Chadema watumieni makamanda wenu machachari kuipeleka chadema ikulu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema watumieni makamanda wenu machachari kuipeleka chadema ikulu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Apr 27, 2011.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Wadau,
  Chadema ina bahati ya kuwa na vijana madhubuti wenye uwezo mkubwa na ushawishi mkubwa katika jamii.Miongoni mwao ni wale waliokuwa wagombea ubunge sehemu mbalimbali nchini.Ninatoa wito kwa viongozi kuwafuatilia wapambanaji hawa na kuchagua baadhi yao na kuwapa majukumu maalum ya kuongoza operesheni ya kuisimika chadema vijijini.Hakika ili kukamata dola chadema inatakiwa kuhakikisha ina matawi na mashina vijijini kote nchini.Kwa uchache ninaweza kutoa mfano kwa mgombea ubunge aliyekuwa tishio kwa CCM ndugu Nassari Joshua aliyekuwa anagombea ubunge Arumeru Mashariki.Hakika huyu ni kijana mdogo lakini mwenye ushawishi mkubwa wa hali ya juu.Ulimi wake ni silaha tosha ya kueneza sera na itikadi ya chadema.Wakati wa uchaguzi mwaka jana mgombea huyu mdogo alikuwa ni gumzo Arusha nzima na mikoa jirani kwa jinsi alivyo machachari...Viongozi tumieni silaha hizi.......
   
 2. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sio huyo tu,kuna Mtera Mwampamba,Habib Mchange,yaani timu ya Cdm imekamilika kama Real Madrid!
   
 3. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ukweli mtupu! Chadema msimwache huyu Kamanda Nassary apumzike! Ana nafasi kubwa sana ya ushawishi kwa watu wa rika zote,ukianzia na vijana, wasomi, mtaani hata kwenye taasisi mbalimbali, ninamfahamu vizuri misimamo yake toka akiwa mdogo, siyo mtu anayeogopa na wala hanunuliki, ni wakati mzuri Chadema wajipange kumtumia kuimarisha chama na kufungua matawi mapya، akiwezeshwa anaweza zaidi huyu. Hamtajuta kuwa naye
   
 4. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Lazima waanzishe mkakati wa kuwarudia wote walioshiriki vyema katika mapambano ya kuleta ukombozi wa taifa hili na wengi wao wameshindwa si kwa upungufu wa kura bali kwa kwa upungufu wa katiba na wasimamizi wa chaguzi kupendelea chama tawala kwa kuhofia kupoteza vibarua vyao
   
 5. M

  Makupa JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  CDM bado sana mnatakiwa mjipange upya, pamoja na ukweli ya kwamba uchaguzi uliopita milifurukuta , ila kutokana na jazba zenu kisiasa naamini watanzania wanaona na sio siri msingagae mwaka 2015 mambo yakawa mabaya kwenu kuliko mnavotarajia. Embu jiulizeni haya maandamano ya kuhusu maisha kuwa magumu hamjui ya kwamba baathi ya sababu ni nje ya uwezo wa serikali.Mfano swala la bei ya mafuta ni kutotakana soko la dunia kuwa na mafuta kwa uchache kuliko mahitaji . Haitaji elimu ya juu kujua hili, acheni kudanganya watanzania maskini ya kuwa cdm mna uwezo wa kuondoa kero ya ku[anda bei ya mafuta.
   
 6. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Fikiri zaidi Kabla ya Kuandika, yaani wewe umeona hivyo tu basi. fikiri ndugu yangu!
   
 7. M

  Makupa JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Wewe ndio unatakiwa kufikiri kwa maana pindi mnapoelezwa ukweli hamtaki. Sio siri mnachopigania kuwa maisha ni magumu hata nyie wana CDM hamjui chanzo zaidi ya kukurupuka .
   
 8. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kweli Ukiwa Muongo usiwe Msahaulifu! Si ni wewe ulikuja hapa jana na Kujitambulisha kama Kijana wa CDM uliyeshindwa kuchukua Fomu au. Kweli CCM wameamua kutuma Viwavi Jeshi hapa Jamvini ila kwa Mwendo huu Mtakimbia tena
   
 9. M

  Makupa JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Siku zote ukweli unauma , na msipokubali maelezo ya upande mwingine hamtafika popote.
   
 10. Antonov 225

  Antonov 225 JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni Kweli uliyosema hayaitaji elimu ya chuo, lakini haitaji elimu hata ya vidudu kujua kwamba ukubwa wa baraza la mawaziri,watumishi hewa,uchakachuaji wa mafuta,hela za epa,IPTL,Dowans na wizi wa fedha za miradi na kadhalika zinaweza kuinusuru TZ kwenye wingu la umaskini ambao hata leo hii serikali ingekuwa na uwezo wa kusema wanashusha kodi ya mafuta ili kunusuru ugumu huu wa maisha.
  -Narudia Dr Slaa amekuwa akisimamia eneo rahisi sana kwa cdm kwamba hii nchi tunaitaji UADILIFU na misingi ya haki. Hakika hata wewe utakombolewa kutoka utumwa wa mawazo ulionao
   
 11. M

  Makupa JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  UADILIFU ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu yoyote. KUMBUKA ya kwamba Dr Slaa alikuwa CCM kabla ya kutimiliwa na kujiunga na CDM, wakati akiwa mwanachama mtiifu wa CCM MBONA hatakuwahi kumskia, pili UADILIFU mnaongelea huanzia katika family level, DR wa ukweli yamemshinda ,hivyo tunachawaomba mjaribu kuwa wa kweli ya kwamaba UADILIFU mnaonglea hata hapo CDM HAUPO.
   
 12. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Kama Rais wako na Waziri mkuu wanasema hata wao hawajui kwanini maisha ni magumu, wewe ni nani ambaye unashindwa kuwauliza vioongozi wa chama chako tawala hadi unataka kuuliza CDM ambayo haijashiika dola? Au unataka wakupe siri umpelekee rais na waziri mkuu? Unashangaza ndg. Kawashauri wabunge wako kwa ushabiki wa kuzomea bungeni na kuunga mkono kila mswada unaoletwa na ccm hata kama ni wa kunyonga wananchi. Hamjui na mnajua kuwa hamjui ula hamtaki kubadilika kwa kuogopa aibu.
   
 13. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Wewe sasa unamwaibisha hata aliyekutuma, hivi Dr Slaa alitimuliwa au aliondoka mwenyewe? Na kama alitimuliwa ilikuwa kwa tuhuma gani? Inaonyesha ni jinsi gani waliokutuma hawajakupa data za kutosha kwa unayoyasema huku. Au nisikulaumu sana watakuwa wamekupa kiasi kidogo mno cha malipo. Haifiki 100,000/:
   
 14. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,757
  Trophy Points: 280
  Kwa mtazamo wako NI SAWA KUKOSA UADILIFU CCM KWA VILE CDM HAUPO..........???? Hivi hayo magamba mnayoyavua leo hii si mlipinga mara baada ya kutolewa pale mwembeyanga.................. hayo magamba ya leo si ndo mliyashika mikono na kuyainua juu wakati wa kampeni kwamba ni maadilifu.............????
   
 15. M

  Makupa JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mngekuwa na uchung wa ukweli kwa wananchi taifa hili wabunge wenu wote wangesusui posho zote ili kuthibitisha mnasimamia mnachopigia porojo.
   
 16. M

  Makupa JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Alitimuliwa na uongozi wa ccm wilaya hakuondoka kwa hiari yake
   
Loading...