Patriote
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 1,718
- 1,047
Napenda niwapongeze viongozi wa CHADEMA wilaya na Namtumbo na mkoa wa Ruvuma, kwa kuwasha moto jimbo la Namtumbo na kuweza kuvifikia vijiji vingi vilivyopo katika Kata 14 kati ya 19 za Wilaya hii. Moto mliouwasha katika vijiji vya kata hizi itawachukua karne CCM kuuzima.
Waliohutubia katika mikutano yenu wamesheheni hoja zenye ushawishi mkubwa, hali iliyopelekea hata wale wabishi kutoka CCM kuamua kubwaga manyanga na kurudisha kadi za CCM. Kwa asilimia kubwa wananchi wa Namtumbo sasa wametambua kuwa adui mkubwa wa maendeleo yao ni CCM na serikali yake na wameahidi kufanya mabadiliko tarehe 25/10/2015. Huku kwetu ndipo CCM ilikuwa ikijizolea kura ila kwa hali ilivyo mwaka huu, CCM wana kazi nzito sana kulichukua tena jimbo hili la Namtumbo.
Vijana wameapa kupambana na watoa rushwa wa CCM hadi mwisho. Katika hali isiyokuwa ya kawaida kundi la vijana wa kijiji cha Likusanguse katika kata ya Magazine walivamia kikao cha mtia nia wa CCM, bwana Edwin, na kupora hela aliyokuwa anagawa kama rushwa kwa waliohudhuria mkutano wake kwa lengo la kuwashawishi wampitishe kwenye kura za maoni.
Vijana wameapa kuendelea na mtindo huo hadi vitendo vya rushwa vitakapokoma. Wanawasubiri wengine waje na rushwa ili wagawane kwani wamechoshwa na vitendo vya kihuni vinavyofanywa wa watia nia wa CCM.