Hakuna kijiji cha Likusanguse Namtumbo hii habari inaonekana ni ya kutunga na tukio ni la kutunga.Mtake msitake jimbo la Namtumbo ni CCM 100% (Kamanda Vita Kawawa).Ni aibu kushabikia tukio la kubuni kwenye mtandao.Kama lengo ni kumpitisha mgombea wa CDM badala ya wa CUF kwa staili hiyo mtaumbuka!Mgombea wa upinzani Namtumbo muda wote ni mgombea wa CUF na si CDM
Kijana acha upotoshaji, wewe sio mkazi wa huku na ndo maana hata hujui kuwa wanaccm wenyewe hawahitaji hata kumsikia huyo unayempigia debe. Ungekuwepo Namtumbo ungejua jinsi upepo wa kisiasa unavyovuma. Kama hujafanya utafiti huna haki ya kuzungumza, usijifungie kwenye box kijana toka nenda Namtumbo utayapata haya. Nenda Kata ya Magazine kuna kijiji kinaitwa Likusanguse (Wakilitaja wenyewe unaweza utafkiri wanasema Lingusenguse ila kiufasaha ni Kijiji cha Likusanguse). Niliyoandika sijasimuliwa nimeshuhudia mwenyewe. Kama Unakifahamu kijiji hicho uliza baada ya kikosi cha makamanda kufika hapo nini kimetokea kwa mtia nia mwingine wa CCM aliyeenda na rushwa baada ya CDM kutoa elimu na kuwatia ujasiri wananchi wa Likusanguse utaelezwa kuwa waliwavurumushia mawe watoa rushwa wa ccm hadi wakapoteana. Ni mpela mpela mpaka kieleweke.
Kuhusu mgumbea wa chama gani anapaswa kusimama mwaka huu via UKAWA. Ukawa waliwekeana vigezo, hakuna kigezo cha
"nani huwa anasimamisha mbunge katika jimbo fulani" , fahamu kuwa hakuna mwenye hati miliki ya Jimbo, tunaangalia performance ya chama fulani katika jimbo fulani. Kweli CUF ipo ila CDM ipo zaidi ya CUF. Matokeo ya uchaguzi mdogo wa mwaka jana yanathibitisha hili. CUF katika Jimbo Zima wana vitongoji 10 tu, wakati CDM wana vijiji 4 kati ya 71, vitongoji 37 na wajumbe 77. Zaidi ya ushindi huo wa mwaka jana unaothibitisha kuwa CDM wameiacha CUF kwa mbaaaali. Kazi waliyoifanya CDM toka mwezi wa 4 hadi leo inawaweka CDM katika nafasi nzuri zaidi kuing'oa CCM. Tunaamini kama tamaa haitatawala ndani ya UKAWA na kama tunataka kuimwaga CCM mwaka huu Namtumbo, tuipe nafasi CDM sio tu kwa kuangalia ushindi wa uchaguzi mdogo bali kwa kazi waliyoifanya katika jimbo hili toka mwezi April had leo na kwa kuwa na mtia nia anayekubalika sana katika jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja zenye ushawishi kwa jamii.
Wana Namtumbo mwaka huu ni wetu kuleta mabadiliko kwani shida tulizonazo zinatokana na sisi kuikumbatia CCM. Uduni wa maisha yetu tunaweza tukauelezea sisi wenyewe, hatuhitaji mtu kutoka nje ya jimbo letu kutueleza kuwa tunaishi maisha ya dhiki. Haihitaji upotoshwaji wa aina yoyote kuwa ninyi tuna maisha bora tuliyoahidiwa kwa miaka 10. Vijana wetu, familia zetu zimekuwa zikitumikishwa na serikali kama vile hatutoi kodi. Benki Tofali ndio nini?? Mmeona wapi haya yakifanyika Ubungo kwa Mnyika, Arusha kwa Lema au Hai kwa Mbowe?? Kukaa namtumbo isiwe nongwa na sisi ni Raia wa Tanzania tunahitaji serikali inayokusanya kodi zetu ituletee maendeleo na huduma za jamii.
Angalie shida tulizonazo kutokana na serikali ya mbovu ya CCM, Maji shida, huduma za afya hovyo - hatibiwi bure mzee, mtoto wala mama mjamzito, Umeme hakuna, Barabara mbovu masoko ya Tumbaku shida, Masoko ya Ufuta shida, Michango kila kukicha. Ufisadi katika miradi ya maendeleo ni kila kijiji. Ufisadi vyama vya msingi kila kijiji. Hivi tuendelee kuwa na CCM kwa lipi hasa ndugu zangu?? Kwa elimu duni inayotupa?? Kwa kuua tumbaku? kwa kutunyima madawa? kwa kushurutishwa kufyatua tofali huku viongoz wa vijiji wakila hela za kununulia tofali?? au kwa Mbunge na madiwani wetu kushindwa kutekeleza majukumu yao??