na biaharamulo,kuna wanaharakati wa kutosha. Pia dar msiiweke mbali,liunganishe taifa tupate mabadiliko. Msisahau kubeba kadi za chama,maana huwa nashindwa kuelewa ambapo watu wanasaka kadi za cdm kama almasi wakati za chama tawala zipo hadi majalalani! Ongezeni na panua chama ili siku ya ukombozi wa mlalahoi tuwe wengi. Si kuwa na wapambe wengi na wanachama wachache. Pia iunganishe pemba na ugunja katika 'gridi' ya taifa! Fikisha salam zangu kwa mama maria Nyerere. Pia ukiweka shahada kwenye kaburi la mwalimu,weka na sala yako kuliombea taifa auheni ya ugumu wa maisha,mifumuko bei,maradhi,na ufisadi. Tunashukuru kwa taarifa yako,"...nendeni kwa amani.."
   
 8. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Endeleeni.
  Mi nasema maandamano haya yaendelee kwa amani siku ambayo polisi watatumwa kuja kupiga watu, mapinduzi yataanzia hapo tuendelee kuungana
   
 9. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dada Regia naomba sana mfanye ziara kanda ya kati bado wamelala hasa Singida na Dodoma mwaka Jana wakati kampeni nilikuwa Singida kule bado kabisa wamefungwa macho upinzani hauna nguvu sana isipokuwa tu kwa Tundu Lissu.
  Niliona Chadema wakichekwa.
   
 10. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Toka amekufa ndo leo chadema inaenda?
  12 years?oh my God

  1999 chadema haikuwepo?
  why now?

  Asume umefiwa afu mtu anakuja kuhani after 12 years lol
  Au ndo kutembelea museum?

  Anyway,all the best!
   
 11. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  viva cdm !!! msisahau kutembelea mikoa ya kusini coz huko ndo bado wa2 hawajaelewa umuhimu wa mabadiliko!!!
   
 12. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mpaka kieleweke!
   
 13. I

  Inkognito Member

  #13
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tupo pamoja
   
 14. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  mkuu,nategemea una tv au redio kwako,iweje uwaze eti cdm hawajawi kwenda Musoma,wafuatiliaji makini watakushangaa!
   
 15. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tunawatakia mafanikio mema, maana nikiona hivi najua chama kiko serious si vile vinavyoishia Ubungo mataa na kuanza kulalamika.
   
 16. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,197
  Trophy Points: 280
  Nafikiri Speaker unaumia sana kuona CDM inafanikiwa kwenye maandamano ila unajikaza kisabuni kujifanya unayapongeza (anyway all the best) msemo huu ni wa mtu aliyekata tamaa. Jana ukazua eti mbona huwaona Zitto na Mnyika ukajibiwa kazi waliyopangiwa leo unazua jingine eti Chadema haijatembelea kaburi kwa miaka 12 unauhakika?
   
 17. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mungu awatangulie wote na kuwabariki sana
   
 18. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,197
  Trophy Points: 280
  Ajabu ina maana hata Mbunge wa Musoma Mjini Vincent Nyerere hajawahi kutembelea kaburi vichwa vingine basi tu mradi aonekane amepost.
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  inawezekana huku bahatika kufatilia vyombo vya habari...Kwa tamaduni zetu mfano tunakawaida ya kutembelea makaburi ya wapendwa wetu...naamini hata wewe huwa huwa unafanya hivyo kila unapopata nafsi...
   
 20. V

  Victim Member

  #20
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  You bring tears to my old ,tired eyes.

  God bless you all.
   
Loading...