CHADEMA wazuru Kaburi la Baba wa Taifa Butiama

CHADEMA wazuru Kaburi la Baba wa Taifa Butiama

kweli kabisa.....tunaendelea kuandamana.cku wakipiga mtu tu...2naanzia hapo mpaka kinaelewekaaaaaaaaaaa
 
Endeleeni.
Mi nasema maandamano haya yaendelee kwa amani siku ambayo polisi watatumwa kuja kupiga watu, mapinduzi yataanzia hapo tuendelee kuungana
kweli yaani wasirogwe kupiga/kuua m2,ikitokea tu...ndo itakuwa petroli ya kung`olea mafisadi...2taandamana mpaka wang`oke wote
 
Msiwasikilize vilaza wa CCM wanakosoa kila kitu. CDM mshikamano ya daima songa mbele usirudi wala kugeuka nyuma utakuwa jiwe la chumvi.
 
mkuu,nategemea una tv au redio kwako,iweje uwaze eti cdm hawajawi kwenda Musoma,wafuatiliaji makini watakushangaa!

Sijasema hawajawahi kwenda musoma,...
MKoa wa mara una wilaya 6,kati ya hizo kuna musoma mjini na musoma vijijini!

Sijawahi kusikia chadema wameenda musoma vijijini,na tatizo langu sio wao kwenda musoma vijijini elewa nacho ongea

Wamesema wanaenda butiama (musoma vijijini)....."kuweka mashada kwenye kaburi la nyerere"
Swali ni kwamba,....na kama ulivo sema hapo juu kwamba (wamekuwa wakienda musoma mara nyingi) kwanini saivi (miaka 12 baada ya nyerere kufa ndo wakaweke shada kaburini?)
 
Nafikiri Speaker unaumia sana kuona CDM inafanikiwa kwenye maandamano ila unajikaza kisabuni kujifanya unayapongeza (anyway all the best) msemo huu ni wa mtu aliyekata tamaa. Jana ukazua eti mbona huwaona Zitto na Mnyika ukajibiwa kazi waliyopangiwa leo unazua jingine eti Chadema haijatembelea kaburi kwa miaka 12 unauhakika?

Watu watasikiaje wasipo ambiwa?
Wataamini vipi wasipo oneshwa?

Leo tumeambiwa wanaenda butiama,.......(tumepata taarifa) next year wakienda tutakua na kumbu kumbu mwaka jana walienda!

Haya,leo hii,nambie walienda lini butiama mara ya mwisho?

Swali ni je,kwanini baada ya miaka 12 leo ndo wanaenda?
Usijibu tu bora umejibu,na utaonekana mwenye "hekima" kama utapotezea swali langu
 
inawezekana huku bahatika kufatilia vyombo vya habari...Kwa tamaduni zetu mfano tunakawaida ya kutembelea makaburi ya wapendwa wetu...naamini hata wewe huwa huwa unafanya hivyo kila unapopata nafsi...

Okey,atleast unajibu swali wewe!

Lakini kwanini baada ya miaka 12?
Ilishindikana nini kwa chadema kwenda 2000,2001,.....2010 hadi leo au walikuwa hawajui kama nyerere amekufa?
 
Mi CDM lakini pia born again christian, kwamba kuna baraka makubirini, i don't know

Kuabudu sanamu,kama unaamini kwenda kaburini unapata baraka basi uko mbali sana na Mungu!
Bora ume waambia na wewe
 
Wakuu,

Baada ya kuingia Musoma na kufanikiwa kufanya maandamano kwa amani na utulivu mkubwa leo vikosi vitatembelea Wilaya za Mkoa huu. Lakini kabla ya kwenda kwenye wilaya, Viongozi wote tukiongozwa na Kamanda Mbowe tutaelekea kuzuru kaburi la baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere na kuweka mashada ya maua.

Vikosi leo vitaelekea Tarime, Rorya, Bunda, Serengeti, Mwibara na Musoma Vijijini.

Hauna Kulala Mpaka Kieleweke.

Aluta Continua

Kutoka Musoma

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira


ASANTE REGIA KWA hii update bado tuko pamoja na nyie makamanda wetu, daima tutakuwa pamoja, mungu awabarikie na awatanguliwe.
 
Watu watasikiaje wasipo ambiwa?
Wataamini vipi wasipo oneshwa?

Leo tumeambiwa wanaenda butiama,.......(tumepata taarifa) next year wakienda tutakua na kumbu kumbu mwaka jana walienda!

Haya,leo hii,nambie walienda lini butiama mara ya mwisho?

Swali ni je,kwanini baada ya miaka 12 leo ndo wanaenda?
Usijibu tu bora umejibu,na utaonekana mwenye "hekima" kama utapotezea swali langu

Mbowe atembelea kaburi la Nyerere

Published 09/20/2005

MGOMBEA urais kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, pamoja na mkewe, Dkt. Liliah Mbowe, wametembelea na kuweka shada la maua pamoja na kuomba dua kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Butiama.

Bw. Mbowe ambaye yupo Kanda ya Ziwa kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu, jana alipita kumsalimia mjane wa Mwalimu, Mama Maria Nyerere.

Alimkaribisha nyumbani, Mama Maria alimshukuru Bw. Mbowe kwa kupita na kumjulia hali na kumtaka yeye pamoja na wagombea wengine kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani.

"Nimerudi juzi nilikuwa Dar es Salaam kwa ajili ya kuombea Uchaguzi, ninawaomba na ninyi kama mnavyotamka basi hakikisheni uchaguzi unakuwa wa amani," alisema Mama Maria.

Katika hatua hiyo, Mama Maria alimuuliza Bw. Mbowe iwapo chumba pamoja na samani walizopewa na Mzee Mbowe kama bado vipo ambapo Bw. Mbowe alisema bado vipo na anakaribishwa sana .

Akizungumzia mtazamo wa Mwalimu kama angekuwepo, Mama Maria alisema huenda angekuwa akisisitiza zaidi juu ya Tanzania kujenga zaidi katika amani na utulivu.

Naye Bw. Mbowe alimshukuru Mama Maria pamoja na familia yake kwa kuwapokea vizuri.

"Ndugu zangu hapa mimi ni nyumbani kabisa si kwamba nimekuja kwa ajili ya mambo ya kisiasa," alisema.

Hii habari ya mbowe mwenyekiti wa chadema kutembelea kaburi la nyerere pia ilitolewa kwenye gazeti la majira la jumanne september 20, 2005(ISSN 0856-5086 No. 4276)
 
R.I.P. Baba wa Taifa,
laiti kama ungerudi leo ukawaona MABEPARI wanavyotumia jina lako kuomba uongozi wa Taifa letu!
 
Mbowe atembelea kaburi la Nyerere

Hii habari ya mbowe mwenyekiti wa chadema kutembelea kaburi la nyerere pia ilitolewa kwenye gazeti la majira la jumanne september 20, 2005(ISSN 0856-5086 No. 4276)

Hayo ndo majibu,mtu akitaka kujua kitu ajibiwe kama alivo uliza sio wengine wanakuja na matusi yao!

Asante sana mkuu,you are a great thinker!
 
Wakuu,

Baada ya kuingia Musoma na kufanikiwa kufanya maandamano kwa amani na utulivu mkubwa leo vikosi vitatembelea Wilaya za Mkoa huu. Lakini kabla ya kwenda kwenye wilaya, Viongozi wote tukiongozwa na Kamanda Mbowe tutaelekea kuzuru kaburi la baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere na kuweka mashada ya maua.

Vikosi leo vitaelekea Tarime, Rorya, Bunda, Serengeti, Mwibara na Musoma Vijijini.

Hauna Kulala Mpaka Kieleweke.

Aluta Continua

Kutoka Musoma

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

hiyo habari njema sana, huu mwaka hatutaki mzaha wakati vyama vingine vinapoteza muda kutetea maslahi ya mafisadi sisi tusonge mbele na kutetea wananchi.


Peoples power!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Okey,atleast unajibu swali wewe!

Lakini kwanini baada ya miaka 12?
Ilishindikana nini kwa chadema kwenda 2000,2001,.....2010 hadi leo au walikuwa hawajui kama nyerere amekufa?
Mimekuuliza una uhakika au unaandika tu almradi umepost jishughulishe usisubiri kutafuniwa kila kitu.
 
Kila baraka ziwafikie kwa jitihada zenu. Hila baada ya kwenda kwenye hilo kaburi mrudi na sera sasa either mwalimu awaambie au muanze kutoa sera mbadala za maendeleo.

Watanzania wamesha choka na maisha magumu, serikali ya CCM ina sera mbovu ziliochanganywa na utapeli wa hali ya juu. Yes utapeli aupendwi na wote isipokua mbinu pia za maendeleo hamna. Its about time sasa Chadema kuacha kutunadia mbuzi ndani ya gunia how about policy for once. Si ndio siasa zenyewe hizo kuja na sera mbadala za maendeleo au?

Maana huko kaburini sijui mtarudi na nini cha kutuambia kuhusu mipango ya maendeleo zaidi ya publicity stunt nyingine na uzalendo wa madoido tu. Its about you guys talked real politics now and enough of this unproductive stunts.
 
Ajabu ina maana hata Mbunge wa Musoma Mjini Vincent Nyerere hajawahi kutembelea kaburi vichwa vingine basi tu mradi aonekane amepost.

Thanks Mpwa for the good signature!!! Acha kuhangaika na pro-Kikwete.
 
Big up kwa sana... Mkizunguka mwaka huu mikoani, then na 2013 mkafanya tena... tanzania yooote ni ya cdm... eeh Mungu uwatangulie
 
Kuabudu sanamu,kama unaamini kwenda kaburini unapata baraka basi uko mbali sana na Mungu!
Bora ume waambia na wewe

Mkuu inaonekana wao kwenda leo inakusumbua sana?!!! Wewe ulitaka frequency iweje?
 
Hayo ndo majibu,mtu akitaka kujua kitu ajibiwe kama alivo uliza sio wengine wanakuja na matusi yao!

Asante sana mkuu,you are a great thinker!

Haya yalikuwa wazi siku nyingi mkuu!!! Tatizo ni jinsi ulivyouliza, kishari...
Au umeanza kufuatilia siasa juzi nini!!!!
 
Back
Top Bottom